Vizuizi kwenye muziki unaodaiwa

Wenye hakimiliki wanaamua jinsi wanavyotaka muziki wao utumike kwenye YouTube. Sera za wenye hakimiliki zitaathiri iwapo video yako itapatikana na jinsi itakavyopatikana. Ikiwa utatumia muziki kwenye video yako, unaweza kupata dai la Content ID likikueleza kuwa umetumia maudhui yaliyo na hakimiliki.

Haya ndiyo maelezo ya kila sera:

  • Kuchuma mapato: Mwenye hakimiliki amechagua kuchuma mapato kupitia muziki huu, hivyo matangazo yanaweza kuonekana kwenye video yako. Wakati mwingine, mwenye hakimiliki anaweza kuchagua kugawana nawe baadhi ya mapato. Hata kama sera hii imetumika, huenda video isipatikane kila mahali au kwenye vifaa vyote.
  • Kuzuia duniani kote: Mwenye hakimiliki mmoja au zaidi hawaruhusu kutumia muziki huu kwenye YouTube. Ikiwa utachagua kutumia muziki huu, video yako inaweza kuzimwa sauti au huenda isipatikane kabisa kwenye YouTube.
  • Kuzuia kwenye baadhi ya nchi au maeneo: Mwenye hakimiliki mmoja au zaidi wameweka vizuizi katika nchi au maeneo ambapo muziki huu unapatikana kwenye YouTube. Iwapo utatumia muziki huu, video yako haitaweza kutazamwa mahali ambako muziki umezuiwa kwenye YouTube.

Kumbuka: Katika hali fulani, wenye hakimiliki wanaweza kubadilisha sera zao na kutuma maombi ya kuondolewa kwa video inayokiuka hakimiliki. Hali ya video yako inaweza kubadilika wakati ujao na inaweza hata kuondolewa kwenye YouTube. Hatua ya kuondoa inaweza kutekelezwa mwenye hakimiliki anapofanya uamuzi tofauti katika suala lako binafsi. Mabadiliko katika sera inayotumika kwenye muziki huo katika video yako yanaweza pia kusababisha video kuondolewa. Pata maelezo zaidi kuhusu Content ID.

Sera hizi hazitumiki nje ya mfumo wa YouTube. Sera hizi zinaweza kutofautiana tunapoamini kwamba umepakia albamu kamili au sehemu kubwa ya albamu. Ikiwa una maswali kuhusu matumizi yako ya muziki, unaweza kuwasiliana na mwanasheria aliyehitimu.

Kupata ruhusa ya kutumia maudhui ya mtu mwingine

Iwapo unapanga kujumuisha nyenzo zinazolindwa na hakimiliki katika video yako, kwa kawaida unatakiwa kwanza uombe ruhusa. YouTube haiwezi kukupatia haki hizi. Hatuwezi kusaidia watayarishi kutafuta na kuwasiliana na wahusika ambao wanaweza kukupatia haki hizo. Ikiwa una maswali kuhusu matumizi ya nyenzo inayolindwa na hakimiliki, unaweza kuwasiliana na mwanasheria aliyehitimu.

 Maktaba ya Sauti ya YouTube ina muziki usio na mirabaha ambao watayarishi wanaweza kutumia kwenye video zao za YouTube.
 

Machaguo ya kutumia muziki katika video zako

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
7067447806373245090
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false