Kuwa mwanachama katika chaneli kwenye YouTube

Uanachama katika chaneli kwenye tovuti kuu na programu ya YouTube unakuwezesha kununua beji zinazoonekana hadharani, emoji na kufikia marupurupu yanayotolewa na mtayarishi kwenye chaneli.

Huenda gharama za uanachama zikatofautiana kulingana na mfumo unaotumia na nchi unayoishi.

Kumbuka: Kuanzia mwezi Januari 2022, baadhi ya watumiaji ambao watajiunga kama wanachama katika chaneli kwa kutumia programu ya Android ya YouTube katika Android watatozwa kupitia Google Play. Hatua hii haitaathiri bei au gharama, itaathiri tu sehemu ambako ununuzi unatozwa. Unaweza kutembelea pay.google.com ili uone gharama za hivi karibuni na uangalie jinsi unavyotozwa.
 

Kujiunga, kubadilisha viwango au kughairi uanachama

Kuwa mwanachama katika kituo

Jiunge na uanachama katika kituo kinachoshiriki, kupitia programu na tovuti kuu ya YouTube.
  1. Tembelea youtube.com au fungua programu ya YouTube.
  2. Nenda kwenye kituo au video iliyopakiwa na mtayarishi ambaye ungependa kumuunga mkono kisha uone iwapo amewasha uanachama kwenye kituo chake.
  3. Bofya Jiunge.
  4. Fuata vidokezo ili uweke maelezo yako ya malipo.
  5. Bofya Nunua.

Baada ya kukamilisha muamala wako, utaona ujumbe wa kukukaribisha.

Kubadilisha kiwango chako cha uanachama

Kuongeza kiwango

  1. Nenda kwenye ukurasa wa kwanza wa kituo cha uanachama unaotaka kubadilisha kisha bofya Angalia manufaa.
  2. Chagua kiwango unachotaka kujiunga kisha Badilisha kiwango.
  3. Chagua Ongeza Kiwango.
  4. Baada tu ya ununuzi utafikia kiwango kilichosasishwa.
    1. Dokezo la bei: Utatozwa tu tofauti ya bei kati ya viwango vya uanachama, kulingana na bei iliyorekebishwa kwa siku zilizosalia kwenye kipindi chako cha kutozwa cha hapo awali.
    2. Kwa mfano: Ikiwa unalipa $4.99 na ukapandisha daraja la uanachama ili ufikie kiwango cha $9.99, huku ukiwa umebakiza nusu mwezi hadi malipo yako yanayofuata, utatozwa ($9.99-$4.99) X (0.5)= $2.50 kwa kipindi kilichobaki kwenye mwezi.
  5. Tarehe yako ya malipo ya kila mwezi haitabadilika kutokana na kuongeza kiwango.

Kushusha kiwango

  1. Nenda kwenye ukurasa wa kwanza wa kituo cha uanachama unaotaka kubadilisha kisha bofya Angalia manufaa.
  2. Chagua kiwango unachotaka kujiunga kisha  Badilisha kiwango.

Maelezo ya malipo na ufikiaji kwa wanachama walioshusha viwango

  • Tarehe yako ya malipo ya kila mwezi haitabadilika kutokana na kushusha kiwango.
  • Utaweza kufikia kiwango chako halisi hadi itakapofika tarehe yako inayofuata ya malipo.
  • Utatozwa bei mpya ya chini ifikapo tarehe yako inayofuata ya malipo.
  • Utaendelea kubaki na zawadi za kutuza uaminifu ulizojipatia kama inavyoonyeshwa kwenye beji yako, ikiwa mtayarishi anatoa.

Utaendelea kubaki na zawadi za kutuza uaminifu ulizojipatia kama inavyoonyeshwa kwenye beji yako, ikiwa mtayarishi anatoa.

Kughairi uanachama katika kituo
Fungua skrini ya udhibiti wa uanachama kwa kubofya Angalia manufaa kwenye ukurasa wa kwanza wa kituo kisha chagua kisha bofya Sitisha uanachama na manufaa.
Pia, unaweza kughairi uanachama wako wakati wowote kwenye kompyuta kwa kufuata hatua hapa chini:
  1. Ingia katika akaunti ya YouTube.
  2. Nenda kwenye youtube.com/paid_memberships.
  3. Tafuta uanachama katika kituo ambao ungependa kughairi kisha bofya Dhibiti uanachama.
  4. Chagua ZIMA.
  5. Chagua SITISHA UANACHAMA.
  6. Utaona skrini ya uthibitisho wa kughairi.

Iwapo unatatizika kughairi uanachama wako, pata maelezo zaidi hapa.

Kununua Uanachama Unaotolewa kama Zawadi
Uanachama unaotolewa kama zawadi unapatikana tu kwenye chaneli zinazoshiriki kwa ajili ya kutumia ofa au ununuzi. Watazamaji wanaweza kujijumuisha na kupata zawadi wakitumia wavuti au vifaa vya Android au iOS.

Uanachama unaotolewa kama zawadi unawawezesha watazamaji kuwanunulia watazamaji wengine fursa ya kufikia manufaa ya uanachama katika chaneli kwa kipindi cha hadi mwezi mmoja. Ili ununue uanachama unaotolewa kama zawadi, lazima uwe unatazama mtiririko mubashara au Onyesho la kwanza kwenye chaneli ambayo kipengele cha Kuzawadi kimewashwa.

Uanachama unaotolewa kama zawadi unapatikana kwenye mitiririko mubashara na Maonyesho ya kwanza kwenye chaneli zinazotimiza masharti. Ikiwa uanachama unaotolewa kama zawadi unapatikana kwenye chaneli husika, unaweza kununua uanachama unaotolewa kama zawadi wakati wa mtiririko mubashara au Onyesho la kwanza:

  1. Tumia kompyuta ili uingie katika akaunti ya YouTube.
  2. Nenda kwenye chaneli inayotimiza masharti ambapo unataka kununua uanachama unaotolewa kama zawadi.
  3. Jiunge na mtiririko mubashara au Onyesho la kwanza la chaneli.
  4. Katika gumzo la moja kwa moja, bofya .
  5. Bofya Zawadi za uanachama .
  6. Chagua idadi ya watazamaji unaotaka kuwapatia uanachama unaotolewa kama zawadi.
  7. Kamilisha muamala.

Uanachama unaotolewa kama zawadi hutolewa katika kiwango cha karibu cha juu zaidi cha bei kinachopatikana, hadi na ikiwa ni pamoja na $5.

Baada ya kununua uanachama unaotolewa kama zawadi, sehemu ya gumzo inayohesabu muda uliosalia itaangazia kwa muda mfupi ununuzi wako katika gumzo la moja kwa moja. Muda ambao ununuzi wako utaangaziwa utategemea gharama. Mtayarishi anaweza kumaliza gumzo la moja kwa moja au mtiririko mubashara kabla ya zawadi yako kutangazwa, lakini bado YouTube itaendelea kusambaza zawadi kwa kipindi fulani cha muda baadaye.

Kumbuka: Idadi ya uanachama uliotoa kama zawadi, jina la chaneli yako na picha ya wasifu wako vinaonekana kwa umma. Maelezo haya yanaweza pia kupatikana kwenye chaneli kupitia Huduma yetu ya YouTube Data API na chaneli husika inaweza kushiriki maelezo haya na huduma za wengine. Ununuzi wako wa uanachama unaotolewa kama zawadi unachukuliwa kuwa umekamilika baada ya YouTube kusambaza zawadi ya kwanza kwa mtazamaji.

Jijumuishe ili upate uanachama unaotolewa kama zawadi
Uanachama unaotolewa kama zawadi unapatikana tu kwenye chaneli zinazoshiriki kwa ajili ya kutumia ofa au ununuzi. Watazamaji wanaweza kujijumuisha na kupata zawadi wakitumia wavuti au vifaa vya Android au iOS.

Jinsi ya kununua na kupata Uanachama Unaotolewa kama Zawadi

Watazamaji lazima wajijimuishe ili waweze kutimiza masharti ya kupokea uanachama unaotolewa kama zawadi. Ukishajijumuisha, utakuwa umetimiza masharti ya kupata uanachama unaotolewa kama zawadi kwenye chaneli yoyote ambayo imewezesha kipengele cha utoaji wa uanachama kama zawadi ambacho umekitumia hivi karibuni (kwa mfano, kwa kutazama video katika chaneli hiyo). Unapopokea zawadi, itawekwa kiotomatiki kwenye akaunti yako na hivyo kukupa uwezo wa kufikia manufaa maalum kama vile beji na emoji maalum.

Ikiwa hapo awali ulijijumuisha kwenye chaneli mahususi tu, bado unatimiza masharti ya kupokea zawadi kwenye chaneli hiyo. Bado utahitaji kujijumuisha kimataifa ili utimize masharti ya kupokea zawadi kwenye chaneli zingine.

Ili ujijumuishe kupokea uanachama unaotolewa kama zawadi, lazima uwe umeingia katika akaunti kwenye chaneli ya YouTube ambayo si Akaunti ya Biashara. Angalia iwapo unatumia Akaunti ya Biashara. Kwa sasa, wanachama katika chaneli hawatimizi masharti ya kupokea uanachama unaotolewa kama zawadi.

Kujijumuisha ili upokee uanachama unaotolewa kama zawadi

Kuna njia nyingi za kujijumuisha ili upokee zawadi, ikiwa ni pamoja na, lakini si tu:

  • Katika gumzo la moja kwa moja
  • Kwenye ukurasa wa kutazama wa video
  • Kwenye ukurasa wa chaneli
  • Kwa kutumia URL ya kipekee ya kujijumuisha ya mtayarishi (kiungo cha ukurasa wa chaneli ambao una zawadi au unaruhusu zawadi mwishoni).

Kujijumuisha kupitia gumzo la moja kwa moja

  1. Nenda kwenye mtiririko mubashara au Onyesho la kwanza katika chaneli inayotimiza masharti ya vigezo.
  2. Katika gumzo hilo la moja kwa moja:
    1. Chagua RUHUSU ZAWADI, au
    2. Chagua kipengele kilichobandikwa cha Zawadi za uanachama .
  3. Thibitisha kuwa ungependa kujijumuisha kwa kuwasha swichi ya "Ruhusu zawadi".

Kujijumuisha kupitia chaneli au ukurasa wa kutazama:

  1. Katika chaneli inayotimiza masharti, nenda kwenye ukurasa wa chaneli au ukurasa wa kutazama wa video.
  2. Bofya JIUNGE  kisha Zaidi   kisha ”Mipangilio ya Zawadi.”
  3. Thibitisha kuwa ungependa kujijumuisha kwa kuwasha swichi ya "Ruhusu zawadi".
​​Kumbuka: Ukichaguliwa kupata uanachama unaotolewa kama zawadi, jina la chaneli yako litaonekana kwa umma. Maelezo haya yanaweza pia kupatikana kwenye chaneli kupitia Huduma yetu ya YouTube Data API na chaneli husika inaweza kushiriki maelezo haya na huduma za wengine.

Ili uchague kutopokea zawadi, fungua "Mipangilio ya Zawadi" kwa kubofya kitufe cha JIUNGE kwenye chaneli au ukurasa wowote ambapo uanachama umewashwa, kisha zima "Ruhusu Zawadi" ili kutopokea zawadi. Hutatimiza tena masharti ya kupokea zawadi kwenye chaneli yoyote.

Kupokea uanachama unaotolewa kama zawadi

Mwanachama katika chaneli au Mtayarishi anaponunua uanachama unaotolewa kama zawadi, kitendo hicho kitatangazwa kwenye gumzo la moja kwa moja. Ikiwa umechaguliwa kupokea uanachama wa mwezi 1, arifa itaonekana kwenye gumzo la moja kwa moja na tutakutumia arifa ya barua pepe.

Huwezi kurejeshewa pesa kwa ajili ya uanachama unaotolewa kama zawadi na pia huwezi kuubadilisha ili upokee malipo ya pesa. Kila uanachama unaotolewa kama zawadi unatoa uwezo wa kufikia manufaa ya uanachama katika chaneli kwa kipindi cha mwezi 1 na huisha baada ya kipindi hicho kupita.

Ili uangalie manufaa ya uanachama wako na ufikie manufaa:

  • Chagua kichupo cha 'Uanachama' kwenye chaneli ambacho wewe ni mwanachama, AU
  • Chagua ANGALIA MANUFAA kwenye ukurasa wowote wa video wa chaneli hiyo.

Uanachama unaotolewa kama zawadi haujirudii na hutatozwa baada ya uanachama huo kuisha. Ikiwa ungependa kusitisha uanachama wako unaotolewa kama zawadi mapema, wasiliana na timu ya usaidizi. Utapoteza uwezo wa kufikia manufaa ya uanachama unaotolewa kama zawadi.

Maelezo ya malipo

Maelezo ya kulipa

Wanachama wapya na waliopo

Ukiwa na uanachama unaoendelea ambao unalipiwa, utatozwa kiotomatiki mwanzoni mwa kipindi cha kutozwa kila mwezi.

Uanachama ulioghairiwa

Ukighairi uanachama unaolipiwa katika kituo, hutatozwa tena isipokuwa uuanzishe upya. Utaendelea kupokea manufaa ya uanachama hadi mwisho wa kipindi husika cha bili.

Uanachama ulioanzishwa upya

Unaweza kuanzisha upya uanachama wako wakati wowote. Endapo utaanzisha upya uanachama ndani ya kipindi kilekile cha kutozwa ulichoghairi, hutatozwa hadi kipindi hicho cha kutozwa kiishe.

Kusasisha maelezo yako ya malipo

Unaweza kubadilisha kadi ya mikopo uliyotumia kulipia uanachama unaolipiwa katika sehemu ya Usajili wangu kwenye Akaunti yako ya Google. Kumbuka kuwa huenda ukahitaji kuweka kwanza kadi mpya kwenye Akaunti yako ya Google.
Ukiwa na uanachama unaoendelea ambao unalipiwa, utatozwa kiotomatiki mwanzoni mwa kipindi cha kutozwa kila mwezi. Unaweza kuangalia tarehe ya malipo yanayofuata na udhibiti uanachama wako kwenye youtube.com/paid_memberships.

Gharama zinazojirudia nchini India

Kutokana na masharti ya eMandate ya Benki Kuu ya India, unapaswa kuthibitisha au kuweka upya maelezo yako ya malipo ili kudumisha uwezo wa kufikia uanachama wako unaorudiwa. Ili ufanye hivyo, fuata maagizo kwenye programu ya YouTube au kwenye youtube.com. Kumbuka kuwa huenda benki yako isitumie malipo yanayorudiwa kwa sasa. Angalia orodha ya benki zinazoruhusu mfumo wa malipo yanayorudiwa au upate maelezo zaidi.

Jinsi uanachama uliositishwa katika kituo unavyoathiri malipo yako

Maelezo kuhusu “Hali ya kusitishwa”

Wakati mwingine, uanachama katika kituo huwekwa katika "hali ya kusitishwa." Huenda hali hii ikatokea ikiwa kituo kitabadilisha Mitandao ya Vituo Mbalimbali, kitaweka mipangilio ya kituo kuwa kinawalenga watoto au hakiwezi kuchuma mapato. "Hali ya kusitishwa" inapotokea, inamaanisha kwamba kituo hakiwezi kuchuma mapato kupitia uanachama na kwa kawaida hali hii huwa ni ya muda mfupi. Kituo kikiwa katika “hali ya kusitishwa” inamaanisha hakitaweza kutoa manufaa.

Maelezo ya malipo

Endapo wewe ni mwanachama anayelipia wa kituo kilichopo kwenye "hali ya kusitishwa," malipo yako yanayorudiwa kila mwezi, kipindi cha kutozwa na uwezo wa kufikia uanachama pia utasitishwa.

Iwapo ulijisajili kwa ajili ya uanachama katika kituo kwenye iOS au Android, malipo yako yanayorudiwa kila mwezi yanaweza kughairiwa ikiwa kituo hicho kipo katika hali ya kusitishwa baada ya kipindi chako cha bili kuisha. Hali hii ikitokea, utapokea arifa kwamba uanachama wako umeghairiwa na utaweza kujiunga ikiwa/wakati uanachama wa kituo utaendelezwa.

Uanachama kwenye kituo unaweza kusitishwa kwa muda usiozidi siku 120; baada ya hapo, uanachama na malipo yanayorudiwa ya kila mwezi ya wanachama yataghairiwa.

Jinsi uanachama uliosimamishwa katika kituo unavyoathiri malipo yako

Endapo kituo kitasimamisha au kupoteza uwezo wa kufikia kipengele cha uanachama (k.m., iwapo kimeondolewa kwenye Mpango wa Washirika wa YouTube), malipo yote yanayorudiwa kila mwezi ya uanachama na uwezo wa kufikia manufaa ya uanachama utasimamishwa mara moja. Watazamaji waliokuwa wanachama wakati kituo kinasimamishwa, watatumiwa barua pepe ya kusimamishwa kwa huduma. Barua pepe itakuwa na maelezo kuhusu jinsi ya kutuma ombi la kurejeshewa pesa.

Kurejesha pesa za uanachama katika kituo

Unaweza kughairi uanachama wako unaolipiwa katika kituo wakati wowote. Baada ya kughairi, hutatozwa tena. Utaweza kutumia beji na kufikia marupurupu yanayotolewa na mtayarishi hadi mwisho wa kipindi cha kutozwa. Kumbuka kwamba hutarejeshewa pesa kwa kipindi cha muda kati ya ulipoghairi uanachama na siku uanachama wako katika kituo ulipoisha rasmi.
Iwapo utagundua utozaji wa uanachama katika kituo ambao haujaidhinishwa kwenye akaunti yako, fuata hatua hizi ili uripoti utozaji ambao haujaidhinishwa. Ikiwa marupurupu yanayotolewa na mtayarishi au vipengele vinginevyo vya uanachama wako unaolipiwa katika kituo vina kasoro, havipatikani au havifanyi kazi kama ilivyoelezwa, unaweza kuwasiliana na timu yetu ya usaidizi ili utume ombi la kurejeshewa pesa wakati wowote. Haturejeshi fedha au kutoa salio kwa vipindi vya bili ambavyo havijakamilika.
Iwapo wewe ni mwanachama aliyejisajili kupitia Apple, utahitaji kuwasiliana na usaidizi wa Apple ili utume ombi la kurejeshewa pesa kwa uanachama wako unaolipiwa katika kituo. Sera ya Apple ya kurejesha pesa itatumika.

Kugawana mapato ya uanachama katika kituo na watayarishi

Watayarishi hupokea asilimia 70 ya mapato ya uanachama yanayotambuliwa na Google baada ya kukata kodi ya mauzo na ada nyinginezo za eneo wanapoishi (kulingana na nchi na mfumo unaotumiwa na watumiaji). Kwa sasa, ada za uchakataji wa malipo (ikiwa ni pamoja na ada za kadi za mikopo) zinashughulikiwa na YouTube

Kutumia na kudhibiti manufaa yako ya uanachama

Manufaa ya uanachama katika chaneli kwa wanachama wote

Unapokuwa mwanachama, utapata uwezo wa kufikia manufaa fulani. Utapokea manufaa tofauti kulingana na viwango vya uanachama unavyojiunga navyo.
  • Machapisho ya jumuiya ya wanachama pekee: Unaweza kuangalia machapisho ya wanachama pekee kwenye kichupo cha Jumuiya cha chaneli. Maudhui ya kipekee huwekwa lebo ya "Wanachama pekee" na hujumuisha machapisho ya maandishi, GIF, kura, video na zaidi.
  • Rafu ya Kutambua Wanachama: Iwapo Mtayarishi atawasha rafu hii, ishara yako inaweza kuangaziwa kwenye ukurasa wa chaneli pamoja na wanachama wengine waliopo. Rafu hii ni njia ya Mtayarishi kukushukuru hadharani kwa kuwa mwanachama kwenye chaneli yake. Ukighairi uanachama wako, hutaangaziwa tena kwenye rafu.
  • Ujumbe wa Mafanikio ya Wanachama: Kwa kila mwezi utakaoendelea kuwa mwanachama (kuanzia mwezi wako wa pili mfululizo wa kuwa mwanachama) utakuwa na uwezo wa kutuma Ujumbe mmoja wa Mafanikio ya Wanachama. Ujumbe wa Mafanikio ya Wanachama ni ujumbe maalum ulioangaziwa ambao unaweza kutumika kwenye gumzo la moja kwa moja katika mitiririko mubashara au Maonyesho ya kwanza. Ujumbe huu maalum unaangazia muda wa jumla ambao umekuwa mwanachama wa chaneli hii na utaonekana kwa watazamaji wote.
  • Beji za Chaneli: Ni beji za uanachama za kipekee zinazoonekana hadharani karibu na jina lako la chaneli kwenye maoni na gumzo la moja kwa moja unalopiga kwenye chaneli hiyo.
    • Kwenye baadhi ya chaneli, beji hii itaonyesha muda ambao umekuwa mwanachama, iwe ni kupitia beji chaguomsingi zenye rangi tofauti au beji maalum.
  • Video za wanachama pekee: Video za kipekee zinazopatikana tu kwa wanachama wa chaneli katika viwango sahihi vya kutazama. Mtu yeyote anaweza kupata video ya wanachama pekee, lakini wanachama walio katika viwango sahihi tu ndio wanaoweza kuitazama. Video hizi zinaweza kupatikana kwenye vichupo vya Uanachama, Maudhui na Jumuiya vya chaneli. Video hizi pia zinaweza kuonekana kwenye mpasho wa chaneli zinazofuatiliwa na mwanachama na Ukurasa wa Kwanza. 
  • Ujumbe wa Mwanachama Mpya: Ukiwa mwanachama katika chaneli wakati mtiririko mubashara unaendelea kwenye chaneli hiyo, ujumbe wenye rangi ya kijani inayong'aa unaosema "Mwanachama Mpya" utatumwa kwenye gumzo la moja kwa moja. Picha ya wasifu wako pia itabandikwa juu kabisa kwenye gumzo kwa dakika 5.
  • Gumzo la moja kwa moja kwa wanachama pekee: Wakati mtiririko mubashara wa umma unaendelea, watayarishi wanaweza kufanya gumzo liwe mahususi kwa wanachama pekee. Ingawa kila mtu anaweza kutazama mtiririko mubashara, wanachama pekee ndio wanaweza kuchapisha gumzo. 
  • Emoji maalum: Ikiwa imepakiwa na mtayarishi, wanachama wa chaneli wanaweza kutumia emoji ya kipekee katika maoni kwenye video na magumzo ya moja kwa moja ya chaneli. Utatumia jina la familia lililotolewa na mtayarishi ili kukamilisha uwekaji emoji kiotomatiki katika gumzo la moja kwa moja. 
  • Marupurupu mengine yanayotolewa na mtayarishi: Ikiwa yanatolewa na chaneli, unaweza pia kupata uwezo wa kufikia marupurupu mengine ya kipekee yanayotolewa na mtayarishi.

Kumbuka: Kipengele cha "Hali ya polepole" kinachodhibiti mara ambazo unaweza kutuma maoni kwenye gumzo la moja kwa moja hakitumiki kwa wanachama wa chaneli wanaoshiriki, wanaolipia huduma.

Marupurupu yanayotolewa na mtayarishi kwa viwango mbalimbali

Kila kiwango kina kiwango chake cha bei. Manufaa yako yanaongezeka kila unapopandisha kiwango. Hali hii inamaanisha kwamba unapojiunga na kiwango cha gharama ya juu zaidi, utaweza kufikia manufaa yanayopatikana kwenye viwango vyote vya chini.

Nitapata manufaa yapi kwenye kila kiwango na ninawezaje kujiunga?

Hii inatofautiana kati ya chaneli na chaneli. Unaweza kuona manufaa mbalimbali unapobofya Jiunge.

Nimeshakuwa mwanachama, hivyo ninawezaje kuona manufaa mbalimbali yanayopatikana?

Nenda kwenye ukurasa wa kwanza wa chaneli ambayo wewe ni mwanachama kisha chagua Angalia manufaa.

Kuwasha au kuzima arifa za uanachama katika chaneli

Kama mwanachama katika chaneli, unaweza kupata maudhui ya wanachama pekee katika Kichupo cha jumuiya, Kichupo cha Uanachama au Kichupo cha Maudhui cha chaneli. Pia unaweza kuona video za wanachama pekee zikijitokeza kwenye Ukurasa wa kwanza na Mpasho wa chaneli unazofuatilia. Pia, tutatumia arifa au barua pepe ili kukufahamisha pale chaneli:

  • Itakapotengeneza chapisho jipya la wanachama pekee 
  • Itakapopakia video mpya ya wanachama pekee 
  • Itakapoanzisha mtiririko mpya wa moja kwa moja wa wanachama pekee
  • Itakaporatibu mtiririko moja kwa moja wa wanachama pekee utakaoanza ndani ya dakika 30

Vilevile, unaweza kuchagua kutopokea arifa na barua pepe zinazohusu maudhui ya wanachama pekee.

Kuzima arifa

Endapo hutaki kufahamu kuhusu maudhui mapya ya wanachama pekee, unaweza:

  • Kuchagua kutopokea arifa na barua pepe za chaneli mahususi ambazo wewe ni mwanachama.
    • Ili uchague kutopokea arifa za maudhui ya wanachama pekee: Nenda kwenye Mipangilio kisha Arifa kisha Zima swichi karibu na Wanachama pekee.
    • Ili uchague kutopokea barua pepe za maudhui ya wanachama pekee: Tumia kiungo cha Kujiondoa kilichopo kwenye barua pepe yoyote ya wanachama pekee utakayopokea. Ikiwa utapenda kujisajili tena ili upokee arifa za barua pepe, nenda kwenye Mipangilio kisha Arifa kisha Chini ya “Arifa za barua pepe” chagua “Barua pepe ulizojiondoa” kisha chagua barua pepe ambazo ungependa kupokea.
  • Kuchagua kutopokea arifa zote za chaneli mahususi:
    • Nenda kwenye chaneli unayofuatilia kisha Arifa  kisha Hakuna . Hatua hii itazima arifa zote za chaneli hii, si tu kwa maudhui ya wanachama pekee.
  • Zima arifa zote kwenye akaunti yako.

Kutazama maudhui ya kipekee katika kichupo cha jumuiya

Maudhui ya kipekee huwekewa lebo ya “Wanachama pekee” katika kichupo cha Jumuiya. Hujumuisha machapisho ya maandishi, GIF, kura, video na zaidi.

Kuripoti manufaa yasiyofaa

Endapo utaona manufaa yanayotolewa ambayo unadhani yanakiuka Mwongozo wa Jumuiya wa YouTube (ikiwa ni pamoja na maudhui ya ngono, ya vurugu au ya chuki, ofa zinazopotosha au taka) unaweza kuyaripoti kwa kubofya Ripoti manufaa kwenye skrini ya ofa, baada ya kubofya kitufe cha Jiunge (au Angalia manufaa, ikiwa wewe ni mwanachama tayari).

Maelezo ya faragha

Hali ya uanachama inayoonekana

Baada ya kujiunga na chaneli, maelezo yafuatayo yataonekana hadharani kwenye YouTube na huenda chaneli ikashiriki maelezo na kampuni za watu wengine:
  • URL ya chaneli yako
  • Jina la chaneli yako ya YouTube
  • Picha ya wasifu wako
  • Ulipojiunga na chaneli ukiwa mwanachama
  • Kiwango chako cha uanachama
Kumbuka: Huenda chaneli ikashiriki maelezo haya na kikundi kidogo cha kampuni mahususi za watu wengine ili kutoa manufaa ya chaneli.

Jinsi maelezo yako yanavyoweza kutumiwa

Huenda watazamaji wengine wakaona maelezo yako yaliyopo hapo juu. Maelezo yatakayoshirikiwa yanaweza kutegemea chaneli uliyojiunga nayo. Orodha hii si kamilifu:
  • Wanachama wote wana beji inayoonekana karibu na jina la chaneli yako katika maoni na gumzo.
  • Ukiwa mwanachama katika chaneli wakati mtiririko mubashara unaendelea kwenye chaneli hiyo, ujumbe wenye rangi ya kijani inayong'aa unaosema "Mwanachama Mpya" utatumwa kwenye gumzo la moja kwa moja kisha picha ya wasifu wako itabandikwa juu kabisa kwenye gumzo la moja kwa moja kwa muda wa dakika 5. Ujumbe huo utaoonyesha jina la chaneli yako kiashiria kikielekezwa juu yake.
  • Baadhi ya chaneli zinaweza kuweka maelezo yako yaliyo hapo juu kwenye orodha ya "Watu wa kuwashukuru" katika video au maelezo yako yanaweza kuwekwa kwenye rafu ya chaneli ya kutambua wanachama.
  • Baadhi ya chaneli zinaweza kushiriki maelezo yako yaliyopo hapo juu ili kukupatia huduma (kwa mfano uwezo mahususi kwa wanachama pekee wa kufikia chumba cha gumzo kinachosimamiwa na kampuni nyingine).

Kuangalia na kuondoa idhini ya kufikia ya tovuti au programu za wengine

Kuondoa idhini ya kufikia ya tovuti au programu za wengine

Iwapo ulitoa idhini ya kufikia akaunti kwa tovuti au programu ambayo huiamini tena, unaweza kuondoa idhini hiyo ya kufikia Akaunti yako ya Google. Tovuti au programu haitaweza kufikia maelezo yoyote zaidi kutoka kwenye Akaunti yako ya Google, lakini huenda ukahitaji kuomba wafute data ambayo tayari wanayo.
  1. Nenda kwenye Akaunti yako ya Google.
  2. Kwenye kidirisha cha usogezaji cha upande wa kushoto, chagua Usalama.
  3. Kwenye Kidirisha cha programu za wengine zenye idhini ya kufikia akaunti, chagua Dhibiti ufikiaji wa programu za wengine.
  4. Chagua tovuti au programu ambayo ungependa kuondoa.
  5. Chagua Ondoa Idhini ya Kufikia.

Kuripoti tovuti au programu za wengine

Fuata hatua hizi ikiwa unaamini kwamba tovuti au programu inatumia vibaya data yako, kama vile kutengeneza ujumbe taka, kukuiga au kutumia data yako kwa njia zilizo hatari.

  1. Nenda kwenye sehemu ya Programu zenye uwezo wa kufikia akaunti yako kwenye Akaunti yako ya Google. Huenda ukahitaji kuingia katika akaunti.
  2. Chagua programu unayotaka kuripoti kisha Ripoti programu hii.

Pata maelezo zaidi kuhusu idhini ya kufikia akaunti kwa ajili ya tovuti na programu za wengine.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
3973093880089218365
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false