Mwongozo wa uendeshaji wa Mitandao ya chaneli mbalimbali (MCN)

Kuondoa vituo kwenye Mtandao wako wa Vituo Mbalimbali

Vipengele hivi vinapatikana tu kwa washirika ambao hutumia Kidhibiti Maudhui cha Studio ya YouTube. Wasiliana na Msimamizi wako wa Washirika wa YouTube ili uweze kuvitumia.

Kuondoa kituo kwenye mtandao wako

Mitandao ya Vituo Mbalimbali (MCN) inaweza kuondoa vituo kwenye mtandao wake kwa kutumia hatua hizi:

  1. Ingia katika akaunti ya Kidhibiti Maudhui cha Studio.
  2. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Vituo .
  3. Tafuta kituo unachotaka kuondoa kisha ukichague.
  4. Bofya TENGANISHA kisha THIBITISHA.

Kutuma ombi la kuondoka kwenye Mtandao wa Vituo Mbalimbali

Ikiwa wewe ni mtayarishi mshirika na unaamini kuwa mkataba wako na Mtandao wa Vituo Mbalimbali unakuruhusu kufanya hivyo, unaweza kutuma ombi la kuondoa ufikiaji wa Mtandao wa Vituo Mbalimbali kwenye kituo chako.

Kuelewa athari kwenye madai

Madai yaliyozalishwa na vipengee vya kituo yanaweza kuondolewa, kutegemea kama maelezo ya umiliki wa vipengee hivyo yamesasishwa kabla ya kituo kuondoka kwenye Mtandao wa Vituo Mbalimbali:

  • Umiliki wa vipengee ukihamishiwa kwa Mdhibiti mpya wa Maudhui kabla ya kutenganisha, madai yote huendelea kuwepo.
  • Umiliki wa vipengee ukiondolewa kabla ya kutenganisha, madai kwenye video zilizozalishwa na mtumiaji na video zilizopakiwa na kituo unachotenganisha yataondolewa. 
  • Umiliki wa vipengee usipobadilishwa kabla ya kutenganisha, madai kwenye video zilizozalishwa na mtumiaji huendelea kuwepo. Faili ya marejeleo inayohusiana na vipengee hivyo itaondolewa. Madai yote kwenye video zilizopakiwa na kituo unachotenganisha yataondolewa.

Pata maelezo zaidi kuhusu kutenganisha vituo kutoka kwa Mdhibiti wa Maudhui.

Kumbuka: Katika hali nyingine, vituo vilivyoondolewa kwenye Mtandao wako wa Vituo Mbalimbali na vituo vilivyohamishwa baina ya Wadhibiti wa Maudhui vitapoteza historia ya data ya mapato kutoka wakati vilipokuwa sehemu ya mtandao wako. Huenda vituo vikahitaji kupakua au kurekodi data ya mapato kabla ya kuondolewa au kuhamishwa. Pata maelezo zaidi kuhusu mabadiliko kwenye kipengele cha kuripoti baada ya kuhamisha umiliki wa kituo.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
7012705816253422262
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false