Ghairi uanachama wako unaolipiwa

Wateja waliosajiliwa wa YouTube Premium na YouTube Music Premium wanaweza kughairi, kusitisha au kuendelea kutumia uanachama wakati wowote katika kipindi chao cha uanachama unaolipiwa. Unaweza pia kubadilisha ili utumie mpango wa mwaka au mpango wa familia.

Bofya kitufe kilicho hapa chini ili uone na udhibiti uanachama wako unaolipiwa. Kisha, fuata hatua zilizo kwenye makala haya ili ughairi uanachama wako wa YouTube Premium au YouTube Music Premium.

Ikiwa ulifanya ununuzi kwa kutumia iPhone au iPad yako au ulijisajili katika uanachama wa YouTube unaolipiwa kupitia Apple, utahitaji kuwasiliana na huduma ya usaidizi ya Apple ili uombe kurejeshewa pesa. Sera ya Apple ya kurejesha pesa itatumika.

Unaweza kughairi uanachama wako wakati wa kipindi cha kujaribu. Ikiwa utaamua kughairi, uanachama wako wa mpango wa jaribio hautatumika kwenye usajili unaolipiwa mwisho wa kipindi cha kujaribu. Utaendelea kutumia usajili hadi mwisho wa kipindi cha kujaribu

Kughairi uanachama wako unaolipiwa

 

Ikiwa umejisajili kwenye huduma ya malipo kupitia Google Play, pata maelezo ya jinsi ya kughairi uanachama wako hapa.

  1. Nenda kwenye youtube.com/paid_memberships.
  2. Bofya Dhibiti uanachama.​
  3. Bofya Zima.
  4. Gusa Endelea ili ughairi.
  5. Chagua sababu yako ya kughairi kisha ubofye endelea.
  6. Bofya Ndiyo, ghairi.

GHAIRI SASA

How to cancel your YouTube Premium or YouTube Music Premium membership

Unatatizika kughairi?

Angalia ikiwa mojawapo ya mambo yafuatayo yanakuhusu:
  1. Unatozwa na Apple. Ikiwa ulijiunga kwa kutumia programu ya YouTube ya iOS, unaweza kughairi uanachama wako unaolipiwa kwenye akaunti yako ya Apple.
  2. Unatozwa na Google Play. Ikiwa unaweza kufikia uanachama wako unaolipiwa wa YouTube kupitia usajili wa Google Play, unaweza kughairi kwenye mipangilio ya akaunti yako ya Google Play.
  3. Umeshaghairi. Unaweza kuthibitisha kwa kuangalia sehemu ya uanachama unaolipiwa ya akaunti yako kwenye youtube.com/paid_memberships.
Vidokezo:

Unapokuwa mwanachama anayelipia wa YouTube, utatozwa kiotomatiki bei ya uanachama mwanzoni mwa kila kipindi cha kutozwa hadi utakapoghairi.

Unapoghairi uanachama wako, hutatozwa tena usipojisajili upya. Utaendelea kupata manufaa yako ya uanachama unaolipiwa wa YouTube hadi mwisho wa kipindi cha bili.

Marejesho ya pesa za ununuzi uliofanywa kwenye Duka la Google Play

Ukipokea YouTube Premium kupitia usajili wa Pixel Pass, pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kudhibiti akaunti yako hapa.
Kuanzia mwaka wa 2022, wateja wapya wa YouTube Premium na YouTube Music Premium waliojisajili kupitia kifaa cha Android watatozwa kupitia Google Play. Wateja ambao tayari wamesajiliwa hawaathiriwi na mabadiliko haya. Unaweza kutembelea payments.google.com ili uone utozaji wa hivi karibuni na uangalie jinsi unavyotozwa. Ili utume ombi la kurejeshewa pesa za ununuzi uliofanya kwenye Google Play, fuata hatua zilizoainishwa hapa.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
9243035233711442283
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false