Kuchangia shirika lisilo la faida kupitia Uhisani wa YouTube

Uhisani wa YouTube unalenga kusaidia kuimarisha njia ambazo watayarishi na mashabiki hushirikiana kupitia michango ya uhusani kwenye YouTube. Baadhi ya video na mitiririko mubashara hukupa chaguo la kuchangia shirika lisilo la faida ambalo mtayarishi wa video analisaidia.

YouTube hulipia ada zote za miamala, kwa hivyo asilimia 100 ya pesa zote unazochanga hutumwa kwa shirika lisilo la faida linalostahiki. Huwezi kurudishiwa pesa unazochangia kwenye mashirika yasiyo ya faida. Soma sehemu yetu ya Maswali Yanayoulizwa Sana kuhusu Uhisani wa YouTube ili upate maelezo zaidi.

Jinsi ya kuchanga

Kitufe cha kuchanga

Baadhi ya watayarishi huwa na vitufe vya kuchanga karibu na video na mitiririko yao mubashara. Ili uchange, fuata hatua zilizo hapa chini.

Nenda kwenye video iliyo na kitufe cha kuchanga, kisha:

  1. Chagua CHANGA.
  2. Chagua kiasi cha pesa ambazo ungependa kuchangia kisha ENDELEA.
  3. Chagua njia ya kulipa.
  4. Bofya CHANGA kisha NIMEMALIZA.

Shirika lisilo la faida na mtayarishi wa YouTube hawataona taarifa zako binafsi.

Utatumiwa risiti kwa njia ya barua pepe baada ya malipo yako kuchakatwa.

Michango ya Gumzo la Moja kwa Moja

Kipengele cha Michango ya Gumzo la Moja kwa Moja kimechukua nafasi ya Super Chat for Good katika michango ya gumzo la moja kwa moja. Mtayarishi anapochangisha pesa kwenye mtiririko mubashara na amewasha gumzo la moja kwa moja, utaona kitufe cha kuchanga katika gumzo hilo.

Ili kuchanga:

  1. Chagua Changa ndani ya gumzo la moja kwa moja. Ni lazima vifaa vya mkononi viwe katika mkao wima ili uone gumzo la moja kwa moja.
  2. Chagua kiasi unachotaka kuchanga au uchague Nyingine ili uweke thamani tofauti.
  3. Chagua Ningependa mchango wangu uonekane hadharani ili uonyeshe jina lako la mtumiaji katika gumzo la moja kwa moja. Vinginevyo, kiasi cha mchango wako kitaonekana kama “Haujatambulishwa.”
  4. Chagua CHANGA.
  5. Ili ukamilishe mchango wako, fuata maagizo yaliyo kwenye skrini.
Kumbuka: Iwapo hungependa jina lako la mtumiaji lionekane karibu na mchango wako, batilisha uteuzi wa kisanduku karibu na Ningependa mchango wangu uonekane hadharani.

Utatumiwa risiti kwa njia ya barua pepe baada ya malipo yako kuchakatwa.

Taarifa za kodi kuhusu mchango wako

Pata maelezo kuhusu taarifa za kodi katika Kituo cha Usaidizi wa Michango.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
11420252030517448079
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false