Jinsi YouTube inavyotathmini maudhui ya Elimu, Hali Halisi, Sayansi na Sanaa (EDSA)

Mwongozo wetu wa Jumuiya unalenga kufanya YouTube iwe jumuiya salama. Wakati mwingine, maudhui ambayo huenda yakakiuka Mwongozo wa Jumuiya yanaweza kusalia kwenye YouTube ikiwa yana muktadha wa Elimu, Hali Halisi, Sayansi au Sanaa (EDSA). Katika hali hizi, maudhui yatapata ruhusa ya EDSA ya kutofuata kanuni. Makala haya yana vidokezo kuhusu jinsi unavyoweza kuweka muktadha—maelezo zaidi yanayowafahamisha au kuwaelimisha watazamaji—katika maudhui yako ya EDSA.

Kumbuka: Kuweka muktadha kwenye maudhui yako ya EDSA si hakikisho kwamba yatapata ruhusa ya EDSA ya kutofuata kanuni.

Jinsi ambavyo maudhui hupata ruhusa ya EDSA ya kutofuata kanuni

Wakaguzi wetu wa maudhui hutathmini ikiwa maudhui yatapata ruhusa ya EDSA ya kutofuata kanuni kulingana na hali mahususi. Kwanza, tunakagua iwapo kuna ukiukaji wa Mwongozo wa Jumuiya kwenye maudhui. Iwapo kuna ukiukaji, tunakagua ikiwa kuna muktadha wa kutosha kwenye maudhui ili kutoa ruhusa ya EDSA ya kutofuata kanuni. Tunakagua ni muktadhaUPI uliopo na ni WAPI muktadha ulipo.

Ni muktadha upi wa kuweka kwenye maudhui ya EDSA

Aina ya muktadha ambao lazima ujumuishe ili kupata ruhusa ya EDSA ya kutofuata kanuni inategemea kilicho kwenye maudhui.

Huwa tunatoa ruhusa nyingi za EDSA za kutofuata kanuni wakati maudhui yana mojawapo au zaidi ya yafuatayo:

1. Hoja za msingi kuhusu kinachoendelea kwenye maudhui:: Bainisha aliye katika maudhui, eleza kinachoonyeshwa kwenye maudhui, lini au mahali ambapo tukio limefanyika au ueleze ni kwa nini maudhui fulani yapo. 

Mifano ya hoja za msingi

Hoja za msingi zinasaidia sana haswa wakati maudhui ni ya vurugu au ya kuogofya au yanaonyesha uchi au ngono. Maudhui haya yanaweza kuwa na madhara kidogo kwa watazamaji kukiwa na muktadha.

Mifano hii inaonyesha maudhui ambayo yana uwezekano mkubwa na uwezekano mdogo kupata ruhusa ya EDSA ya kutofuata kanuni: 

Uwezekano mkubwa wa kupata ruhusa ya EDSA ya kutofuata kanuni

Uwezekano mdogo wa kupata ruhusa ya EDSA ya kutofuata kanuni

Video ya usalama inayoonyesha waathiriwa wa wizi wa kimabavu wakijeruhiwa iliyo na maelezo kwenye video. Maelezo yanaweza kujumuisha mahali na wakati ambapo uhalifu ulifanyika na kwa nini video imechapishwa.

Video ya usalama ambayo inaonyesha waathiriwa wa wizi wa kimabavu wakijeruhiwa iliyo na emoji, kama vile 😆 au 😲, zilizopachikwa kwenye picha.

Video ya upasuaji inayoonyesha vidonda pamoja na maelezo kwenye video. Maelezo yanaweza kujumuisha aina ya upasuaji unaofanyika na sababu za kufanyika.

Video ya upasuaji inayoonyesha vidonda iliyo na jina au maelezo yanayosema kwamba "zitatisha" au "kuogofya" mtazamaji.

Maudhui yenye uchi kidogo ambao ni sehemu ya kazi ya maigizo, ambapo maudhui ya uchi yanaonyeshwa katika muktadha wa hadithi ndefu.

Video fupi za uchi zilizotolewa kwenye filamu mbalimbali za mambo halisi zilizo na maneno yenye lugha chafu yaliyowekelewa.

Video ya vurugu ambapo watu wanapata majeraha yanayoweza kusababisha kifo ambayo ina taarifa za waliohusika kuitayarisha inayowajulisha watazamaji kwamba vurugu ni sehemu ya tendo la uigizaji.

Video ya vurugu ambapo watu wanapata majeraha yanayoweza kusababisha kifo ambapo mtazamaji wa kawaida hawezi kusema ikiwa vurugu hii ni halisi au sehemu ya tendo la uigizaji.

 

2. Shutuma, mitazamo ya kupinga au tashtiti: Tangaza kwamba maudhui yako yanashutumu madai fulani, yanajumuisha mitazamo ya kupinga au yana tashtiti.

Mifano ya shutuma, mitazamo ya kupinga au tashtiti

Msisitizo wa shutuma, mitazamo ya kupinga au tashtiti ni muhimu hasa wakati mada ya maudhui ni matamshi ya chuki au maelezo ya kupotosha. Maudhui fulani yanaweza kuwa ya kupotosha yenyewe, lakini yanaweza kuwa na athari kidogo kwa watazamaji kunapokuwa na muktadha. Muktadha unaweza kujumuisha kukashifu mambo ya chuki au kukosoa madai ya uongo kwa kuangazia maoni kutoka vyanzo vya kuaminika kama vile mamlaka za afya au za uchaguzi.
Mifano hii inaonyesha maudhui ambayo yana uwezekano mkubwa na uwezekano mdogo kupata ruhusa ya EDSA ya kutofuata kanuni:

Uwezekano mkubwa wa kupata ruhusa ya EDSA ya kutofuata kanuni

Uwezekano mdogo wa kupata ruhusa ya EDSA ya kutofuata kanuni

Maudhui ambapo mtu anatoa dai la uongo kwamba watu ambao wana umri wa zaidi ya miaka fulani hawakubaliwi kupiga kura katika uchaguzi wa kidemokrasia. Maudhui haya pia yanafafanua kwamba dai ni la uongo.

Maudhui ambapo mtu anatoa dai la uongo kwamba watu ambao wana umri wa zaidi ya miaka fulani hawakubaliwi kupiga kura katika uchaguzi wa kidemokrasia bila muktadha zaidi.

Maudhui ambapo mtu anatoa madai ya uongo kwamba chanjo za COVID-19 zina chipu ndogo na mkosoaji wake anasema kwamba dai ni la uongo.

Maudhui ambapo mtu anadai kwamba chanjo zilizoidhinishwa za COVID-19 zina chipu ndogo bila muktadha zaidi.

Maudhui yanayonukuu mtu anayetoa wito wa vurugu dhidi ya kikundi kwa misingi ya mbari zao. Maudhui yanakosoa na kukemea vitendo vya mtu huyo.

Maudhui ambapo mtu anatoa wito wa vurugu dhidi ya kikundi kwa misingi ya mbari yao bila muktadha zaidi au yenye jina au maelezo yanayochochea vurugu.

 

3. Kupinga tabia hatarishi: Kuwaambia watazamaji wasiige kilicho kwenye video.

Mifano ya kupinga tabia hatarishi

Hatua ya kupinga uigaji husaidia kupunguza uwezekano wa madhara kwa watazamaji na jumuiya ya YouTube. Hatua hii ni muhimu hasa wakati maudhui yanaonyesha vitendo ambavyo vina madhara au ni hatari au wakati maudhui yanahusiana na kujijeruhi. Kumbuka kuwa hiki si kibali cha kuhimiza au kutenda tabia hatari. Kusema tu, "Usijaribu hili ukiwa nyumbani" huenda hakutasababisha kupata ruhusa ya kutofuata kanuni ikiwa hakuambatani na maelezo kuhusu uwezekano wa madhara.
Mifano hii inaonyesha maudhui ambayo yana uwezekano mkubwa na uwezekano mdogo kupata ruhusa ya EDSA ya kutofuata kanuni:

Uwezekano mkubwa wa kupata ruhusa ya EDSA ya kutofuata kanuni

Uwezekano mdogo wa kupata ruhusa ya EDSA ya kutofuata kanuni

Maudhui yanayoonyesha mzaha wa uvamizi wa nyumbani na maudhui yanamfahamisha mtazamaji asiige shughuli hii hatari kwa sababu inaweza kusababisha madhara ya kimwili au ya kihisia.

Maudhui yanayoonyesha mzaha wa uvamizi wa nyumbani au video ya maoni kuhusu mzaha wa uvamizi wa nyumbani. Kucheka au kuitikia kitendo hatarishi huenda kusitoshe kupunguza uwezekano wa madhara kwa mtumiaji anayekiiga.

Maudhui yanayoonyesha tukio hatari la madaha barabarani linaloweza kujeruhi watazamaji. Maudhui yanafahamisha mtazamaji asiige tukio la madaha kwa sababu ya madhara makubwa yanayoweza kutokea au yanapendekeza usimamizi wa kitaalamu.

Maudhui yanayoonyesha tukio la madaha barabarani linaloweza kujeruhi watazamaji bila muktadha zaidi.

 

Kumbuka: Mifano iliyo hapo juu si orodha kamili ya muktadha unaoweza kuweka kwenye maudhui yako ya EDSA. Ukiwa huna uhakika, weka aina nyingi za muktadha kwenye maudhui yako ya EDSA. Ili usaidie kuzuia maudhui kusababisha madhara, jumuisha taarifa kwenye video yako, si tu jina au maelezo ya video yako.

Ukiwa huna uhakika, jumuisha aina mbalimbali za miktadha zilizoelezewa hapo juu: maelezo ya msingi ya kweli yanayoelezea kilicho kwenye maudhui yako, mitazamo mbalimbali na kupinga wazi na kupinga kwa kuelemisha dhidi ya kuiga tabia hatarishi na zenye madhara. Hakikisha kuwa unajumuisha maelezo kwenye maudhui yenyewe, kama vile video au sauti, ili kusaidia kuepuka uwezekano wa maudhui kusababisha madhara. 

Tunaweza kuweka mipaka ya umri au onyo kwenye maudhui hata yakipata ruhusa ya EDSA ya kutofuata kanuni kwa sababu baadhi ya watazamaji huenda wakayaona kuwa nyeti au yasiyofaa (kwa mfano video ya eneo la vita). Katika hali fulani, tunaweza kutoa ruhusa za EDSA za kutofuata kanuni kulingana na maslahi ya umma. Hali hizi zinaweza kujumuisha, kwa mfano, maudhui kama wagombea viti vya kisiasa wa kitaifa wakiwa katika kampeni, video ya kuogofya kutoka maeneo ya vita au migogoro ya kibinadamu, maoni yanayopinga mwongozo wa mamlaka ya afya yaliyotolewa wakati wa kusikilizwa kwa kesi hadharani, au maudhui ya uchi kwenye muktadha wa elimu ya ngono.

MAHALI pa kuweka muktadha kwenye maudhui yako ya EDSA

Unaweza kuweka muktadha kwenye:

  • Video
    • Kwa mfano unaweza kuweka video au kuwekelea maandishi.
  • Sauti
    • Kwa mfano unaweza kuweka kidokezo ukijumuisha mtazamo wa kukemea au kinzani.
  • Jina la video
  • Maelezo ya video
Kumbuka: Hatutoi ruhusa za EDSA za kukiuka kanuni kwa muktadha ambao huenda uko kwenye maoni, lebo, maelezo ya chaneli, maoni yaliyobandikwa au mifumo mingine. Maudhui hayo hayaonekani kila wakati kwa watazamaji.
Muhimu: Katika maudhui yenye hatari kubwa ya kudhuru, tunahitaji muktadha kwenye VIDEO au SAUTI. Video na sauti ni sehemu ya maudhui ambapo watazamaji wanaweza kupata muktadha, pamoja na wakati maudhui yamepachikwa kwenye tovuti au programu nyingine. Maudhui ambapo tunahitaji muktadha kwenye sauti au video ili kutoa ruhusa ya EDSA ya kutofuata kanuni yanajumuisha maudhui yanayohusiana na matamshi ya chuki, mashirika hatari ya uhalifu, usalama wa watoto, kujiua na kujijeruhi na vurugu ya kuogofya.

Na aina nyingine za maudhui, kama maoni je?

Sera na mwongozo unaotumika kwenye video pia ndio unaotumika kwenye aina zingine za maudhui.

Maudhui yasiyopata ruhusa za EDSA za kukiuka kanuni

Maudhui fulani hayakubaliwi kwenye YouTube, hata yakiwa na muktadha. Usichapishe:

  • Maudhui yanayoonyesha unyanyasaji wa watoto kingono (CSAM)
  • Video, picha za kawaida au sauti ya unyanyasaji mkali wa kingono wa kimwili
  • Video zilizorekodiwa na mtendaji wa tukio hatari au kubwa la vurugu ambalo linaonyesha silaha, vurugu au waathiriwa waliojeruhiwa
  • Upakiaji upya wa maudhui ghafi yaliyotayarishwa na au yanayohimiza mashirika ya kihalifu au kigaidi
  • Maagizo kuhusu jinsi ya kushiriki katika kitendo cha kujijeruhi au kufa kwa kujiua
  • Maagizo kuhusu jinsi ya kutengeneza bomu kwa lengo la kuwajeruhi au kuwaua wengine
  • Maagizo ya jinsi ya kutengeneza bunduki au vifaa vilivyopigwa marufuku
  • Ofa za mauzo yasiyoruhusiwa
  • Maagizo kuhusu jinsi ya kutumia kompyuta au teknolojia ya habari kuhatarisha data binafsi au kusababisha madhara makubwa kwa watu wengine
  • Maudhui yanayoonyesha taarifa ya faragha ya mtu, kama vile anwani yake ya nyumbani, anwani za barua pepe, kitambulisho cha kuingia katika akaunti, namba za simu, namba ya pasipoti au taarifa za akaunti ya benki (upekuzi na utangazaji wa taarifa binafsi)
  • Ponografia dhahiri
  • Maudhui taka

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
17259341840794528944
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false