Kujanibisha metadata ya video

Vipengele hivi vinapatikana tu kwa washirika wanaotumia Kidhibiti Maudhui cha YouTube kudhibiti maudhui yao yaliyo na hakimiliki.

Unaweza kuweka majina na maelezo ya video yaliyotafsiriwa kwenye video zako. Hii husaidia video zako kuweza kufikiwa na mashabiki nje ya nchi unakoishi na hukusaidia kukuza hadhira ya kimataifa. Mashabiki wako wataweza kupata video zako kwa kutafuta katika lugha yao na tutaonyesha jina na maelezo ya video katika ukurasa wa kutazama pamoja na kila sehemu kwenye YouTube katika lugha sahihi, kwa watumiaji sahihi.

Unaweza kujanibisha metadata ya video ukitumia kiolesura cha YouTube au unaweza kupakia faili ya CSV kwa kutumia kiolezo cha Kusasisha Ujanibishaji wa Video.

Ili upakie metadata ya video iliyotafsiriwa:

  1. Pakua kiolezo cha Kusasisha Ujanibishaji wa Video kwenye ukurasa wa Violezo vya Uwasilishaji wa Maudhui.

  2. Kamilisha kiolezo ukitumia data yako iliyotafsiriwa.

  3. Hifadhi faili katika muundo wa .csv.

  4. Bofya kiungo cha Thibitisha na Upakie kinachoonekana chini ya UWASILISHAJI WA MAUDHUI katika upande wa kushoto wa menyu ya Kidhibiti Maudhui.

  5. Bofya Chagua faili ili upakie faili yako ya .csv iliyohifadhiwa.

    Ikiwa utapata bango jekundu lenye hitilafu za uthibitishaji, utahitaji ufanye marekebisho katika faili yako, uhifadhi mabadiliko na uipakie upya ili uone aikoni ya kijani.

  6. Bofya kitufe cha Chakata kifurushi 

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
8942019981474449565
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false