Vifaa vinavyotumia YouTube Premium na YouTube Music Premium

Ikiwa una YouTube Premium au YouTube Music Premium, manufaa ya uanachama wako yanapatikana kwenye vifaa vyote vinavyoweza kufikia YouTube. Pata maelezo zaidi kuhusu uanachama wetu wa YouTube unaolipiwa.

Vifaa vya mkononi

  • Manufaa yote ya YouTube Premium na Music Premium—kama vile video bila matangazo, uchezaji wa chinichini na zaidi—yanapatikana kwenye programu ya vifaa vya mkononi ya YouTube na programu ya YouTube Music.
  • Sasisha upate toleo jipya kabisa la programu ya YouTube au YouTube Music ili uhakikishe kuwa unaweza kupata manufaa yote ya mwanachama wa YouTube Premium.

Vifaa vilivyounganishwa kwenye televisheni

Ukiwa mwanachama wa YouTube Premium, unaweza kutazama video bila matangazo na YouTube Originals kwenye televisheni yako. Manufaa yako ya YouTube Premium yanapatikana kwenye kifaa chochote cha kutiririsha, televisheni inayoweza kuunganisha kwenye intaneti au kifaa cha michezo ya video ambacho umetumia kuingia katika programu ya YouTube.

Vidokezo:
  • Programu ya YouTube Music haipatikani kwenye vifaa vya sebuleni.
  • Uchezaji wa chinichini na nje ya mtandao unapatikana tu kwenye programu za vifaa vya mkononi za YouTube, YouTube Kids na YouTube Music. Pata maelezo zaidi kuhusu kutumia manufaa ya YouTube Premium.
  • Hakikisha kuwa una toleo jipya kabisa la programu ya YouTube na umeingia katika ukitumia akaunti yako ya YouTube Premium.

Vifaa vya kutiririsha muziki

  • Chromecast ya Sauti kwenye programu ya YouTube Music: Wanachama wa Premium wanaweza kucheza faili za sauti katika programu ya YouTube Music kwenye vifaa vya Chromecast ya Sauti au spika zilizounganishwa kwenye Google Cast.

Vivinjari vinavyotumika

Chromecast

Miundo ifuatayo ya Chromecast hairuhusu kuingia moja kwa moja katika akaunti ya YouTube kwenye TV: 

  • Ultra
  • Toleo la tatu
  • Toleo la pili
  • Toleo la kwanza

Ili kutuma video za YouTube kwenye TV yako ukitumia Chromecast:

  1. Ingia katika akaunti yako ya YouTube Premium ukitumia kifaa cha mkononi.
  2. Unganisha kifaa chako kwenye TV yako ukitumia aikoni ya .
  3. Tumia kifaa chako cha mkononi kuvinjari na kuchagua video nyingine za YouTube.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
525887779537230144
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false