Ingia katika akaunti ya Kidhibiti Maudhui

Vipengele hivi vinapatikana tu kwa washirika ambao hutumia Kidhibiti Maudhui cha Studio ya YouTube. Wasiliana na Msimamizi wako wa Washirika wa YouTube ili uweze kuvitumia.

Funguo za siri hukupa ulinzi thabiti zaidi dhidi ya hatari kama vile wizi wa data binafsi. Pata maelezo zaidi kuhusu funguo za siri.

Wasimamizi na watumiaji wanaokubali mwaliko wa kujiunga kwenye akaunti ya Kidhibiti Maudhui wanahitaji kuingia katika akaunti ili wafikie Kidhibiti chao cha Maudhui.

  • Kidhibiti Maudhui: Zana ya wavuti kwa washirika wanaodhibiti maudhui na haki kwenye YouTube. Akaunti ya Kidhibiti Maudhui inamiliki kituo kimoja au zaidi cha YouTube na vipengee vinavyohusishwa nazo. Inajulikana pia kama Kidhibiti Maudhui cha Studio.
  • Msimamizi: Mtu anayesimamia Kidhibiti Maudhui na kualika wengine kukifikia.
  • Mtumiaji: Yeyote anayetumia Kidhibiti Maudhui.

Kuingia katika akaunti

  1. Ingia katika akaunti ya YouTube.
  2. Bofya picha yako ya wasifu .
  3. Chagua Badilisha akaunti .
    • Utapata orodha ya akaunti unazoweza kutumia.
    • Ikiwa una idhini ya kufikia Kidhibiti Maudhui, jina la akaunti litaonyeshwa kwenye orodha pamoja na Kidhibiti Maudhui chini yake.
  4. Bofya akaunti ya Kidhibiti Maudhui. YouTube itabadilisha ili utumie akaunti hiyo.

Kidokezo: Unaweza pia kutumia Kibadilishaji cha Kituo kubadilisha kwa urahisi kati ya vituo vyako na Kidhibiti chako cha Maudhui.

Ukikamilisha kutumia Kidhibiti Maudhui, bofya picha ya wasifu kisha uchague akaunti nyingine au uondoke kwenye akaunti.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
13054652019817638426
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false