Unaweza tu kubadilisha lugha ya video uliyopakia. Pata maelezo kuhusu jinsi ya kuangalia manukuu yanayopatikana unapotazama video katika lugha tofauti.
Mipangilio ya lugha ya video ni kipengele kinachotumiwa kusaidia YouTube na wachangiaji kuelewa lugha ya asili ya video yako. Kipengele hiki husaidia unapoweka manukuu kwenye video za YouTube. Pia kinatumiwa kuwasaidia watazamaji kupata video kwa lugha zao.
Kubadilisha lugha ya video
Unaweza kubadilisha lugha ya video uliyopakia ikiwa haijawekwa kwa usahihi:
- Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube
.
- Kwenye menyu ya kushoto, chagua Maudhui
.
- Bofya jina au kijipicha cha video.
- Sogeza chini kisha ubofye ONYESHA ZAIDI.
- Chini ya "Lugha na uthibitishaji wa manukuu", chagua lugha iliyokusudiwa ya video yako, jina na maelezo yake.
- Unaweza pia kubadilisha manukuu ya video yako. Pata maelezo kuhusu jinsi ya kubadilisha lugha ya manukuu ya video yako.
- Ili uhifadhi mabadiliko uliyoyafanya, bofya kitufe cha HIFADHI katika sehemu ya juu ya ukurasa.
Kumbuka: Ukibadilisha mipangilio ya lugha asili ya video yako, manukuu ya baadaye yatakayotafsiriwa yatatumia lugha mpya kama lugha chanzo ya tafsiri. Manukuu yako ya rasimu na yaliyochapishwa hayataathiriwa.