Kudhibiti mapendekezo na matokeo yako ya utafutaji

Kuna njia kadhaa za kuboresha matokeo ya utafutaji na mapendekezo yako ya YouTube. Unaweza kuondoa video mahususi kwenye historia ya video ulizotazama na mambo uliyotafuta kutoka kwenye historia ya mambo uliyotafuta. Unaweza pia kuzima historia ya video ulizotazama na ya mambo uliyotafuta au uanze upya kwa kufuta historia ya mambo uliyotafuta na ya video ulizotazama.

Iwapo hutaki kuona mapendekezo kwenye ukurasa wa kwanza, unaweza kufuta na kuzima historia ya video ulizotazama.

Historia ya video ulizotazama na historia ya mambo uliyotafuta

  • Kuondoa video mahususi kwenye historia ya video ulizotazama: Ukiona unapendekezewa mada ambayo hupendezwi nayo, jaribu kuondoa video ambayo ulitazama awali kuhusu mada hiyo. Hatua hii inaweza kupunguza uwezekano wa kupata mapendekezo sawa katika siku zijazo.
  • Kuondoa utafutaji mahususi kwenye historia ya video ulizotazama: Ukiona unapendekezewa mada isiyokuvutia, jaribu kuondoa video uliyoitazama awali kuhusu mada hiyo. Hatua hii inaweza kupunguza uwezekano wa kupata mapendekezo sawa katika siku zijazo.
  • Kuzima historia: Unaweza kuzima historia ya video ulizotazama na mambo uliyotafuta ikiwa hutaki video ulizotazama au mambo uliyotafuta yashawishi mapendekezo na matokeo ya utafutaji utakayopata siku zijazo. Kwa mfano, unapotafiti mada ya mradi wa shule ambayo wewe binafsi haikuvutii. Kumbuka kuendeleza kurekodi historia ya shughuli zako ukimaliza.
  • Kufuta historia: Iwapo historia nzima ya video ulizotazama na mambo uliyotafuta haihusiani na mambo yanayokuvutia, unaweza kufuta historia ya video ulizotazama na mambo uliyotafuta. Kidokezo: Iwapo unataka kutumia historia ya video ulizotazama ili kurudia kutazama baadhi ya video, jaribu kuweka video hizo kwenye orodha ya kucheza au ya "Tazama Baadaye" ili uweze kuzipata tena.

Kuboresha mapendekezo yako

Televisheni zinazoweza kuunganisha kwenye intaneti, vifaa vya kutiririsha au vifaa vya michezo ya video

Kuondoa maudhui yanayopendekezwa kwenye ukurasa wa kwanza

Unaweza kuondoa video zinazopendekezwa kwa kuchagua “Hainivutii” kwenye ukurasa wako wa kwanza au katika ukurasa wa Mwanzo na ukurasa wa Tazama Inayofuata kwenye televisheni zinazoweza kuunganisha kwenye intaneti, vifaa vya kutiririsha au vifaa vya michezo ya video:

  1. Nenda kwenye video inayopendekezwa ambayo ungependa kuondoa.
  2. Bonyeza na ushikilie kitufe cha kuchagua kwenye kidhibiti chako cha mbali.
  3. Chagua Hainivutii.
  4. Chagua Tueleze ni kwa nini ili ushiriki sababu yako ya kutaka video iondolewe. Unaweza kuchagua Tayari nimetazama video, Sipendezwi na video au Usipendekeze kituo ili utusaidie kukupendekezea video zinazokufaa zaidi.

Futa maoni yako ya “Hainivutii" na “Usipendekeze kituo”

Maoni yako ya “Hainivutii” na “Usipendekeze kituo” yanaweza kutumika kuweka mapendeleo kwenye mapendekezo yako. Ili ufute maoni yote uliyotoa ya “Hainivutii” na “Usipendekeze kituo”, tafadhali fuata maagizo hapa chini ukitumia kompyuta, Android, au iPhone au iPad yako.

Mapendekezo kutokana na Shughuli zako kwenye Google

YouTube inaweza pia kutumia data inayotokana na Shughuli za Akaunti yako ya Google ili kukupatia mapendekezo, matokeo ya utafutaji, arifa za ndani ya programu na video unazopendekezewa katika sehemu nyinginezo.

Unaweza kuangalia na kudhibiti shughuli zako katika myactivity.google.com. Pata maelezo zaidi kuhusu kudhibiti shughuli za Akaunti yako ya Google.

Chagua mada kwenye mapendekezo yako

Ukiwa umeingia katika akaunti, utaona mada kwenye Ukurasa wa kwanza na kurasa za kutazama ili kukusaidia kuchuja mapendekezo yako. Mada hizi zinatokana na mapendekezo yako yaliyopo, yaliyowekewa mapendeleo. Mada hizi pia hulingana na maudhui yanayohusiana na yale unayotazama. Mada hizi zinakusudiwa kukusaidia upate maudhui unayotaka kutazama kwa haraka zaidi.

Ukipata video ambayo haihusiani na mada uliyochagua kwenye Ukurasa wa kwanza, tujulishe kwa kugusa Zaidi '' kisha Si <mada> .

Topic filters are found on the home page, near the top.

Kuondoa maudhui yanayopendekezwa kwenye ukurasa wa kwanza

Iwapo huwezi kufuata maagizo haya, huenda unatumia toleo la awali la YouTube. Iwapo unatumia kivinjari kipya, sasisha ili utumie toleo jipya la YouTube.

Maudhui yafuatayo yanayopendekezwa yanaweza kuondolewa kwenye ukurasa wa kwanza kwenye kompyuta yako:

  • Video
  • Vituo
  • Sehemu
  • Orodha za kucheza

Ili kuondoa video inayopendekezwa kwenye ukurasa wako wa kwanza:

  1. Elekeza kwenye video inayopendekezwa au alama ya X kwenye sehemu ambayo ungependa kuondoa.
  2. Chagua Zaidi '' karibu na jina la video au orodha ya kucheza.
  3. Chagua Hainivutii   ili kuondoa video kwenye mipasho yako.
  4. Chagua Tueleze sababu ili ushiriki ni kwa nini ungependa video iondolewe. Unaweza kuchagua Tayari nimetazama video au Sijapendezwa na video ili ufanye mapendekezo yakufae zaidi.

Unaweza pia kuhakikisha kuwa video kutoka kwenye vituo mahususi hazionekani katika mapendekezo yako. Chagua menyu, kisha Usipendekeze kituo

Futa maoni ya “Hainivutii" na “Usipendekeze kituo”

Maoni yako ya “Hainivutii” na “Usipendekeze kituo” yanaweza kutumika kuboresha mapendekezo yako. Ili ufute maoni yote uliyotoa ya “Hainivutii” na “Usipendekeze kituo”:

  1. Tembelea ukurasa wa Shughuli Zangu. Huenda ukahitaji kuingia katika Akaunti yako ya Google.
  2. Pata Shughuli zingine za Google katika Menyu ya upande wa kushoto au chini ya bango la Shughuli Zangu.
  3. Chagua "maoni ya 'Hainivutii' kwenye YouTube," kisha uchague Futa.

Angalia makala yetu mengine kwa maelezo zaidi kuhusu historia ya video ulizotazama, historia ya mambo uliyotafuta na uboreshaji wa mapendekezo yako.

Mapendekezo kutokana na Shughuli zako kwenye Google

YouTube inaweza pia kutumia data inayotokana na Shughuli za Akaunti yako ya Google ili kukupatika mapendekezo, matokeo ya utafutaji, arifa za ndani ya programu na video zilizopendekezwa katika sehemu nyinginezo.

Unaweza kuangalia na kudhibiti shughuli zako katika myactivity.google.com. Pata maelezo zaidi kuhusu kudhibiti shughuli za Akaunti yako ya Google.

Kudhibiti video ulizopenda

Mapendekezo na matokeo ya utafutaji wako pia yanatokana na video ulizopenda. Unaweza kupenda, kuweka alama kuwa haijakupendeza na kuondoa video ulizopenda ili kushawishi mapendeleo na matokeo ya utafutaji wako.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
17554052178679224739
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false