Mwongozo wa maudhui yanayofaa watangazaji

Tumerahisisha chaguo za miundo ya matangazo yanayoonyeshwa kabla au baada ya video yako kucheza ili kuongeza mapato ya mtayarishi. Tumeondoa chaguo za matangazo mahususi kwa matangazo yanayoonyeshwa kabla ya video kucheza au baada ya video kucheza, yanayoweza kurukwa na yasiyorukika. Sasa unapowasha matangazo kwenye video ndefu mpya, tunawaonyesha watazamaji wako matangazo yanayoonyeshwa kabla ya video kucheza au baada ya video kucheza, yanayoweza kurukwa na yasiyorukika panapofaa. Badiliko hili linafanya mbinu bora zinazopendekezwa za kuwasha miundo yote ya matangazo zifae kwa kila mtu. Chaguo zako za matangazo yanayochezwa katikati ya video hazijabadilika. Pia, tumehifadhi chaguo zako za matangazo katika video ndefu zilizopo, isipokuwa ukibadilisha mipangilio ya uchumaji wa mapato.
Iwapo uko kwenye Mpango wa Washirika wa YouTube, unaweza kupokea sehemu ya mapato kutokana na matangazo. Makala haya yanalenga kukusaidia ufahamu video mahususi au Video Fupi kwenye chaneli yako zinazofaa watangazaji. Watayarishi wanaweza kutumia makala haya kufahamu dodoso la uthibitishaji wa kujifanyia kwenye mfumo na kanuni mahususi kuhusu maudhui yanayoweza kuonyesha matangazo, yanayoweza kuonyesha matangazo machache na maudhui ambayo hayawezi kuonyesha matangazo na yanapaswa kuzima kipengele cha uchumaji wa mapato. Sera zetu zinatumika kwenye sehemu zote za maudhui yako (video, Video fupi au mtiririko wa moja kwa moja, kijipicha, mada, maelezo na lebo). Pata maelezo zaidi kuhusu mbinu zetu bora.

Mifumo yetu hukosea, lakini unaweza kuomba uhakiki unaofanywa na binadamu dhidi ya maamuzi yanayofanywa na mifumo yetu ya kiotomatiki.

Tarehe 23, Aprili 2024: Tumesasisha mifano ya kashfa na lugha chafu iliyokithiri inayoweza kusababisha ukadiriaji wa “haichumi mapato ya matangazo” kwenye mwongozo wetu kuhusu lugha isiyofaa. Lugha hii iliyosasishwa si mabadiliko ya sera na inanuia kufanya sera yetu iliyopo iwe wazi zaidi na haibadilishi jinsi video zako zinavyokaguliwa.
Tarehe 23, Machi 2022: Kutokana na vita vinavyoendelea Ukraini, maudhui yanayopuuza, kuhalalisha au yenye nia ya kujinufaisha na vita hivyo hayatakidhi vigezo vya uchumaji wa mapato hadi ibainishwe vinginevyo. Lengo la sasisho hili ni kutoa ufafanuzi na katika hali fulani kupanua mwongozo wetu unaohusiana na vita hivi.

Note: All content uploaded to YouTube must comply with both our Community Guidelines and our Program Policies. If your content violates our Community Guidelines, it may be removed from YouTube. If you see violative content, you can report it.

Utakachopata kwenye makala haya

Utapata mifano ya maudhui ambayo hayafai matangazo, jambo litakalosababisha hali ya uchumaji wa mapato kuwa "matangazo machache au hamna matangazo".

Zifuatazo ni mada zote kuu ambazo hazifai watangazaji:

Ili upate maelezo zaidi kuhusu hoja muhimu zilizotumiwa kwenye mwongozo huu, angalia jedwali letu la ufafanuzi.

Tafadhali kumbuka kuwa muktadha ni muhimu sana. Maudhui ya kisanaa kama vile video za muziki yanaweza kuwa na vipengele kama vile lugha isiyofaa, marejeleo ya utumiaji kiasi ya dawa za kulevya au maudhui ya ngono yasiyo dhahiri na bado yakafaa matangazo.

Kufungua maelezo yote ya sera mara moja kunaweza kusaidia iwapo ungependa kutafuta hoja mahususi kwenye ukurasa huu. Bofya hapa ili ufungue mwongozo wote.

Lugha isiyofaa

Maudhui yaliyo na matumizi ya lugha chafu au isiyofaa mwanzoni mwa video au katika sehemu kubwa ya video huenda yasifae matangazo. Matumizi madogo ya lugha chafu (kama vile kwenye video za muziki, nyimbo zinazosindikiza, muziki wa utangulizi au utamatishaji au wimbo unaochezwa chinichini) hayatasababisha video yako isifae matangazo.

Maelezo ya Sera
Mwongozo wa matangazo Maelezo na chaguo za dodoso

Maudhui haya yanaweza kutumika kuchuma mapato ya matangazo

Lugha chafu iliyofupishwa au iliyobanwa au maneno kama vile "bure" au "shenzi" kwenye jina, kijipicha au video. Lugha chafu kiasi kama vile "malaya", "bwege", "mpumbavu" na "shonde" inayotumiwa mara kwa mara kwenye video. Lugha chafu inayotumiwa ndani ya muziki au maudhui ya video ya ucheshi.

Ufafanuzi:
  • “Lugha chafu iliyobanwa” inarejelea mambo kama vile kuzima sauti au kuweka sauti nyingine ya mashine inayozuia neno na pia kufunika maneno yaliyoandikwa kwa kutumia pau nyeusi, ishara, au maandishi yanayowekwa baada ya kurekodi.
  • “Lugha chafu yenye maneno yaliyofupishwa” inarejelea ufupisho kama vile WTF (“matusi ya kingono”) ambapo neno halisi linafupishwa kwa kutumia baadhi ya herufi zake.
Maudhui haya yanaweza kuchuma mapato machache au yasichume kabisa mapato ya matangazo

Lugha chafu zaidi (kama vile matusi ya kingono) inayotumiwa katika sekunde 7 za kwanza au lugha chafu kiasi (kama vile "shonde") kwenye jina au kijipicha.

Baadhi ya mifano ya maudhui ambayo pia yanapatikana katika aina hii:
  • Matumizi ya lugha chafu kwenye video yote (kama vile lugha chafu inayotumiwa katika sentensi nyingi).
  • Lugha chafu iliyotumiwa kwenye jina au kijipicha cha muziki au maudhui ya vichekesho vya jukwaani.
Maudhui haya hayatachuma mapato ya matangazo

Lugha chafu zaidi (kama vile matusi ya kingono) inayotumiwa katika vijipicha au majina. Matumizi yoyote ya lugha chafu iliyokithiri, ambayo inajumuisha lugha ya chuki au maneno ya kufedhehesha kwenye video, kijipicha au jina kama vile "mfi***wa" au "mku**u”.

Ili upate maelezo ya ziada kuhusu lugha ya chuki au kashfa, unaweza pia kurejelea mwongozo wetu kuhusu maudhui ya chuki na ya kudhalilisha ndani ya kituo chetu cha usaidizi.

Baadhi ya mifano ya maudhui ambayo pia yanapatikana katika aina hii:

Ili upate maelezo zaidi kuhusu hoja muhimu zilizotumiwa kwenye mwongozo huu, angalia jedwali letu la ufafanuzi.

Vurugu

Maudhui ambayo sehemu inayoangaziwa inahusu damu, vurugu au majeraha, yanapoonyeshwa bila muktadha mwingine, hayafai matangazo. Iwapo unaonyesha maudhui ya vurugu katika muktadha wa habari, elimu, sanaa au hali halisi, muktadha huo wa ziada ni muhimu. Kwa mfano, iwapo video inatoa ripoti ya habari zinazoaminika kuhusu tukio la vurugu katika muktadha wa uanahabari, huenda ikaruhusiwa kuchuma mapato. Vurugu katika uchezaji wa video ambayo haijahaririwa inakubaliwa kuonyesha matangazo kwa jumla, lakini hayaruhusiwi katika klipu za filamu ambapo vurugu inayokithiri ndiyo inayoangaziwa. Michezo yote (iwe halisi au la) inajumuishwa kwa mujibu wa sera hii.

Maelezo ya Sera
Mwongozo wa matangazo Maelezo na chaguo za dodoso
Maudhui haya yanaweza kutumika kuchuma mapato ya matangazo

Utekelezaji wa sheria ikiwa ni pamoja na jukumu la kawaida likifanywa (kama vile kukamatwa kwa lazima, kudhibiti umati, kuzozana na afisa, kuingia kwa lazima); vurugu ya uchezaji ambayo haijahaririwa inayotokea baada ya sekunde 15 za kwanza; vurugu isiyokithiri yenye kiasi kidogo cha damu; maiti ambazo zimebanwa kikamilifu, kutiwa ukungu, kuandaliwa kuzikwa au kuonyeshwa katika matukio ya kihistoria kama vile vita, kama sehemu ya video ya elimu.

Baadhi ya mifano ya maudhui ambayo pia yanapatikana katika aina hii:

Vurugu ya jumla

  • Maudhui yanayoigizwa yanayoonyesha vurugu isiyoogofya au vurugu inayoogofya.
    • Kama sehemu ya masimulizi mapana, yanayoonyesha tukio la muda mfupi linalohusu madhara ya mwili (kama vile majeraha ya risasi) ikiwa sehemu ya tukio la kitendo cha vurugu.
    • Dondoo za vurugu za vita kutoka kwenye filamu ya mapambano (kama vile maudhui ya kuigizwa) ambapo majeraha hayawezi kutambulika.
    • Watu wakilia kutokana na kifo katika maudhui ya kuigiza.
  • Kuonyesha majeraha yasiyoogofya.
    • Mhusika akianguka kwa magoti ambapo kiasi kidogo cha damu huonyeshwa au hamna damu kabisa.
    • Kuanguka ghafla kutoka kwenye mlima au kujigonga kwenye ukuta bila kukusudia au kiajali, kama sehemu ya spoti au filamu.
Michezo ya Video
  • Vurugu kwenye michezo ya video ni pamoja na:
    • Matukio ya kuogofya (kama vile mashambulizi ya kikatili kwa mtu) nje ya sekunde 15 za mwanzo za video.
    • Vurugu isiyo ya kweli, ya mzaha na kwa jumla inakubalika kwa umri wote (kama vile michezo ya video inayofaa familia inayoonyesha kukimbia ili kutoroka mazimwi).
    • Vurugu ambayo imehaririwa, kutiwa ukungu au vinginevyo kufichwa (kama vile tukio la kukatwa kichwa lililotiwa ukungu).
Vifo na majanga
  • Maudhui ya kielimu au kihistoria yaliyo na:
    • Maoyesho yasiyoogofya ya maiti.
      • Kuonyesha hadharani mwili wa aliyekufa kama njia ya kumpa heshima za mwisho ambapo maiti yake haitishi.
    • Picha za maiti zinazoogofya zilizohaririwa kikamilifu (kama vile kutiwa ukungu).
  • Maonyesho ya majanga yanayohusisha tukio moja la kifo au zaidi (bila kujumuisha matukio nyeti kama vile mauaji ya watu wengi kwa kuwafyatulia risasi au mashambulizi ya kigaidi) kwa kuonyesha kidogo au kutoonyesha kabisa vitendo vya vurugu au matokeo yake.
    • Ripoti za matukio ya karibu ya mauaji ya binadamu bila maelezo ya kuogofya kuhusu wahusika.
  • Ripoti zenye maudhui ya kuelimisha, yaliyoigizwa, ya kihabari au video za muziki zilizo na:
    • Wakati unaodokezwa wa kifo au majeraha makubwa ya mwili
    • Uharibifu mkubwa wa mali ambapo kifo au majeraha makubwa ya mwili yanaweza kutokea (kama vile milipuko, moto, kuanguka kwa majengo n.k).
    • Maonyesho ya maiti ambao hawajaandaliwa katika mazishi ya umma yaliyo na majeneza yaliyo wazi.
Uwindaji
  • Maudhui ya uwindaji ambapo hakuna maonyesho yanayoogofya ya majeraha kwa wanyama au maumivu ya muda mrefu.
    • Video za uwindaji ambapo tukio la kuua au kujeruhi haliwezi kubainika, na hamna video mahususi kuhusu jinsi mnyama huyu aliyekufa anatayarishwa kwa madhumuni kuwa nyara au chakula.
Ukatili kwa wanyama
  • Maonyesho yasiyoogofya ya wanyama wakishambuliana katika mazingira halisi.
    • Wanyama wawindaji wanaokimbiza windo ambapo maelezo ya kuogofya (kama vile kulenga viungo vya mwili vya mnyama anayewindwa vilivyo na damu au matukio ya kuogofya ya kuwinda mnyama) hayajumuishwi; damu inaweza kuonekana kwa muda mfupi, lakini si sehemu kuu ya maudhui.
Unyanyasaji kwa wanyama
  • Wanyama wakiwa katika dhiki wakati wa mafunzo yanayolenga aina mahususi za wanyama, matibabu au kuhamishwa kwa wanyama.
  • Maonyesho au majadiliano kuhusu unyanyasaji wa wanyama bila video halisi ya unyanyasaji huo.
Vurugu katika uchezaji wa spoti
  • Vurugu katika spoti za mapigano zinazojumuisha silaha (kama vile mchezo wa vitara) licha ya mavazi ya kujilinda au tahadhari za usalama.
  • Majeraha yasiyoogofya katika spoti au majeraha yanayoogofya kama sehemu ya uchezaji wa spoti ambapo damu inaonyeshwa.
    • Spoti za mapambano kama vile ndondi zinazofanywa katika muktadha wa kitaalamu (kama vile kituo au ukumbi wa kufanya mazoezi).
  • Majeraha yasiyoogofya (kama vile kuteguka kifundo) yanayoonyeshwa katika uchezaji wa spoti.
Mapigano (bila kujumuisha mapambano ya spoti)
  • Maonyesho ya mapigano katika muktadha wa elimu bila majeraha au mapigo makali.
    • Hatua za kujilinda ambazo zinaonyeshwa kama mafunzo.
  • Maonyesho ya muda mfupi ya watu wakipigana bila majeraha yanayoonekana.
Utekelezaji wa sheria na majibizano makali
  • Mawasiliano yasiyo ya kivita au yasiyochukiza na wanaotekeleza sheria.
    • Mawasiliano ya kawaida na polisi (kama vile kuuliza maelekezo, kupokea tiketi ya kuegesha, n.k.).
  • Majibizano yasiyo ya kimwili na polisi, kusachiwa na polisi au polisi kuingia kwa nguvu katika nyumba pamoja na kukimbizwa na polisi.
  • Majibizano makali, vurugu au mabishano na wanaotekeleza sheria katika muktadha wa kielimu au ripoti za kihabari.
    • Uchambuzi kwa kutumia klipu kutoka kwenye ripoti ya habari kuhusu maandamano ya vurugu yaliyofanywa na raia (kama vile kupiga au kuangusha raia chini).
    • Kuripoti polisi wanapowamwagia maji raia kwenye maandamano.
Vita na migogoro
  • Majadiliano au maonyesho ya kielimu yasiyoogofya kuhusu vita na/au migogoro.
    • Ufyatuaji kutoka kwenye maeneo yasiyoonekana bila maonyesho ya maumivu au mateso.
Vurugu kuhusu watoto
  • Video zinazoangazia mchezo wa kupigana au migogoro ya nyumbani kati ya watoto bila majeraha au dhiki.
  • Maudhui ya muziki kuhusu vurugu kati ya watoto bila kuonyesha video au kwa kuonyesha video ya muda mfupi ya matendo hayo.
Ufafanuzi:
  • “Vurugu kiasi” inarejelea mabishano katika maudhui halisi au matendo ya muda mfupi ya vurugu kama vile kupiga ngumi.
  • "Vurugu isiyo ya kuogofya" hurejelea maonyesho ya tabia ya vurugu dhidi ya mtu mwingine kama vile kumnyooshea kidole huku ukifoka au vitendo vichache vya vurugu (kama vile kurusha chupa ukutani).
Maudhui haya yanaweza kuchuma mapato machache au yasichume kabisa mapato ya matangazo

Utekelezaji wa sheria kwa njia ya kuogofya kama vile majeraha yanayoonekana; maiti zenye majeraha au madhara dhahiri katika miktadha ya elimu au hali halisi (kama vile chaneli ya kujifunza historia); vurugu ya mchezo ya kuogofya katika kijipicha au kuonekana mapema katika maudhui; video ghafi ya mapambano kwa silaha bila majeraha; ufafanuzi wa maelezo ya kuogofya ya majanga; maudhui ya kuigiza yanayoonyesha majeraha mabaya na ya kushtua.

Baadhi ya mifano ya maudhui ambayo pia yanapatikana katika aina hii:

Vurugu ya jumla

  • Vurugu iliyoigizwa ambayo husababisha majeraha makubwa ambapo matokeo au athari huonekana na ipo.
    • Sehemu za matukio yaliyo na damu au yanayotisha ambapo mifupa iliyovunjika inaonekana.
    • Maudhui ya video ndefu yaliyoigizwa, yaliyo na tukio fupi la vurugu ambalo linaogofya zaidi (kama vile mauaji wa watu wengi) au mkusanyiko wa video wa matukio kama hayo yanayoogofya.
    • Maelezo yanayoogofya zaidi ya matukio yanayosikitisha (katika muundo wa sauti au video).
    • Watu wanaoteseka kwa kushindwa kupumua au wana maumivu makali, kama vile kutokana na kukohoa bila kukoma.
    • Video ya majanga yanayojumuisha madhara kwa watu yanaoonekana au mateso kutokana na majanga hayo, kama vile dhiki kuu ya kihisia.
  • Video ghafi ya magofu ya majengo yaliyoharibiwa kutokana na tukio la vurugu (kama vila magofu ya shule baada ya kimbunga) au watu walio na majeraha ya kawaida (kama vile kuteguka kwa vifundo vya mguu au kuweka bandeji kwenye vidole).

Michezo ya Video

  • Vurugu ya mchezo inayoogofya kwenye kijipicha au katika sekunde 8 hadi 15 za mwanzo za video. 
    • “Vurugu ya mchezo inayoogofya” ni pamoja na mauaji ya kikatili au majeraha mabaya yanayoangazia ugiligili na sehemu za mwili kama vile kukatwa vichwa na kukatwa kwa viungo vya mwili. 

Vifo na majanga

  • Kuripoti majanga yanayohusisha waathiriwa wengi yanayojumuisha maelezo ya kutisha au kuogofya.
    • Filamu ya hali halisi kuhusu mauaji ya watu ya hivi karibuni inayotumia lugha ya ufafanuzi wa mazingira ya kifo.

Mapigano (bila kujumuisha mapambano ya spoti)

  • Mapigano ya mtaani yanayoangazia majeraha au mapigo yanayoonekana katika muktadha wa elimu.
    • Mapigano ya mtaani yanayoogofya ikiwa ni pamoja na matukio yanayoangazia majeraha na dhiki ya hisia (kama vile kupiga mayowe).

Utekelezaji wa sheria na majibizano makali

  • Majibizano makali sana na maofisa wa kutekeleza sheria, kwa kawaida ni pamoja na vitendo vya kikatili vinavyofanywa na au dhidi ya maofisa wa kutekeleza sheria.
    • Kuwapiga raia kwa kutumia fimbo ambapo majeraha yanatokea
    • Kuwatemea mate polisi 

Vurugu katika uchezaji wa spoti

  • Majeraha ya spoti yanayoogofya kama sehemu ya video pana yenye muktadha.
    • Mikusanyiko au klipu za kuangazia zinazojumuisha majeraha lakini haziyalengi kimahususi.

Ukatili kwa wanyama

  • Ukatili kwa wanyama katika ulimwengu halisi ambao hujasababishwa na binadamu au wanyama waliopewa mafunzo na binadamu (kama vile simba wa mwituni wakiwinda swala, lakini si mbwa waliopewa mafunzo ya kukamata sungura).
    • Wakati mada kuu ya video ni kuangazia majeraha ya wanyama yanayoogofya kwa muda mrefu (kama vile damu au mifupa).

Uwindaji

  • Maudhui ya uwindaji yanayoangazia picha zinazoogofya za muda mfupi kama vile wanyama waliojeruhiwa au wanaoteseka (kama vile sehemu za mwili zenye damu) zinazoonyeshwa katika maudhui.

Vita na migogoro

  • Video ghafi ya kweli isiyoogofya ya mapambano kwa silaha (kama vile vita) bila muktadha wa elimu, bila matukio yanayotisha wala majeraha dhahiri.
Maudhui haya hayatachuma mapato ya matangazo

Maiti za kuogofya katika video isiyo ya elimu; uchezaji wa video unaoangazia mada zilizopigwa marufuku (kama vile unyanyasaji wa kingono). Matendo ya vurugu yanayoogofya zaidi (ikiwa ni pamoja na yanayojumuisha utekelezaji wa sheria) na majeraha. Uchochezi au kusifu vurugu.

Baadhi ya mifano ya maudhui ambayo pia yanapatikana katika aina hii:

Vurugu ya jumla

  • Kuangazia damu, matumbo, damu nyingi, ugiligili wa mwili (watu au wanyama), picha za maeneo ya uhalifu au ajali zenye muktadha mdogo au bila muktadha.
  • Kuonyesha matokeo ya kuogofya ya kitendo cha vurugu ambacho kinajumuisha picha za kuogofya sana, ikiwa ni pamoja na:
    • Maonyesho ya umwagaji damu kwa kiasi kikubwa au ya kutisha (kama vile vidonda kutokana na mguu uliokatwa au majeraha makubwa baada ya kuungua)
    • Maumivu makali (kama vile watu kulia au kuzirai kutokana na maumivu makali kwenye vidonda)
  • Maudhui yanayoangazia picha za kuogofya, kushtua na/au za vurugu, au matukio ya uchochezi au yanayosifu vurugu.

Michezo ya Video

  • Kuangazia uchezaji uliotengenezwa ili kuunda hali ya kushtuka. Mifano ni pamoja na:
    • Kujumuisha wahusika wasiodhibitiwa na mchezaji kwa mauaji ya watu.
  • Vurugu za kuogofya za michezo kwenye kijipicha au katika sekunde saba za mwanzo za video.
    • “Vurugu za kuogofya za michezo ” ni pamoja na majeraha mabaya (kama vile kukatwa vichwa, kukatwa kwa viungo vya mwili) yanayoangazia ugiligili na/au sehemu za mwili zilizo na maumivu makali au ya muda mrefu.
  • Uchezaji wa video unaoonyesha unyanyasaji wa kijinsia.
  • Uchezaji wa video unaoonyesha vurugu zinazochochewa na chuki au vurugu zinazolenga kikundi cha watu wanaolindwa.
  • Uchezaji wa video unaoonyesha mateso ya kuogofya.
  • Uchezaji wa video unaoonyesha vurugu ya kuogofya unaowalenga watoto.
  • Uchezaji wa video unaoonyesha vurugu ya kuogofya zinazolenga watu halisi waliotajwa.

Vifo & majanga

  • Maonyesho ya maiti ambao hawajaandaliwa au walio na majeraha yanayoogofya zaidi.
  • Maonyesho ya maiti ambao hawajaandaliwa katika muktadha usio wa elimu.
  • Maonyesho ya matukio ya kifo cha mtu mmoja au zaidi katika muktadha wowote.
    • Kifo kwa kukosa hewa.
    • Gari lenye wasafiri linaloonekana likianguka kutoka kwenye daraja.
  • Wakati unaodokezwa wa kifo au majeraha makubwa ya mwili.
    • Uharibifu mkubwa wa mali ambapo kifo au majeraha makubwa ya mwili yanaweza kutokea (kama vile milipuko, moto, kuanguka kwa majengo n.k).
  • Mwonekano wa maiti wanaoogofya licha ya kuhaririwa (kama vile kutiwa ukungu) katika muktadha usio wa elimu.

Mapigano (bila kujumuisha mapambano ya spoti)

  • Kuangazia au kuonyesha kwa muda mrefu mapigano mtaani, hata bila majeraha, katika miktadha isiyo ya elimu.

Uwindaji

  • Maudhui ya uwindaji yanayoangazia picha zinazoogofya za wanyama waliojeruhiwa au wanaoteseka (kama vile sehemu za mwili zenye damu).

Unyanyasaji kwa wanyama

  • Maonyesho ya unyanyasaji kwa wanyama (kimwili na kihisia) au ukatili kwa wanyama, kama vile kupiga teke.
  • Kutangaza au kuhimiza vurugu kwa wanyama inayodhibitiwa na binadamu (kama vile vita vya majogoo au mbwa) ambako kunaweza kujumuisha au kutojumuisha picha zinazoogofya.
  • Video ya wanyama wakiwa katika dhiki inayosababishwa na matendo ya wanadamu, kama vile kuweka mnyama kimakusudi katika njia ya kuumiza, katika hali zinazochosha au matukio mengine hatari yanayosumbua au yasiyo halisi.

Utekelezaji wa sheria na majibizano makali

  • Maonyesho yanayoangazia ukatili wa polisi katika muktadha usio wa elimu.

Vurugu katika uchezaji wa spoti

  • Video za spoti ambapo onyesho la majeraha ya kuogofya ni mada kuu ya video.

Vita na migogoro

  • Picha zinazoogofya au masimulizi ya ufyatuaji, milipuko, mauaji au bomu.
  • Video ya vita iliyo na maonyesho yanayoogofya ya majeraha, kifo au mateso katika muktadha wowote.

Vurugu kuhusu watoto

  • Maudhui yanayoangazia vurugu dhidi ya watoto katika muktadha wowote au yanayoangazia majeraha au dhiki kwa wahusika.

Ili upate maelezo zaidi kuhusu hoja muhimu zilizotumiwa kwenye mwongozo huu, angalia jedwali letu la ufafanuzi.

Maudhui ya watu wazima

Maudhui yanayoangazia maudhui ya ngono kwenye jina au kijipicha au mada za kingono hayafai kwa utangazaji. Kuna vizuizi vichache kwa video za muziki na video za elimu ya ngono isiyo dhahiri. Sera hii inajumuisha video halisi na video za madoido zilizotengenezwa kwa kompyuta. Kubainisha kuwa dhamira ya maudhui ni ucheshi hakufanyi maudhui yanayoangazia ngono yafae kwa utangazaji.

Maelezo ya Sera
Mwongozo wa matangazo Maelezo na chaguo za dodoso
Maudhui haya yanaweza kutumika kuchuma mapato ya matangazo

Mahaba au kupiga busu; mazungumzo kuhusu uhusiano wa kimahaba au kimapenzi bila kurejelea tendo la ngono; uchi uliofichwa kabisa usioonekana na usiolenga kuchochea hadhira kingono; uchi unaohusisha tendo la kunyonyesha ambapo mtoto anaonekana; elimu kuhusu ngono bila kudhihirisha tendo lenyewe; kucheza dansi katika hali inayohusisha miondoko ya sehemu za mwili ambazo kwa kawaida huhusishwa na tendo la ngono katika juhudi za kutaka kutamaniwa au kuvutia, lakini hazionyeshwi dhahiri kingono; kucheza dansi ya kingono katika mazingira ya kitaaluma, kama vile katika dansi au video ya muziki iliyopangwa.

Baadhi ya mifano ya maudhui ambayo pia yanapatikana katika aina hii:

Maudhui yanayochochea ngono

  • Matukio ya mahaba ambayo hayachochei ngono, kama vile matukio ya kupapasa au kubusu yaliyohuishwa, halisi au ya kuigiza.
    • Matukio yanayohusisha hisia za kingono kati ya wahusika bila maonyesho dhahiri ya vitendo vya ngono.
    • Tukio la kupiga busu katika masimulizi mapana ambapo lengo ni mahaba na halinuiwi kuchochea kingono.
    • Matendo ya muda mfupi ya ngono isiyo dhahiri bila kuonyesha sehemu nyeti kama vile, kuonyesha kitanda kinachotetemeka, kutoa sauti za ngono au kugusana kingono.
  • Majadiliano ya ngono katika miktadha ambayo haichochei ngono au ya ucheshi:
    • Maneno ya wimbo au mazungumzo yanayorejelea hisia kali, ashiki au tamaa ya ngono.
    • Elimu ya ngono.
    • Magonjwa ya zinaa (STD) na jinsi yanavyoenezwa.
    • Hali za kingono (kama vile kukabili uchungu baada ya tendo la ngono) zinazoangazia tu jinsi ambavyo ngono hufanyika na hazielezei jinsi ya kuboresha utendaji.
    • Kuchanga mbegu za kiume.
    • Maonyesho ya kisayansi ya viungo vya uzazi kwa kutumia picha au michoro au miigo.
    • Mwelekeo wa kingono na/au jinsi utambulisho wa ngono hubadilika katika mahusiano.
    • Matumizi ya mizaha ya ngono au madokezo (kama vile kuiga vitendo vya ngono katika hali ya ucheshi) ambayo hayatumii maneno machafu (kama vile maneno ya muziki yanayorejelea mvutano wa ngono).
    • Maudhui yanayorejelea mapendeleo ya ngono yasiyo ya kawaida kwa njia isiyo ya kingono (kama vile “unapenda chakula kipi au unatamani chakula gani?”).

Dansi

  • Miondoko ya dansi ya kingono, kama vile kucheza dansi kwa kuonyesha sehemu za siri au kutikisa nyonga au kunengua kiuno.
  • Kucheza dansi kwa kutingisha makalio au kugusisha sehemu za siri.
  • Kucheza dansi na kudhihirisha sehemu za mwili kwa mavazi mafupi.
  • Kuonyesha tendo la kupapasa sehemu za siri za mwili.
  • Wahusika wanaocheza dansi kwa kukaribiana kimwili. Kwa mfano, kukaribiana kwa sehemu zao za nyonga.
  • Miondoko ya dansi inayoiga vitendo vya ngono, kama vile dansi ya kugusana kwa sehemu za nyonga au kupakataliwa kingono, inayowasilishwa katika mazingira ya kitaalamu (k.m. studio za kucheza dansi).
  • Video za muziki zenye picha zinazorudiwa za sehemu za siri za mwili.

Uchi

  • Uchi uliobanwa ambako uchi si lengo kuu, kama vile matukio ambako huenda wahusika wako uchi lakini hamna chuchu, makalio au sehemu za siri zinazoonekana (kama vile zimetiwa ukungu au kupunguza ubora wa picha kikamilifu).
    • Uchi uliotiwa ukungu wa watu wa kihistoria wakiwa wamevaa mavazi yasiyoficha uchi kabisa katika muktadha wa elimu.
    • Sehemu za siri zilizobanwa kikamilifu zisizoweza kubainika na huonyeshwa kwa madhumuni yasiyo ya ngono, kama vile taratibu za matibabu.
  • Maonyesho ya watu wakiwa wamevaa mavazi yasiyoficha uchi kabisa ambako maonyesho hayalengi kuchochea ngono, kama vile bikini zinazovaliwa kwenye ukumbi wa kuogelea.
    • Maoni kuhusu mavazi yanayolenga muundo na umuhimu wa mavazi badala ya kulenga sehemu zilizofunikwa na nguo, kama vile chuchu.
    • Maonyesho ya sanaa, kama vile sanamu, michoro au picha zilizotengenezwa na kompyuta zinazojumuisha uchi katika michoro, kama vile wahusika katika sanaa au picha ya watu wa zamani katika nguo zinazofunika kiuno pekee.
    • Mavazi yanayoonyesha viungo vya mwili au mavazi yanayofunika tu matiti au makalio ya wanawake au misuli ya wanaume yanayoonekana katika muktadha unaofaa, kama vile maonyesho ya mitindo, majaribio ya kimatibabu au katika fuo za burudani.
    • Uchi unaoonekana kwa kiasi kidogo kama sehemu ya spoti kama vile mchezo wa ndondi, ambako mavazi kama hayo yanaweza kuhitajika.
    • Matiti au makalio ambayo hayajafunikwa au yamefunikwa kidogo (kama vile wakati mtu amevaa mavazi ya kuogelea) yasiyochochea ngono na si lengo kuu la video.
  • Vifaa vinavyotumiwa kuiga uzito au kuonekana kwa sehemu za siri kwenye mwili, bila kujumuisha vifaa vinavyotumiwa kuchochea ngono.
    • Matiti ya bandia yanayotumiwa na wale ambao wamefanyiwa upasuaji wa matiti, au watu waliobadilisha jinsia na/au wasiojitambulisha kwa jinsia ya kike au kiume.
    • Vifaa vinavyotumiwa na jumuiya ya waliobadilisha jinsia na/au wasiojitambulisha kwa jinsia ya kike au kiume, kama vile vifaa vya kukojoa ukiwa umesimama wima au vifaa vinavyofanana na sehemu nyeti za wanaume. 

Uchi unaohusisha kunyonyesha

  • Mwanamke anayenyonyesha mtoto wake bila kufunika matiti au matiti yake yakiwa yanaonekana.
  • Kuonyesha kwa ishara ya mikono au matumizi ya pampu ya kukamua maziwa ya mama huku chuchu zikionekana na kuna mtoto katika tukio.

Ufafanuzi:

  • “Yanayolenga ngono” hurejelea lengo la kuchochea hadhira kingono.
  • “Madokezo ya kingono” hurejelea matumizi yoyote ya maneno ili kupendekeza au kufanya mzaha kuhusu jambo la kingono.
  • “Yanayochochea ngono” hurejelea video, sauti au maandishi yanayodokezea lengo la kuchochea hadhira kingono.
  • “Ubayana” hurejelea kiwango cha kuonyesha kitendo cha ngono au uchi ili kusisimua hadhira.
  • “Uchi unaohusisha kunyonyesha” hurejelea matiti na/au chuchu zilizo dhahiri katika muktadha wa kunyonyesha. Ni lazima ujumuishe marejeleo ya kitendo cha kunyonyesha katika muktadha huo, kama vile mtoto anayejiandaa kunyonya au anayeendelea kunyonyeshwa.
Maudhui haya yanaweza kuchuma mapato machache au yasichume kabisa mapato ya matangazo

Sanaa ya zamani inayoonyesha tendo la ngono linaloweza kubainika (kama vile picha ya tendo la ndoa) au kuangazia sehemu za siri kwenye vijipicha; elimu kuhusu ngono isiyo ya kusisimua yenye vitendo vya ngono vilivyohuishwa; mizaha inayohusisha mada za ngono; kucheza dansi kwa kuangazia mavazi mafupi; kugusa kimakusudi au kuangazia sana sehemu za siri kwenye dansi.

Baadhi ya mifano ya maudhui ambayo pia yanapatikana katika aina hii:

Maudhui yanayochochea ngono

  • Mada au vijipicha vilivyo na mandhari ya kingono (ikiwa ni pamoja na ishara zinazopotosha).
    • Video za muziki zenye vijipicha au mada zilizo na mandhari ya kingono (ikiwa ni pamoja na ishara zinazopotosha).
    • Maelezo au marejeleo yasiyo dhahiri ya shughuli za kingono (kama vile marejeleo yasiyo dhahiri ya sehemu nyeti kwa kutumia emoji au picha).
    • Kuashiria au kuvutia hadhira kwenye kitu kupitia kijipicha kinachopendekeza matendo ya ngono yanayodokezwa.
    • Wafanyabiashara ya ukahaba kuangaziwa kama huluki.
    • Vitendo vya ngono (Ikiwa ni pamoja na matendo yanayoashiria ngono).
    • Madokezo ya kingono, kama vile sauti za miguno au kulamba sikio.
    • Vifaa vya ngono vilivyoangaziwa kwenye maudhui hata ambapo havitumiki. 
  • Maonyesho ya vitendo vya ngono visivyo vya kusisimua katika maudhui ya elimu, filamu ya hali halisi au maigizo.
    • Vitendo vya ngono na historia zake, vinavyofafanuliwa kwa madhumuni ya elimu, kama vile mada za kimatibabu.
  • Maudhui yanayohusiana na ngono, kama vile filamu za hali halisi kuhusu sekta ya ngono.
  • Maudhui ya elimu au hali halisi yaliyo na:
    • Mazungumzo kuhusu vitendo vya kingono, kama vile vidokezo vya binafsi ambavyo mtu alivyojifunza akiwa mfanyabiashara ya ukahaba au lugha chafu inayotumiwa kama sehemu ya mazungumzo ya kingono.
  • Mada au kijipicha kinachoangazia maudhui ya watu wazima katika sanaa za zamani.

Dansi

  • Dansi ya kutingisha makalio au kugusisha sehemu za siri inayoangazia mavazi mafupi ya anayecheza dansi.
  • Dansi ambapo mhusika mmoja ananyakua matiti au makalio ya mwenzake au ambapo mhusika mmoja anaingiza mikono yake ndani ya mavazi ya mwenzake.
  • Kuvuta karibu sehemu za siri za mwili kwa kukusudia katika dansi.

Uchi

  • Maudhui ya elimu au filamu za hali halisi zinazoangazia uchi wote.
    • Mihtasari ya historia au sekta inayohusiana na ngono au uchi, kama vile kuonyesha mwili wote ukiwa umepakwa rangi.
  • Sanaa za zamani zinazoangazia sehemu za siri zinazoonekana.

Ufafanuzi:

  • “Uchi uliobanwa” hurejelea mambo kama vile kutia ukungu, kuficha uchi kwa kutumia pau nyeusi au kupunguza ubora wa picha.
  • Tendo la ngono lisilo dhahiri: Tabia inayoiga kitendo cha ngono kama vile kugusana kingono.
Maudhui haya hayatachuma mapato ya matangazo

Sehemu za siri za mwili zilizofunikwa kidogo au uchi kabisa; uchi wa kunyonyesha bila mtoto kuwepo katika tukio; vitendo vya kingono (hata kama vimetiwa ukungu au kukisiwa), majadiliano ya mada za ngono, kama vile mapendeleo ya ngono yasiyo ya kawaida, vidokezo, hali za kushiriki tendo hili; kijipicha cha video kilicho na maudhui ya ngono (ikiwa ni pamoja na maandishi au viungo); ishara na matukio yanayochochea ngono; kuonyesha vifaa vya ngono; maudhui yanayohusiana na tasnia na wafanyakazi wa ngono; ngono kati ya wanyama inayoangazia sehemu za siri au matukio ya kujamiiana; kuiga mienendo au vitendo vya ngono katika kudensi; densi za wazi zenye ashiki za ngono zinazolenga kuchochea hadhira kingono.

Baadhi ya mifano ya maudhui yanayopatikana pia katika aina hii:

Maudhui yanayochochea ngono

  • Mada au vijipicha vilivyo na mandhari ya kingono (ikiwa ni pamoja na ishara zinazopotosha).
    • Ufafanuzi au marejeleo yasiyo dhahiri ya shughuli za kingono (kama vile marejeleo yasiyo dhahiri ya sehemu nyeti kupitia emoji au picha).
    • Kuashiria au kuvutia hadhira kwenye kitu kupitia kijipicha kinachopendekeza matendo ya ngono yanayodokezwa.
    • Mada ya kupotosha ambako video inaahidi maudhui ya ngono, lakini hayapo (kama vile video ya kupika yenye mada “tazama ponografia”).
    • Uchi uliobuniwa na kompyuta katika muktadha wa matibabu.
  • Tabia au kitendo cha ngono kinachoangaziwa na kisicho dhahiri.
    • Mada kuu ya video inadokeza vitendo vya ngono vinafanyika, kama vile vifaa vinavyotetemeka, sauti za ngono, n.k.
  • Maonyesho ya vinyago vya ngono, vifaa vya ngono, au bidhaa nyingine zinazonuiwa kuboresha vitendo vya ngono hata kama hazitumiwi.
    • Kuonyesha kimakosa kifaa cha ngono katika video, ambacho hakihusiani na mada za ngono (kama vile kuonyeshwa katika mandhari ya nyuma).
    • Kifaa cha kimatibabu kinachofanana na sehemu za siri kinapoonyeshwa wakati wa mjadala.
  • Matukio yanayoonyesha picha za dansi za kingono, kupapasa au kuiga ili kuchochea hadhira kingono.
    • Matukio mafupi kuhusu vitendo vya ngono (ikiwa ni pamoja na matendo ya kingono yasiyo dhahiri) kama sehemu ya masimulizi mapana.
    • Matukio ambako lengo kuu ni kuonyesha hisia za ngono.
  • Madokezo ya kingono kwa kutumia vifaa ambavyo havichochei ngono:
    • Vifaa vinavyofanana na sehemu za siri kama vile maumbo ya binadamu yaliyo na sehemu za siri halisi.
    • Matumizi ya vifaa vya kawaida (kama vile. biringanya) au emoji zinazonuiwa kufanana na sehemu za siri na kuchochea hadhira kingono.
  • Sauti, maandishi au mijadala dhahiri ya kingono:
    • Burudani inayohusiana na ngono, kama vile ponografia au huduma nyingine za ngono (ikiwa ni pamoja na viungo vya usajili unaolipishwa wa mifumo ya maudhui ya watu wazima).
    • Uigaji au matendo dhahiri ya kingono yanayolenga kuchochea ngono.
    • Kuonyesha na vifaa vya ngono (kama vile mwongozo).
    • Ulengaji wa kashfa za kingono au kuonyesha nyenzo za faragha za ngono.
    • Kuiga shughuli za kingono (kama vile maudhui ya ponografia).
    • Kutangaza vitendo vya ngono kwa lengo la kulipwa.
    • Matumizi halisi ya vifaa vya ngono (au bidhaa nyingine zinazonuiwa kuchochea vitendo vya ngono).
    • Tabia inayopotosha ya ngono au maudhui yanayohusiana na uchi.
      • Vijipicha vinavyolenga kupotosha watazamaji kwa kutumia maonyesho ya kingono ya vitu au matukio ya kawaida, mara nyingi ambayo hayahusiani na mada halisi ya video.
    • Matukio ambayo yamehaririwa kwa lengo la kuchochea kingono.
      • Mikusanyiko ya vitendo vinavyochochea ngono, kama vile matukio ya kufanya mapenzi au kugusana kingono.
      • Mada za maudhui yanayochochea ngono (kama vile "Kipindi kizuri cha ngono").
    • Ngono ya wanyama wakati:
      • Video za kupandana ambazo zinalenga sehemu nyeti.
      • Sehemu za siri za wanyama au vitendo vya kupandana vinavyoonyeshwa kwa njia inayochochea ngono.
  • Majadiliano ya hali za kingono, kama vile kupiga punyeto, mishindo, kufanya ngono, vidokezo au vitendo vingine vya ngono. Hii pia inaweza kujumuisha madokezo ya kingono au maandishi yenye matusi au sauti dhahiri ya kingono, kama vile mazungumzo ya kina kuhusu ngono.
    • Mijadala dhahiri kuhusu vidokezo vya ngono au jinsi ya kufanya ngono.
    • Mikusanyiko ya sauti za vitendo vya ngono bila picha au video za kitendo halisi (kama vile sauti za kulamba sikio au za kimahaba).
    • Maelezo ya shughuli za ngono yanayolenga kuchochea hadhira kingono.
    • Kutaja vifaa vya ngono hata kama havijafafanuliwa.
    • Mada au vijipicha vinavyorejelea maudhui ya watu wazima, kama vile 18+, 21+, ‘watu wazima pekee,’ ‘ponografia,’ n.k., isipokuwa iwe katika muktadha wa elimu au hali halisi.
    • Matumizi ya vikaragosi au emoji katika maandishi zinazowakilisha sehemu za siri za mwili au vitendo vya kuchochea watazamaji.
  • Michezo ya video ya kingono inayolenga watu wazima au kusawiri kingono wahusika katika mchezo wa video kwa lengo la kuchochea hadhira kingono.

Dansi

  • Miondoko ya kingono ambapo mhusika mmoja anagusa sehemu zake za siri kwenye sehemu za siri za mhusika mwenzake.
  • Mtu kujipanua au kupanua miguu yake akielekea alipo mwenzake kana kwamba wanashiriki tendo la ngono.
  • Kucheza dansi kwa kupakatana au kuvua nguo wakati wa kucheza, isipokuwa kama dansi iliyopangwa, video ya muziki au vinginevyo katika mazingira ya kitaalamu.

Uchi

  • Uchi uliobanwa au ambao ubora wa picha umepunguzwa ambako sehemu nyeti za mwili bado zinaweza kutambuliwa.
    • Matukio yanayoonyesha uchi uliofunikwa na nyota au kutiwa ukungu, lakini bado unaweza kutambulika kutokana na kivuli chake.
  • Maonyesho yasiyo ya muda mfupi ya uchi (yaliyohuishwa, halisi au ya kuigizwa).
    • Maudhui yanayoangazia (iwe kwa kulenga au kuonyesha mara kwa mara) matiti au sehemu za siri (kama vile maudhui yanayoangazia sehemu za siri za mtu "sehemu za siri zilizodinda" zilizotokeza kwenye nguo zake za ndani au za kuogelea).
  • Maonyesho ya sehemu za siri za mwili, kama vile picha zinazorudiwa au zinazolenga nafasi ya katikati ya matiti au maumbo yanayolenga kuchochea hadhira kingono.
    • Mikusanyiko ya michoro ya sehemu za siri zinazoweza kutambuliwa.
    • Sehemu nyeti za mwili zilizofunikwa kidogo (kama vile kwa chupi ya ugwe) (kama vile matiti, nafasi ya katikati ya matiti, makalio, n.k.,) zinazoonekana mara kwa mara.
  • Uchi halisi au uliohuishwa, kama vile kuonyesha sehemu nyeti za mwili au vitendo vya ngono. 
  • Uchi wa watoto
    • Maudhui yanayoonyesha sehemu za siri, kama vile wakati wa kubadilisha nepi au watoto wakiogelea bila mavazi yoyote.

Uchi unaohusisha kunyonyesha

  • Maudhui ya elimu kuhusu jinsi ya kutumia pampu ya kukama maziwa ya mama ambapo chuchu zinaonekana lakini hakuna mtoto mahali hapo.
  • Mafunzo kwa ishara za mikono ambapo chuchu zinaonekana na hakuna mtoto katika tukio.
  • Huonyesha mwanamke anayekama maziwa yake kwenye kikombe na hakuna mtoto katika tukio.

Ili upate maelezo zaidi kuhusu hoja muhimu zilizotumiwa kwenye mwongozo huu, angalia jedwali letu la ufafanuzi.

Maudhui ya kuogofya

Huenda maudhui yanayoweza kukera, kuudhi au kuogofya watazamaji yasifae matangazo. Vipengele vinavyoogofya ambavyo havijahaririwa si lazima visababishe video yako isifae matangazo, lakini muktadha ni muhimu.

Maelezo ya Sera
Mwongozo wa matangazo Maelezo na chaguo za dodoso
Maudhui haya yanaweza kutumika kuchuma mapato ya matangazo

Maudhui yanayoogofya kidogo au kiasi ambayo yamebanwa au yanaonyeshwa katika muktadha wa elimu, hali halisi au madhumuni mengineyo.

Baadhi ya mifano ya maudhui yanayopatikana pia katika aina hii:

Sehemu, ugiligili au uchafu wa mwili

  • Sehemu, ugiligili au uchafu wa mwili ambao unalenga watoto au unaonyeshwa katika muktadha wa elimu, sayansi, hali halisi au sanaa, ambapo lengo si kuogofya.
  • Sehemu, ugiligili au uchafu ulioigizwa ambapo lengo ni kuhofisha, hasa kwa madhumuni ya burudani (kama vile kiinimacho) lakini ambapo lazima muktadha halali utolewe.

Taratibu za kimatibabu na urembo

  • Taratibu za kimatibabu au urembo, zinazolenga kuelimisha na zinazoangazia utaratibu wenyewe badala ya sehemu, ugiligili au uchafu wa mwili.
    • Taratibu za chale, kutoboa mwili au za kuondoa mikunjo zenye kiasi kidogo cha damu.
  • Maonyesho yaliyohaririwa au ya muda mfupi ya sehemu, ugiligili au uchafu wa mwili wakati wa taratibu za kimatibabu au urembo.
  • Video za binadamu na wanyama wanaozaa, zenye malengo ya elimu kwa watazamaji, bila kuangazia zaidi sehemu, ugiligili au uchafu wa mwili.

Ajali na majeraha

  • Ajali ambako hamna majeraha yanayoonekana (kama vile sehemu ya ndani ya mwili, sehemu zinazovuja damu).
  • Ajali ambazo hazisababishi mfadhaiko halisi kutokana na athari kidogo tu inayoonekana (k.m. kuanguka kutoka kwenye pikipiki).
  • Ajali ambako mwathiriwa hana dhiki au maumivu kutokana na ajali (hamna kulia au kupiga mayowe kulikoonyeshwa).
  • Ajali ambako hamna matibabu ya muda mrefu yatahitajika.
  • Ajali na majeraha ambayo yanaonyeshwa katika muktadha wa habari, hali halisi au sanaa (kama vile filamu au video ya muziki).

Kutayarisha na kula wanyama

  • Kushughulikia sehemu za wanyama kwa njia ambayo haitishi.
    • Maonyesho ya nyama, samaki wakiwa katika hali ya kuandaliwa ili kuliwa, kama vile wakati wa kuonyesha mbinu za mapishi au maandalizi.
  • Kula au kuandaa kwa njia ya kutisha bidhaa za vyakula vya wanyama ambavyo havifanani na sehemu za wanyama.
    • Kula samakigamba katika mkahawa ambao wako hai au bado wanaonekana wakisonga.
    • Kula vyakula vilivyoandaliwa (kama vile uduvi) kama sehemu ya maonyesho ya “mukbang” au ASMR.
  • Maonyesho ya muda mfupi ya sehemu za wanyama na sifa dhahiri za uso (bila kujumuisha samaki, konokono, au krateshia, ambao wanaruhusiwa kuangaziwa kwa njia dhahiri).

Ufafanuzi

  • "Lengo la kuhofisha" hurejelea lengo la video la kutisha, ambalo hubainishwa na muktadha uliotolewa na pia lengo kuu.
  • "Ajali" hurejelea matukio yasiyotarajiwa ambayo kwa kawaida husababisha uharibifu au majeraha, ikiwemo hali ambapo jeraha lenyewe huenda lisionekane kwa njia wazi (kama vile ajali za magari).
  • "Kufichuliwa" hurejelea uonekanaji wa sehemu, ugiligili au uchafu wa mwili (kama vile tishu au damu).
  • "Mafadhaiko” hurejelea hisia mbaya au ya mshangao inayotokana na ajali au jeraha linaloonekana au linalokisiwa.
  • "Dhiki" hurejelea video, sauti au maonyesho yanayokisiwa ya kuteseka kwa watu kutokana na maumivu au kutokuwa na fahamu. Katika hali hii, inahusiana na watu waliohusika katika ajali na watu wanaopitia au kufanyiwa utaratibu wa kimatibabu au urembo (ukiwemo kujifungua).
  • “Hali isiyoshtua” (inapotumiwa katika muktadha wa sehemu za mnyama zilizo dhahiri au kula mnyama au mdudu) hurejelea njia inayoangazia matumizi ya chakula bila lengo la kuzua shauku kuhusu mnyama. Mnyama au jinsi anavyoliwa haikusudiwi kuogofya wala hamna maelezo ya kutisha au yaliyotiwa chumvi.
  • "Kutesa" hurejelea jinsi mnyama anatayarishwa au kuliwa katika njia ya kikatili au mbaya. Kwa mfano, kutupwa, kuangushwa, kuchezewa kwa burudani, kudungwa au kukatwa kichwa. Si lazima mnyama awe hai ili kushughulikiwa kwa njia isiyofaa na mateso haya yanaweza kufanywa kwa kutumia zana, vyombo au mikono.
  • "Muktadha wa kitaalamu" hurejelea taaluma ya kuwa mchinjaji au muuzaji wa samaki na miktadha ambapo wanakata na kutayarisha wanyama waliokufa.
  • "Sehemu dhahiri za uso" ni sehemu za uso zinazothibitisha kwa hadhira kuwa mnyama alikuwa hai au bado yuko hai. Sehemu zinajumuisha pua, masikio, mdomo, macho, n.k.
Maudhui haya yanaweza kuchuma mapato machache au yasichume kabisa mapato ya matangazo

Maudhui yanayoshtua, kama vile picha za sehemu za mtu au mnyama, ambazo hazijabanwa au zinakusudiwa kuogofya lakini bado kuna muktadha wa jumla.

Baadhi ya mifano ya maudhui yanayopatikana pia katika aina hii:

Sehemu za mwili, ugiligili au uchafu wa mwili

  • Kuangazia sehemu halisi za mwili, ugiligili au uchafu wa mwili ambapo lengo ni kushtua.
  • Maonyesho yaliyoigizwa ya sehemu za mwili, ugiligili na uchafu wa mwili, yanayoangazia maelezo ya kutisha na ya kikatili.
    • Matukio ya upasuaji katika maudhui ya kuigiza yaliyo na damu nyingi.

Taratibu za kimatibabu na urembo

  • Maudhui ya elimu au kisanii yaliyo na taratibu za kimatibabu au urembo zinazoangazia kuonyesha kwa kina sehemu za mwili, ugiligili au uchafu wa mwili ambao haujahaririwa, lakini ambapo sifa hizi si lengo kuu.
    • Upasuaji unaoangaziwa ambao haujahaririwa ambapo sehemu zinaonekana lakini si mada kuu ya video.
    • Mtaalamu wa matibabu akionyesha uondoaji wa uchafu masikioni au kupasua chunusi kwa kutoa maelezo ya hali hiyo.

Ajali na majeraha

  • Ajali ambapo kuna tukio kubwa la kugongana ambalo linaweza kuleta mfadhaiko.
  • Ajali ambako majeraha yanaonekana (kama vile kuona damu ikitoka kwenye nguo au nje ya gari), lakini ambapo hamna dhiki kwa mwathiriwa inayoweza kukisiwa.
  • Ajali kubwa ya gari ambapo hamna waathiriwa wanaoonyeshwa wakiteseka.

Kutayarisha na kula wanyama

  • Ulaji wa mnyama kwa njia ya kutisha “mukbang” au ASMR unaoonyesha sehemu za mnyama ambazo hazijaandaliwa au kula sehemu hizo kwa njia ya kikatili au isiyo ya kawaida.
  • Kuangazia sehemu za kiumbe hai zinazoweza kutambulika (kama vile kuangazia macho ya mnyama wakati wa kupika).
  • Sehemu za mnyama aliyechunwa ngozi na vitu vya kuogofya na kutisha, lakini hamna kushughulikia kusikofaa (k.m. kuangazia nyama na mishipa inayovuja damu katika sehemu za mnyama anayeandaliwa).
Maudhui haya hayatachuma mapato ya matangazo

Maudhui ya kuogofya zaidi ambapo lengo la video yote ni kuogofya watazamaji. Kwa jumla, hakuna muktadha uliotolewa, huku vitu vya kuogofya na kutisha, hali ya hatari au kutesa ni wazi na dhahiri.

Baadhi ya mifano ya maudhui yanayopatikana pia katika aina hii:

Sehemu za mwili, ugiligili au uchafu wa mwili

  • Maonyesho ya kukera au kutisha ya kikatili ya sehemu ya mwili, ugiligili au uchafu wa mwili yenye muktadha mdogo au yasiyo na muktadha wowote.
    • Uchafu wa masikio au kupasua chunusi bila ufafanuzi dhahiri wa utaratibu, ambapo sehemu kubwa ya video inaangazia sehemu za mwili, ugiligili au uchafu wa mwili, hata katika miktadha ya elimu.
  • Maigizo ya sehemu za kutisha zinazoonyeshwa, zenye muktadha mdogo, lengo kuu likiwa kushtua.

Taratibu za kimatibabu na urembo

  • Sehemu za mwili, ugiligili au uchafu wa mwili ambao haujahaririwa unaoonyeshwa kwa kiasi kikubwa cha video na ambazo zinaogofya na kutisha hata kama kuna muktadha.
    • Wataalamu wa matibabu wakielezea jinsi ya kutelekeza upasuaji mahususi.
  • Taratibu za matibabu zinazoonyeshwa bila muktadha au zenye muktadha unaopotosha, ambapo sehemu kubwa ya video inaonyesha sehemu za mwili, ugiligili, au uchafu unaoogofya.

Ajali na majeraha

  • Maonyesho ya kufadhaisha ya ajali na majeraha mabaya zaidi ambapo sehemu za mwili zinaweza kuonekana au ambapo majeraha mabaya yanaweza kutokea.
    •  Kuonyesha kuvuja damu na sehemu iliyoumia inaonekana.
  • Ajali mbaya zaidi bila muktadha.

Kutayarisha na kula wanyama

  • Kuonyesha, kuandaa au kula wanyama walio hai ambapo lengo kuu ni kushtua watazamaji, mara nyingi kwa njia ya kuogofya.
  • Kuangazia kwa uzito sehemu dhahiri za uso au kutesa mnyama bila muktadha.
  • Maonyesho ya kikatili au yanayoogofya ya maandalizi (kuchunwa ngozi) au mauaji ya wanyama wanaoonekana kuwa na dhiki.
  • Maonyesho yasiyo ya elimu ya maandalizi ya kula wanyama walio hai wanaoonekana kuwa na dhiki.
  • Maonyesho yasiyo ya elimu ya kula wanyama kwa kuangazia sehemu dhahiri za uso.

Ili upate maelezo zaidi kuhusu hoja muhimu zilizotumiwa kwenye mwongozo huu, angalia jedwali letu la ufafanuzi.

Vitendo hatari na maudhui yasiyothibitishwa

Maudhui yanayotangaza matendo hatari au ya kuumiza yanayosababisha majeraha ya kimwili, kihisia au kisaikolojia hayafai kwa matangazo.

Maelezo ya Sera
Mwongozo wa matangazo Maelezo na chaguo za dodoso
Maudhui haya yanaweza kutumika kuchuma mapato ya matangazo

Matukio au matendo ambayo ni hatari kiasi lakini yanatekelezwa katika mazingira yanayodhibitiwa na ya kitaalamu ambako hamna anayejeruhiwa vibaya. Marejeleo mafupi ya mashirika hatari katika maudhui ya elimu au ya kuigiza.

Baadhi ya mifano ya maudhui ambayo yanapatikana pia katika aina hii:

Vitendo vya jumla vilivyo hatari

  • Shughuli ambapo hatari ipo bila majeraha yanayoweza kuonekana kama vile:
    • Vitendo vya kitaalamu au spoti hatari zaidi kama vile kupaa kwa mabawa bandia.
    • Video ya mtu akiendesha baiskeli au pikipiki kwa gurudumu moja au kukwepa vizuizi kwa kasi.
    • Magari yakiendeshwa kwa kasi au yakienda kombo bila kufanya mambo hatari (kama vile kuendeshwa kwa magurudumu ya upande mmoja au bila kugusa usukani) au kusababisha usumbufu kwa wengine (kama vile kuendeshwa katikati ya barabara).

Mikusanyiko ya matukio ya kuanguka

  • Video za mikusanyiko ya matukio ya kuanguka bila kuangazia majeraha ya kuogofya (kama vile kujigonga kwenye mlango wa vioo). 

Mizaha na changamoto

  • Mizaha au mashindano ambapo kuna mshangao, kuchanganyikiwa au wasiwasi lakini hamna hatari au madhara ya muda mrefu kama vile mashindano ya kumiminiana maji baridi.
  • Majadiliano au ripoti kuhusu mizaha au mashindano hatari bila video au sauti inayoelezea wakati wa hatari (kama vile ripoti kuhusu mashindano ya moto bila maelezo ya tukio).
  • Maudhui ya elimu, hali halisi au taarifa ya habari inayoonyesha mizaha au mashindano yanayosababisha dhiki ya kihisia (kama vile kupigana, lugha chafu na matusi, kama vile mizaha ya “umefutwa kazi!”).

Maelezo ya kupotosha ya kimatibabu na kisayansi

  • Maudhui ambayo hayajabainishwa kuhusu virusi, magonjwa ya kuambukizana na COVID-19 bila lengo la kutia hofu (kama vile video ya watoto kuhusu tofauti ya virusi na bakteria).

Maelezo hatari ya kupotosha

  • Maudhui ya kielimu au filamu ya hali halisi yanayojaribu kufafanua jinsi makundi yanayotangaza maelezo hatari ya kupotosha yanavyokua, kujulikana na/au kusambaza maelezo ya kupotosha.
  • Maudhui ya elimu au hali halisi yanayolenga kukanusha maelezo hatari ya kupotosha kama vile Pizzagate, QAnon, StopTheSteal, n.k.
  • Maudhui ya elimu au hali halisi yanayolenga kutoa maelezo ya kupotosha kuhusu mabadiliko ya tabianchi.

Kuvuta mvuke na tumbaku 

  • Matangazo kwa umma yenye hatua za uzuiaji.
  • Maudhui yaliyoigizwa yanayoangazia matumizi.
  • Maudhui ya elimu au hali halisi yanayoonyesha sekta za tumbaku au mivuke.

Pombe

  • Uwepo wa pombe au watu wazima wakinywa pombe katika maudhui bila kutangaza au kuhimiza unywaji wa pombe bila kuwajibika.

Mashirika ya kigaidi ya kigeni (FTO)

  • Maudhui ya elimu, ripoti za wanahabari, au video za muziki zinazojadili shambulizi la kigaidi kama mada kuu.
  • Maudhui ya elimu, au yaliyoigwa kuhusu vikundi hivi kuwa mada ya jumla bila video ya mashambulizi ya kigaidi.
  • Ripoti za kihabari zinazoangazia makundi ya kigaidi ya kigeni au ugaidi kwa lengo la kuchekesha.
  • Ripoti zenye maudhui ya kuelimisha, yaliyoigizwa, ya kihabari au video za muziki zinazoangazia picha za FTO lakini vinginevyo hazijatajwa kama mada kuu ya maudhui. 

Makundi ya ulanguzi wa dawa za kulevya (DTO)

  • Ripoti zenye maudhui ya kuelimisha, yaliyoigizwa, ya kihabari au video za muziki zinazolenga ulanguzi wa kimataifa wa dawa za kulevya kwa jumla.
  • Ripoti zenye maudhui ya kuelimisha, yaliyoigizwa, ya kihabari au video za muziki zinazoonyesha DTO na picha zinazohusiana kama vile kauli mbiu.
  • Ripoti ya elimu, uigizaji, ripoti ya kihabari au video za muziki zinazoangazia maudhui ya kuchekesha kuhusu DTO au ulanguzi wa kimataifa wa dawa za kulevya kama mada kuu.
  • Matangazo ya huduma kwa umma kuhusu vikundi vinavyohusiana yanayoangaziwa katika ripoti za wanahabari
  • Ripoti za kihabari ikiwa ni pamoja na matukio ya hali za vurugu na matendo kama vile utekaji nyara au uulizaji maswali unaofanywa na DTO.

Ufafanuzi:

  • “Kujeruhiwa vibaya” humaanisha majeraha ambayo hayawezi kutibiwa bila huduma inayofaa ya matibabu au hayawezi kutibiwa nyumbani kama vile kuvunjika mifupa, kuteguka kwa viungo vya mwili au kuvuja damu nyingi.
  • Ubadilishaji wa mwili unaweza kujumuisha mambo kama vile chale, kutoboa mwili au upasuaji wa kimatibabu.
  • “Maigizo” humaanisha maudhui yanayotokana na mswada kama vile filamu au mazingira dhahania.
Maudhui haya yanaweza kuchuma mapato machache au yasichume kabisa mapato ya matangazo

Maudhui yanayoonyesha madhara au maumivu ya mwili lakini hili si lengo la video, hii inajumuisha matendo yanayotekelezwa katika mazingira ambayo hayadhibitiwi na yasiyo ya kitaalamu. Mada kuhusu kiongozi wa shirika hatari au matangazo husika ya huduma kwa umma.

Baadhi ya mifano ya maudhui ambayo yanapatikana pia katika aina hii:

Vitendo vya jumla vilivyo hatari

  • Matendo yanayohusisha shughuli zenye hatari sana kama vile kukimbia juu ya majengo marefu au kuonyesha majeraha mabaya kama vile tukio la ajali ya kusketi.
  • Maudhui ya elimu, hali halisi au taarifa za habari kuhusu: 
    • Matendo hatari yenye majeraha ya kuogofya.
    • Watoto wanaohusika katika kamari au kuendesha magari yaliyobuniwa kutumiwa na watu wazima. 
  • Magari yanayoendeshwa kwa kasi au yanayoenda kombokombo na kufanya mambo hatari (k.m. kuendeshwa kwa magurudumu ya upande mmoja au bila kugusa usukani) au kusababisha usumbufu kwa wengine (k.m. kuendesha katikati ya barabara). 
  • Maudhui ya elimu, yaliyoigizwa au video ya muziki inayoonyesha vitendo hatari ambavyo vinajumuisha mtoto kama mshiriki au mwathiriwa.

Mikusanyiko ya matukio ya kuanguka

  • Maonyesho yanayolenga matukio yenye majeraha ya kuogofya ambayo hayasababishi kifo au ulemavu wa kudumu (k.m. mkusanyiko wa video za ajali za barabarani za pikipiki).

Mizaha na mashindano

  • Ripoti za elimu, hali halisi au habari kuhusu mzaha au shindano lililo na:
    • Vitisho au kuhimiza madhara ya kimwili au kiakili dhidi ya mtu mwenyewe au wengine kama vile kulala kifudifudi katikati ya reli ya treni. 
    • Matendo ambayo hayapaswi kuigwa kama vile mashindano ya kunywa dawa ya klorini na yanayoweza kusababisha hatari ya papo hapo kwa afya ya mtu.
  • Mizaha au mashindano yanayosababisha dhiki ya kihisia kama vile majibizano makali, lugha chafu na matusi. Haya yanaweza pia kujumuisha hatua za kuhatarisha maisha ya mtu kama vile mizaha ya kufutwa kazi au kuchochea hisia au kutishia mtu katika muktadha wa mahusiano (k.m. mizaha ya talaka ambapo mtu mmoja anatatizika kihisia, au mizaha ya kukamatwa na polisi katika familia, n.k.).
  • Mizaha inayojumuisha kiasi kikubwa cha ugiligili wa mwili au vurugu iliyokithiri.
  • Mashindano yanayojumuisha kula vitu visivyo vya sumu, vitu ambavyo haviwezi kuliwa kama vile kula gundi au chakula cha wanyama. Kula vitu vinavyoweza kuliwa ambavyo ni hatari vikiliwa kwa kiasi kikubwa kama vile pilipili, au vinavyosababisha athari kiasi kwa mwili. 

Kuvuta mvuke na tumbaku

  • Maoni kuhusu bidhaa au ulinganishaji wa bidhaa za tumbaku (k.m. ulinganishaji wa juisi ya mvuke).
  • Kutaja huduma za uraibu katika muktadha wa elimu au hali halisi.

Pombe

  • Maudhui ya elimu, hali halisi au yaliyoigwa yanayoangazia watoto wakinywa pombe au bidhaa za pombe. 

Makundi ya kigaidi ya kigeni (FTO)

  • Video za vichekesho zinazorejelea makundi ya kigeni ya kigaidi au ugaidi.
  • Maudhui ya elimu, hali halisi au video za muziki zinazoangazia kwa ucheshi makundi ya kigaidi ya kigeni. 
  • Picha za makundi ya kigaidi ya kigeni zilizoshirikiwa lakini si mada au mandhari kuu ya maudhui. 

Makundi ya ulanguzi wa dawa za kulevya (DTO)

  • Matangazo kwa umma kuhusu makundi hayo bila muktadha.
  • Maudhui ya elimu au hali halisi au matangazo ya huduma kwa umma kuhusu makundi ya ulanguzi wa dawa za kulevya (DTO).
    • Maudhui ya elimu ambayo kimsingi yanalenga viongozi wa DTO au DTO mahususi.
    • Yanaweza kujumuisha hali zisizoogofya za mashambulizi au matokeo yake, hali za mateka, n.k.
    • Matangazo kwa umma kuhusu vikundi vinavyohusiana.
    • Hali na vitendo vya vurugu kama vile utekaji nyara au kuulizwa maswali kunakofanywa na DTO. 

Ufafanuzi:

  • “Athari kiasi kwa mwili” hurejelea mambo kama vile kuhisi kutapika bila sababu, kikohozi kinachosababisha kutapika.
Maudhui haya hayatachuma mapato ya matangazo

Kimsingi, maudhui yanaonyesha ajali, usungusungu, mizaha au matendo hatari kama vile majaribio au matendo yenye hatari za kiafya (kama vile kunywa au kula visivyoweza kuliwa); mijadala ya video zinazovuma zinazoonyesha aina hii ya maudhui. Kusifu, kuandikisha au maonyesho ya kuogofya ya mashirika hatari.

Baadhi ya mifano ya maudhui ambayo yanapatikana pia katika aina hii:

Vitendo vya jumla vilivyo hatari

  • Uhimizaji wa matendo hatari au matendo yanayokisiwa kuwa hatari.
    • Magari katika matukio na majeraha ya kushtua (k.m. tukio la kugongana au kuonyesha mtu aliyepoteza fahamu barabarani baada ya kugongwa na lori).
  • Watoto wanaohusika katika kamari au kuendesha magari yaliyobuniwa kutumiwa na watu wazima.
  • Matendo hatari yanayojumuisha mtoto kama mshirika au mwathiriwa.

Mikusanyiko ya matukio ya kuanguka

  • Mikusanyiko ya matukio ya kuanguka inayojumuisha shughuli zinazosababisha kifo au uharibifu mbaya (usioweza kubadilishwa au unaofanya mtu apoteze fahamu, kifafa, ulemavu, n.k.). 

Mizaha na mashindano

  • Mizaha au mashindano ambayo hayapaswi kuigwa kama vile mashindano ya kunywa klorini na yanayoweza kuhatarisha pakubwa afya ya mtu papo hapo.
  • Mizaha au mashindano yanayohusiana na: 
    • Kujiua, kifo, ugaidi kama vile mizaha ya kilipuzi bandia, au vitisho kwa kutumia silaha hatari.
    • Matendo yasiyotakikana ya ngono kama vile kubusu kwa nguvu, kugusa kingono, unyanyasaji wa kingono, kamera za upelelezi katika vyumba vya kubadilisha nguo.
    • Madhara ya mwili au dhiki ambapo dhiki hiyo si lengo kuu la video.
    • Dhiki ya muda mrefu ya kihisia kwa mtoto kama vile mzaha wa muda mrefu unaofanya mtoto aogope au afadhaike. Inaweza kujumuisha kumfanyia mtoto mzaha aamini kuwa wazazi wake wamekufa.
    • Vitisho au kuhimiza madhara ya kimwili au kiakili dhidi ya mtu mwenyewe au wengine kama vile kulala kifudifudi katikati ya reli ya treni.
    • COVID-19, inayohimiza shughuli hatari kama vile kujiweka kimakusudi katika hali ambapo unaweza kupata virusi au kuleta wasiwasi (k.m. kikundi cha watu ambao hawataki kujitenga au kujifanya umeambukizwa ukiwa katika eneo la umma).
    • Kutangaza matumizi ya silaha kwa nia ya kudhuru wengine.
    • Kuonyesha matumizi ya vitu kwa kiasi ambacho kinasababisha hali zinazoogofya kama vile kutapika baada ya kula pilipili kali.
    • Mashindano ambayo, yakirudiwa, yanaweza kusababisha madhara makubwa kama vile mashindano ya moto au shindano la 'bird box'.
    • Kuhimiza shughuli za ulaghai au zisizo halali (k.m. kuvunja na kuvamia jengo).

Maelezo ya kupotosha ya kimatibabu na kisayansi

  • Kutangaza madai au desturi hatari kwa afya au matibabu:
    • Kukataa uwepo wa hali zilizothibitishwa za afya, kwa mfano, Virusi vya Ukimwi.
    • Video zinazohimiza au kutoa maagizo kuhusu suluhu ya hali za afya ambazo hazijathibitishwa kisayansi (k.m. kuponyesha saratani kupitia chaguo za vyakula).
    • Kueneza maelezo ya kupotosha yanayopinga ukweli uliothibitishwa wa matibabu na kisayansi, kama vile kupinga upokeaji wa chanjo.
    • Maudhui yanayotangaza au kuruhusu mipango au huduma za kushawishi watu kuwa mashoga.
  • Kutangaza au kuhimiza maelezo hatari ya kupotosha kuhusu COVID-19:
    • Maudhui yanayohimiza watu wasipokee chanjo ya COVID-19.
    • Madai ya uongo au ya kupotosha kuhusu athari au usambazaji wa chanjo. Madai haya yanaweza kujumuisha:
      • Madai kuwa chanjo itasababisha utasa. 
      • Madai kuwa chanjo ina chipu ndogo. 
      • Madai kuwa chanjo zinaweza kutumiwa kuua kwa upole aina fulani ya watu.
    • Madai kuwa barakoa au umbali wa kutengana haupunguzi hatari ya kupata au kuenezwa kwa COVID-19.
    • Madai kuhusu kuenezwa kwa COVID-19 ambayo hayatokani na ukweli uliohakikishwa kimatibabu au kisayansi (k.m. kuwa inasambazwa kupitia mtandao wa kielektroniki wa 5G).
    • Video zinazohimiza au kutoa maagizo kuhusu suluhu za COVID-19 ambazo hazijathibitishwa kisayansi (k.m. kudungwa sindano ya Hydroxychloroquine).

Maelezo hatari ya kupotosha

  • Kutoa madai ya uwongo ambayo kwa kiwango kikubwa yanaweza kudhoofisha ushiriki au imani katika michakato ya kidemokrasia au uchaguzi.
    • Taarifa zinazoweza kuthibitishwa kuwa si za kweli kuhusu taratibu za upigaji kura wa umma, ustahiki wa mgombea wa kisiasa kulingana na umri au mahali alipozaliwa, matokeo ya uchaguzi au ushiriki wa sensa unaokinzana na rekodi rasmi za serikali.
  • Kutangaza maelezo hatari ya kupotosha (k.m. Pizzagate, QAnon, StopTheSteal).
  • Kuhimiza vikundi vinavyotangaza maelezo hatari ya kupotosha.
  • Kupinga maelezo yanayoaminika ya kisayansi kuhusu kuwepo na sababu za kubadilika kwa hali ya anga.

Kuvuta mvuke na tumbaku 

  • Kutangaza tumbaku na bidhaa zinazohusiana na tumbaku na matumizi yake.
  • Video za watoto wanaotumia bidhaa za mvuke/tumbaku.
  • Kuwezesha uuzaji wa bidhaa za tumbaku au mivuke.
  • Matumizi ya bidhaa za mivuke au tumbaku kwa njia ambayo haikunuiwa na mtengenezaji (k.m. kunywa juisi ya mvuke wa nikotini). 

Pombe

  • Kuonyesha watoto wakinywa pombe, hata kama si mada kuu ya video. 
  • Kutangaza unywaji wa pombe kwa watoto.

Mashirika ya kigaidi ya kigeni (FTO)

  • Video zisizo za elimu zinazoangazia FTO au mada za ugaidi, kama vile: 
    • Mijadala kuhusu shambulizi la kigaidi kama mada kuu.
    • Picha au majina yanayohusiana na kundi au viongozi mahali popote kwenye maudhui (kama vile katika kijipicha).
  • Maudhui yanayoangazia picha za kuogofya, kushtua na/au za vurugu, au matukio ya uchochezi au yanayosifu vurugu.
  • Maudhui yaliyobuniwa na au yanayosaidia makundi ya kigaidi.
  • Maudhui yanayosifu au kukanusha mashambulizi ya kigaidi.

Mashirika ya ulanguzi wa dawa za kulevya (DTO)

  • Video zisizo za elimu zinazolenga DTO mahususi, viongozi wa DTO au ulanguzi wa kimataifa wa dawa za kulevya.
    • Majadiliano yasiyokusudiwa, yasiyo na utaratibu kuhusu mada hii katika video humaanisha kuwa "si ya kielimu", kwa kuwa hakuna tangazo dhahiri kuwa lengo la video ni kufafanua mada.
  • Maonyesho yasiyo ya elimu ya picha zinazohusiana na DTO kama vile bendera, kaulimbiu, mabango, n.k.
  • Kuandikisha wanakikundi.
  • Muziki unaohusiana na “narcocorridos” au vinginevyo kusifu au kutangaza DTO.
  • Hali na vitendo vya vurugu kama vile utekaji nyara au uulizaji maswali unaofanywa na DTO.
  • Maudhui ya vichekesho yanayoangazia DTO au ulanguzi wa kimataifa wa dawa za kulevya kuwa mada kuu.

Ili upate maelezo zaidi kuhusu hoja muhimu zilizotumiwa kwenye mwongozo huu, angalia jedwali letu la ufafanuzi.

Maudhui ya chuki na yanayodhalilisha

Maudhui yanayochochea chuki, kubagua, kudhalilisha au kudunisha mtu au kikundi cha watu hayafai matangazo. Maudhui ya vichekesho yanaweza kuruhusiwa. Kubainisha lengo lako la kuchekesha haitoshi na bado maudhui hayo huenda yasifae matangazo.

Maelezo ya Sera
Mwongozo wa matangazo Maelezo na chaguo za dodoso
Maudhui haya yanaweza kutumika kuchuma mapato ya matangazo

Maudhui yanayorejelea vikundi vya watu wanaolindwa au kukosoa maoni au vitendo vya mtu kwa njia isiyo na madhara.

Baadhi ya mifano ya maudhui ambayo yanapatikana pia katika aina hii:

  • Maudhui ya habari yanayoelezea kikundi kinacholindwa au ripoti katika njia isiyo ya chuki kuhusu ubaguzi ambao kikundi kama hicho kinaweza kupata, kama vile ripoti za habari kuhusu chuki kwa mashoga.
  • Maudhui ya kuchekesha yanayokashifu au kudokezea kudhihaki, kudunisha au maoni mengine ya kudhalilisha vikundi vya watu wanaolindwa.
  • Mijadala ya umma kuhusu vikundi vya watu wanaolindwa bila kuchochea chuki wala kuvikabili kwa vurugu.
  • Maudhui ya kisanaa yanayotumia istilahi nyeti au ishara kwa njia isiyo ya chuki kama vile katika video maarufu za muziki.
  • Maudhui ya elimu au hali halisi:
    • Maneno yaliyobanwa ya ubaguzi wa rangi au hoja za kushusha hadhi zilizo na lengo la kuelimisha hadhira (k.m. ny*ni).
    • Yaliyo na picha inayoangazia chuki.
  • Kukosoa maoni, mitazamo au vitendo vya mtu au kikundi cha watu bila lengo lolote la kuchochea au kushusha hadhi.

Ufafanuzi:

“Kikundi cha watu wanaolindwa” hurejelea vikundi vya sifa zilizo hapa chini. Kuchochea chuki, kubagua, kudhalilisha au kudunisha mtu au kikundi cha watu kulingana na sifa zilizo hapa chini hakuchukuliwi kufaa watangazaji.

  • Mbari
  • Ukabila au asili ya kikabila
  • Uraia
  • Dini
  • Ulemavu
  • Umri
  • Kuwa mwanajeshi aliyestaafu
  • Mwelekeo wa kingono
  • Utambulisho wa kijinsia
  • Tabia zozote nyingine zinazohusiana na ubaguzi au utengaji wa kimfumo.
Maudhui haya yanaweza kuchuma mapato machache au yasichume kabisa mapato ya matangazo

Maudhui ambayo huenda yanakera watu au vikundi, lakini yanatumiwa kwa sababu za kielimu, habari au katika ripoti ya hali halisi.

Baadhi ya mifano ya maudhui ambayo yanapatikana pia katika aina hii:

  • Hotuba au mijadala ya kisiasa inayoweza kujumuisha lugha ya kukera lakini inalenga kutoa mafunzo, kama vile mijadala ya kisiasa kuhusu haki za wabidili jinsia.
  • Maudhui ya elimu:
    • Maneno ya ubaguzi wa rangi au hoja za kudunisha zisizobanwa zenye lengo la kuelimisha hadhira. (k.m. matusi kwa misingi ya rangi bila kubana).
    • Yana video ghafi ya mtu akifanya matendo yafuatayo bila kutangaza au kuhimiza matendo kwa njia dhahiri:
      • Kulenga kuaibisha au kutukana mtu au kikundi cha watu.
      • Kutaja mtu mahususi kwa lengo la unyanyasaji au uchokozi.
      • Kukataa kuwa matukio mabaya yalitokea na huyaficha.
      • Kashfa na mashambulizi mabaya ya mtu binafsi.
Maudhui haya hayatachuma mapato ya matangazo

Chuki au unyanyasaji dhidi ya watu au vikundi.

Baadhi ya mifano ya maudhui ambayo yanapatikana pia katika aina hii:

  • Taarifa zinazolenga kushusha hadhi ya kikundi cha watu wanaolindwa au kudokezea au kutaja hali ya kudunishwa, kama vile “watu wote kutoka nchi hii wanaudhi”.
  • Maudhui yasiyo ya elimu yanayoangazia ubaguzi wa rangi au hoja za kushusha hadhi.
  • Kutangaza, kuhimiza au kuruhusu vurugu dhidi ya wengine.
    • Kuchochea ubaguzi dhidi ya vikundi vya watu wanaolindwa, kama vile kusema "unapaswa kuchukia walemavu wote katika nchi hii”.
  • Kuhimiza makundi ya chuki, ishara za chuki au vifaa vya kikundi cha chuki.
  • Kumwaibisha au kumtukana vibaya mtu au kikundi.
  • Kutaja mtu au kikundi kwa lengo la unyanyasaji au matusi.
  • Kukataa au kusifu kuwa majanga yalitokea, kulaumu waathiriwa au walionusurika kuwa vigezo vilivyosababisha majanga.
  • Mashambulizi mabaya na maneno ya kumkashifu mtu binafsi.
  • Kuonyesha itikadi au imani katika njia hasidi kwa kujumlisha au kudunisha.
    • Kuchukulia vibaya watu, vikundi, itikadi au imani, kama vile kusema “ufeministi haufai”.

Ili upate maelezo zaidi kuhusu hoja muhimu zilizotumiwa kwenye mwongozo huu, angalia jedwali letu la ufafanuzi.

Dawa za kujistarehesha na maudhui yanayohusiana na dawa

Maudhui yanayotangaza au yanayoangazia uuzaji, utumiaji au matumizi mabaya ya dawa za kulevya, dawa halali zinazodhibitiwa au vifaa au bidhaa nyingine hatari hayafai matangazo.

Maelezo ya Sera
Mwongozo wa matangazo Maelezo na chaguo za dodoso
Maudhui haya yanaweza kutumika kuchuma mapato ya matangazo

Marejeleo ya elimu, vichekesho au yanayohusiana na muziki kuhusu dawa za kujiburudisha au vifaa vinavyohusiana na dawa za kulevya, ambapo lengo si kutangaza au kusifu matumizi ya dawa za kulevya. Uuzaji wa dawa za kulevya katika maudhui ya michezo ya video. Ripoti za hali halisi au ripoti za waandishi wa habari zinazoonyesha maudhui yanayoiga utumiaji wa dawa za kulevya.

Baadhi ya mifano ya maudhui ambayo yanapatikana katika aina hii:

  • Maudhui ya elimu kuhusu dawa za kulevya au vifaa vya kutengeneza, kutunza na kutumia dawa za kulevya, kama vile athari za kisayansi za matumizi ya dawa au historia ya ulanguzi wa dawa za kulevya.
  • Masimulizi binafsi ya kuachana na uraibu wa dawa za kulevya.
  • Video za muziki zinazoonyesha dawa za kulevya kwa muda mfupi.
  • Maudhui ya michezo inayoonyesha uuzaji wa dawa za kulevya. 
  • Ripoti za hali halisi au ripoti za waandishi wa habari kuhusu ununuzi, utengenezaji, matumizi au usambazaji wa dawa za kulevya kama vile simulizi kuhusu uchunguzi (kusachi na kukamata) wa dawa za kulevya.
  • Maudhui yaliyoigizwa, hali halisi au ripoti ya waandishi wa habari ikiwa ni pamoja na matukio ya michezo ya video yanayoonyesha matumizi ya dawa za kulevya (kama vile kujidunga).
Maudhui haya yanaweza kuchuma mapato machache au yasichume kabisa mapato ya matangazo

Maudhui yasiyo ya elimu na yasiyo ya mafunzo yanayolenga utengenezaji au matumizi yasiyo halali (ikiwa ni pamoja na kujidunga) ya dawa za kulevya, ambapo lengo si kusifu wala kutangaza matumizi ya dawa za kulevya.

Baadhi ya mifano ya maudhui ambayo yanapatikana katika aina hii:

  • Maudhui yaliyoigizwa, ikiwa ni pamoja na muziki na michezo ya video, inayoonyesha matumizi ya dawa za kujiburudisha.
    • Matukio ya kujidunga dawa ili kulewa katika maudhui ya kuigiza.
Maudhui haya hayatachuma mapato ya matangazo

Maudhui yanayotangaza au kuhimiza matumizi ya dawa za kulevya, kama vile kutoa maagizo ya jinsi ya kununua, kuuza au kupata dawa za kulevya au vifaa vya dawa za kulevya ili kuhimiza matumizi kwa ajili ya kujiburudisha.

Baadhi ya mifano ya maudhui ambayo yanapatikana katika aina hii:

  • Kushiriki maoni na maarifa kuhusu dawa za kulevya.
    • Vidokezo au mapendekezo kuhusu utengenezaji au matumizi ya dawa za kulevya, kama vile upanzi wa bangi.
    • Maoni kuhusu maduka, wauzaji, ziara za hospitali, na mambo mengine kuhusu bangi.
    • Kuuza au kununua dawa za kulevya mtandaoni au nje ya mtandao.
      • Kushiriki viungo vya tovuti za kununua dawa za kulevya au anwani halisi ya maeneo ya kununua dawa za kulevya.

Ili upate maelezo zaidi kuhusu hoja muhimu zilizotumiwa kwenye mwongozo huu, angalia jedwali letu la ufafanuzi.

Maudhui yanayohusiana na bunduki

Maudhui yanayolenga uuzaji, uundaji, au matumizi mabaya ya bunduki bandia au halisi hayafai kwa matangazo.

Maelezo ya Sera
Mwongozo wa matangazo Maelezo na chaguo za dodoso
Maudhui haya yanaweza kutumika kuchuma mapato ya matangazo

Bunduki zisizo za kiotomatiki au nusu otomatiki na ambazo hazijarekebishwa zinazoonyeshwa katika mazingira salama kama vile eneo la mazoezi ya kulenga au eneo la wazi ili kutohatarisha maisha ya watazamaji au mali inayomilikiwa na wengine. Kuunganisha na kutenganisha bunduki halisi na bunduki yenye risasi bandia za rangi kwa madhumuni ya kurekebisha au matengenezo. Matumizi sahihi ya bunduki za risasi za plastiki au za mipira.

Baadhi ya mifano ya maudhui ambayo pia yanapatikana katika aina hii:

  • Majadiliano kuhusu sheria za bunduki au tatizo la kudhibiti bunduki.
  • Maoni na maonyesho kuhusu bunduki.
  • Maudhui yanayoangazia zana za kulenga na kuzima sauti.
  • Bunduki bandia wakati hazitumiki kudhuru mtu au mali.

Ufafanuzi:

  • "Mazingira salama" humaanisha maeneo kama vile ya ufyatuaji au maeneo yaliyofungwa ambayo yamejengwa hasa kuwa maeneo ya kufanya mazoezi ya ulengaji shabaha.
  • “Marekebisho” yanarejelea jambo lolote ambalo linaathiri, linaboresha au kubadilisha utendaji wa ndani ya bidhaa; na pia vifyatuaji vya haraka, vifyatuzi na risasi zinazolipuka au zinazosababisha moto au viambatisho vingine kama vile kamera za mwangaza au miale isiyoonekana au zana za kubeba risasi nyingi. 
  • “Bunduki bandia” ni bunduki ambayo kimsingi haitoi risasi. Ufafanuzi huu unajumuisha bunduki ambazo hazitoa risasi halisi. 
     
Maudhui haya yanaweza kuchuma mapato machache au yasichume kabisa mapato ya matangazo

Matumizi ya bunduki nje ya mazingira yanayodhibitiwa; matumizi ya bunduki za risasi za plastiki au za mpira (BB) dhidi ya wengine wasio na zana za kujikinga.

Baadhi ya mifano ya maudhui yanayopatikana pia katika aina hii:

  • Kuonyesha bunduki zikitumika katika mazingira ambayo hayajaandaliwa wala kudhibitiwa (k.m. nje ya nyumba kwenye mtaa au popote ambapo watazamaji au mali inayomilikiwa na wengine itawekwa katika hatari).
Maudhui haya hayatachuma mapato ya matangazo

Maudhui yanayoonyesha utengenezaji au urekebishaji wa bunduki (ikiwa ni pamoja na kuunganisha au kutenganisha), yanayotangaza watengenezaji au wauzaji wa bunduki au yanayowezesha uuzaji wa bunduki, watoto wanaotumia bunduki bila usimamizi wa watu wazima. Maudhui yanayoonyesha bunduki zilizorekebishwa kuwa na vifyatuzi au vifyatuaji vya haraka, jicho la bunduki lenye uwezo wa kuona wakati wa usiku au miale isiyoonekana au kutumia risasi za joto, vilipuzi, au zinazosababisha moto. Maudhui yanayoangazia zana za kubeba risasi nyingi (zenye risasi 30 au zaidi) ambazo zimeunganishwa au hazijaunganishwa kwenye bunduki. Maudhui yanayoangazia bunduki za kiotomatiki au bunduki zilizorekebishwa ili kufyatua zaidi ya risasi moja kwa mfyatuo mmoja.

Baadhi ya mifano ya maudhui ambayo pia yanapatikana katika aina hii:

  • Mwongozo wa jinsi ya kuweka kifyatuzi kwenye bunduki.
  • Mapendekezo ya watengenezaji maarufu wa bunduki au viwanda ambako unaweza kununua bunduki (k.m. “Maduka 15 bora ya kuuza bunduki”).
  • Kuelekeza watumiaji moja kwa moja kwenye tovuti inayoshughulikia uuzaji wa bunduki.
  • Matangazo ya kuuza bunduki au vifaa vyake, ikiwa ni pamoja lakini si tu:
    • Kuuza kwa sehemu inayohusiana na bunduki au kifaa ambacho ni muhimu au kinachoboresha utendaji wa bunduki ikiwa ni pamoja na:
    • Sehemu za bunduki ambazo zimekamilika kwa asilimia 80
    • Risasi
    • Klipu za risasi
    • Vizima sauti ya bunduki
    • Mishipi ya risasi
    • Vifyatuzi
    • Zana za kubadilisha uwezo wa bunduki
    • Ncha za kushikia bunduki
    • Bunduki zenye kamera za kulenga
    • Zana za kulenga
  • Video zinazotangaza maudhui ya maduka ya bunduki.
  • Video zinazotangaza watengenezaji au kuponi za mapunguzo ya bei kwenye maduka ya bunduki.
  • Video zilizo na maagizo kuhusu jinsi ya kutengeneza bunduki (k.m. kuunganisha na kutenganisha sehemu za bunduki au hatua za kurekebisha bunduki), mwongozo au programu au vifaa vya Uchapishaji wa 3D wa bunduki au sehemu zake.
  • Kuunganisha au kutenganisha sehemu za bunduki kwa madhumuni ya kurekebisha.

Ili upate maelezo zaidi kuhusu hoja muhimu zilizotumiwa kwenye mwongozo huu, angalia jedwali letu la ufafanuzi.

Masuala tata

‘Masuala tata’ ni mada ambazo zinaweza kuwaudhi watazamaji, ambazo mara nyingi hutokana na ya misiba ya watu. Sera hii inatumika hata wakati maudhui yanalenga kutoa maoni pekee au hayana picha za kuogofya.

Masuala tata ni pamoja na unyanyasaji wa watoto, unyanyasaji wa kingono kwa watu wazima, dhuluma za kingono, kujijeruhi, kujiua, matatizo ya ulaji, unyanyasaji nyumbani, utoaji mimba na eutanasia.

Maelezo ya Sera
Mwongozo wa matangazo Maelezo na chaguo za dodoso
Maudhui haya yanaweza kutumika kuchuma mapato ya matangazo

Maudhui yanayohusiana na jinsi ya kuzuia masuala tata. Maudhui ambapo masuala tata yanatajwa kwa kifupi katika video na hayajafafanuliwa na si ya kuogofya. Maudhui ambayo hayajafafanuliwa na si ya kuogofya yanayohusiana na unyanyasaji nyumbani, kujijeruhi, unyanyasaji wa kingono kwa watu wazima, utoaji mimba na dhuluma za kingono.

Baadhi ya mifano ya maudhui ambayo yanapatikana katika aina hii: 

  • Mada kuu ya utoaji wa habari isiyo ya kuogofya na isiyo na maelezo kuhusu masuala tata.
  • Maudhui ya kutoa mimba yasiyo ya kuogofya, yakijumuisha akaunti za binafsi, makala au maudhui ya utaratibu wa matibabu.
  • Maudhui yanayoshughulikia ukweli wa kihistoria au kisheria yanayohusiana na kutoa mimba.
  • Kuripoti mada za habari zinazohusiana na maudhui yasiyo ya kuogofya, yasiyo na maelezo yanayohusiana na kujiua au kujijeruhi, unyanyasaji wa kingono kwa watu wazima, unyanyasaji nyumbani, unyanyasaji wa kingono au kifo cha huruma.
  • Maudhui ambayo yameigizwa au ya kisanii kuhusu masuala tata yasiyo ya kuogofya sana.
    • Filamu inayoonyesha mtu akiruka kutoka kwenye daraja, lakini mwili wake kutoonyeshwa.
  • Marejeleo ya jumla kuhusu matatizo ya ulaji yasiyo na viashiria vinavyochochea au vinavyoweza kuigwa.  

Mada na kijipicha: 

  • Marejeleo ya masuala tata yasiyo ya kuogofya.
    • Maandishi au picha ya wembe.

Ufafanuzi: 

  • Marejeleo yanayoonyeshwa kwa muda mfupi si lengo kuu la maudhui (hayaangaziwi) na yanajumuisha marejeleo ya haraka ya mada zinazotajwa kuwa nyeti au za kutatanisha. Kwa mfano, hatua ya kukubali kwa muda mfupi mada nyeti au ya kutatanisha haitachukuliwa kuwa lengo kuu, lakini maudhui yanayoonyeshwa kwa muda mfupi. 
    • Kama vile “Katika video ya wiki ijayo tutajadiliana kuhusu kupungua kwa kiwango cha watu kujiua.”
  • Viashiria vinavyochochea au vinavyoweza kuigwa:   
    • BMI au uzito mdogo sana.
    • Kuonyesha mwili mwembamba au uliodhoofika sana.
    • Uchokozi unaohusiana na uzito au ukubwa wa mwili.
    • Marejeleo ya ulaji wa chakula kingi kwa haraka, kuficha au kuweka akiba ya chakula.
    • Kufanya mazoezi ili kufikia kiwango cha chini mno cha kalori.
    • Kutapika au kutumia vibaya dawa zinazosaidia kitendo cha kwenda choo.
    • Kuangalia hatua alizopiga mtu katika kupoteza uzito.
    • Urejeleaji wa jinsi ya kuficha tabia yoyote kati ya zilizotajwa hapo juu.
Maudhui haya yanaweza kuchuma mapato machache au yasichume kabisa mapato ya matangazo

Maudhui kuhusu masuala tata ambayo hayasababishi hofu yanapotazamwa, japo huenda yanatoa ufafanuzi. Masuala tata yaliyowakilishwa kwa njia ya maigizo, kisanaa, kielimu, hali halisi au kisayansi. Mada kuu ambayo haijafafanuliwa na si ya kuogofya inayohusiana na unyanyasaji wa watoto. Maudhui yasiyo ya kuogofya lakini yamefafanuliwa yanayohusiana na unyanyasaji wa kingono kwa watu wazima, dhuluma za kingono au unyanyasaji nyumbani.

Baadhi ya mifano ya maudhui ambayo yanapatikana katika aina hii: 

  • Maudhui ambayo yanajadili unyanyasaji wa watoto kama mada kuu bila maelezo ya kina au maudhui ya kuogofya.
  • Maudhui ambayo yameigizwa au ya kisanii kuhusu matatizo ya ulaji yaliyo na viashiria vinavyochochea au vinavyoweza kuigwa. 
  • Maudhui ambayo yameigizwa au yaliyohuishwa kuhusu masuala tata yasiyo ya kuogofya sana bila muktadha wa kielimu au kisanii. 
  • Maudhui ambayo yameigizwa au ya kisanii kuhusu masuala tata yasiyo ya kuogofya sana. 
    • Filamu inayoonyesha mtu akikata kifundo cha mkono huku damu ikionyeshwa.
  • Masimulizi ya kupona kutokana na matatizo ya ulaji kama vile safari ya mtu akikabiliana na bulimia.

Mada na kijipicha: 

  • Maudhui ya kuogofya ya masuala tata katika kijipicha yakijumuisha maonyesho halisi, ya kuigiza na ya kisanii. 
Maudhui haya hayatachuma mapato ya matangazo

Maudhui ya kuogofya au ufafanuzi wa kina kuhusu masuala tata kama mada kuu. Urejeleaji dhahiri wa matatizo ya ulaji unaoambatana na muktadha au marejeleo yoyote kati ya yafuatayo: BMI au uzito mdogo sana, kuonyesha mwili mwembamba mno au uliodhoofika, udhalilishaji au uchokozi unaohusiana na uzito au ukubwa wa mwili, marejeleo ya ulaji wa chakula kingi kwa haraka, kuficha au kuweka akiba ya chakula, kufanya mazoezi ili kufikia kiwango cha chini mno cha kalori, kutapika au kutumia vibaya dawa zinazosaidia kitendo cha kwenda choo, kuangalia hatua alizopiga mtu katika kupoteza uzito na urejeleaji wa jinsi ya kuficha tabia yoyote kati ya zilizotajwa hapo juu.

Baadhi ya mifano ya maudhui yanayopatikana pia katika aina hii:

  • Ushahidi wa mhusika unaotoa maelezo kamili na ya kushtua au wasifu wa waathiriwa wakijadili mambo waliyoyapitia yanayohusiana na:
    • Unyanyasaji wa watoto
    • Pedofilia
    • Kitendo cha kujijeruhi
    • Kujiua
    • Unyanyasaji nyumbani
    • Eutanasia
  • Kutangaza au kuhimiza masuala tata katika maudhui, mada au kijipicha kama vile “jinsi ya kujiua na kufa kiheshima."
  • Maonyesho yanayoogofya ya kujijeruhi ambapo makovu, damu au majeraha yanaonekana. 
  • Sauti dhahiri inayojadili suala tata linaloendelea.
  • Marejeleo ya wazi ya matatizo ya ulaji yakiwa na viashiria vinavyochochea au vinavyoweza kuigwa.
  • Maonyesho ya masuala tata ya kuogofya kwa kiasi fulani bila muktadha wa kielimu au kisanii.
    • Video ghafi za mtu akikata kifundo cha mkono huku damu ikionyeshwa.
  • Maonyesho ya masuala tata yaliyohuishwa yanayowasilishwa ili kuibua mihemko.   
    • Yanayoonyesha wahusika wakiwachokoza wengine.

Ufafanuzi:

Lengo kuu au kuangazia inarejelea sehemu fulani ya video, video nzima au mjadala endelevu kuhusu suala fulani tata. Marejeleo ya haraka kuhusu suala tata hayachukuliwi kuwa lengo kuu kuhusu suala hilo. Kwa mfano, hatua ya kukubali kwa muda mfupi mada nyeti au ya kutatanisha kama vile “Katika video ya wiki ijayo tutajadiliana kuhusu kupungua kwa visa vya watu kujiua” haitachukuliwa kuwa lengo kuu, lakini sehemu ya video inayozungumzia mada kama hiyo itachukuliwa kuwa sehemu inayoangaziwa. Si lazima lengo kuu liwe limetamkwa. Iwapo kuna picha au maandishi yanayolenga suala nyeti, yatachukuliwa pia kuwa yanaangazia.

Ili upate maelezo zaidi kuhusu hoja muhimu zilizotumiwa kwenye mwongozo huu, angalia jedwali letu la ufafanuzi.

Matukio nyeti

Tukio nyeti ni tukio au mabadiliko ambayo huweka hatari kubwa katika uwezo wa Google wa kutoa ubora wa juu, maelezo muhimu na ukweli bayana pamoja na kupunguza maudhui yasiyojali au ya unyanyasaji katika vipengele dhahiri na vya uchumaji wa mapato. Wakati wa tukio nyeti, tunaweza kuchukua hatua mbalimbali ili kushughulikia hatari hizi.

Mifano ya matukio nyeti ni kama vile dharura za kiraia, majanga ya kiasili, dharura za afya ya umma, ugaidi na shughuli zinazohusiana, mizozo au matendo ya vurugu ya umma. Sera hii inatumika hata wakati maudhui hayana picha za kuogofya. 

Maelezo ya Sera
Mwongozo wa matangazo Maelezo na chaguo za dodoso
Maudhui haya yanaweza kutumika kuchuma mapato ya matangazo

Mijadala inayohusisha kupoteza maisha au mikasa ambayo si ya unyanyasaji au ya madharau. 

Katika hali fulani, tunaweza kuzuia uchumaji mapato kutokana maudhui yoyote yanayohusiana na tukio nyeti ili kuepuka matumizi mabaya au unyanyasaji wa waathiriwa. Muktadha ni muhimu: kwa mfano, tunaweza kuruhusu maudhui kuchuma mapato ya matangazo ikiwa yanaangazia ripoti za habari zinazoaminika, maudhui ya hali halisi au majadiliano kuhusu tukio nyeti.

Maudhui haya hayatachuma mapato ya matangazo

Watayarishi hawapaswi kuchuma mapato kutokana na maudhui yanayonufaika au kutumia vibaya tukio nyeti kwa nia ya kupata faida.

Mifano (orodha ambayo haijataja vipengele vyote): 

  • Kuonekana kuwa unanufaika kutokana na mkasa mkuu ilhali watumiaji hawapati manufaa yoyote, uuzaji wa bidhaa au huduma ambazo huenda zisifikie viwango na/au mwongozo wa mashirika husika ya usimamizi (kwa mfano, mashirika ya kutoa misaada ya dharura, mamlaka za afya au mashirika ya kimataifa). 
  • Kutumia maneno muhimu yanayohusiana na tukio nyeti ili kujaribu kuongeza watazamaji zaidi.

Ili upate maelezo zaidi kuhusu hoja muhimu zilizotumiwa kwenye mwongozo huu, angalia jedwali letu la ufafanuzi.

Kuwezesha nyendo danganyifu

Maudhui yanayohimiza au kutangaza tabia danganyifu, kama vile kuingia mahali bila ruhusa, kudanganya au udukuzi kwa kutumia kompyuta kwa madhumuni binafsi au kulipwa.

Maelezo ya Sera
Mwongozo wa matangazo Maelezo na chaguo za dodoso
Maudhui haya yanaweza kutumika kuchuma mapato ya matangazo

Marejeleo au kauli za elimu, kuchekesha au zinazohusiana na muziki kuhusu mienendo isiyo ya kweli. Maudhui ambayo hayatangazi tabia danganyifu kama vile ripoti za waandishi wa habari kuhusu makosa madogo dhidi ya kanuni za maadili.

Baadhi ya mifano ya maudhui ambayo yanapatikana katika aina hii:

Kuingia bila ruhusa

  • Kupitia majengo yaliyoachwa au maeneo yaliyotengwa ili kushiriki au kutoa elimu kwa hadhira na maelezo ya kuwa na ruhusa ya kufanya hivyo.
    • Ziara za maeneo yanayodhibitiwa katika eneo la Chernobyl ukiwa na vibali muhimu na ruhusa.
  • Ripoti za kihabari kwenye:
    • Maudhui yanayokiuka kanuni za maadili za maduka ya rejareja au jengo la biashara (kama vile kuendelea kusalia dukani baada ya saa za kazi). 
    • Kujifanya kuwa mfanyakazi wa duka la rejareja bila ruhusa ya mmiliki (kama vile kuvaa sare za dukani na kutoa mwongozo kuhusu bidhaa kwa wateja). 

Udukuzi

  • Majaribio ya kuingia bila idhini (huduma ambayo wadukuzi wa uadilifu huuzia kampuni ili kufanya majaribio ya athari za kiusalama kwenye majengo na maelezo).
  • Zawadi za hitilafu (zawadi zinazotolewa kwa kupata hitilafu za kompyuta katika mifumo au programu).
  • Udukuzi wa kidijitali, mbinu za kuishi, mbinu na vidokezo (k.m. kudukua simu, udanganyifu katika michezo, kubadilisha michezo, huduma za VPN).
  • Ripoti za elimu, hali halisi au za kihabari juu ya utumiaji au kuhimiza matumizi ya programu za udukuzi katika mashindano ya spoti pepe. 

Uhalifu

  • Filamu za hali halisi kuhusu uhalifu.
  • Masimulizi ya binafsi ya watu walioathiriwa na uhalifu.
Maudhui haya hayatachuma mapato ya matangazo

Maudhui yanayonuiwa kufunza watazamaji kuhusu jinsi ya kuingia bila idhini au kufanya mabadiliko ambayo hayajaidhinishwa kwenye mifumo, vifaa au mali kwa njia hasidi. Kuonyesha matendo ambayo yanakiuka kanuni ya maadili ya mali. Kuonyesha bidhaa au huduma zinazosaidia kupotosha au kudanganya, kama vile huduma za kuandika makala ya elimu au mbinu za udukuzi ili kushinda katika mashindano ya spoti pepe

Baadhi ya mifano ya maudhui ambayo yanapatikana katika aina hii:

Kuingia bila ruhusa

  • Kuendeleza au kuhimiza matukio ya kuingia bila ruhusa, kama vile matendo ya usiku ya kuingia katika jengo linalolindwa.
  • Kukiuka kanuni za maadili za maduka ya rejareja au jengo la biashara.
  • Kuiga wafanyakazi wa duka la rejareja ndani ya duka bila idhini ya mmiliki wa duka.
  • Kuonyesha wizi wa kuvunja nyumba bila muktadha wa ziada, k.m. video ya CCTV ya wizi wa kuvunja nyumba.

Udukuzi

  • Kuhimiza au kuruhusu watazamaji kufuatilia kidijitali mtu mwingine au shughuli zake bila idhini yake.
  • Vidokezo kuhusu jinsi ya kuvizia mawasiliano ya simu ya mtu mwingine bila idhini yake.
  • Matumizi au kuhimiza matumizi ya programu za udukuzi katika michezo yenye ushindani kwenye intaneti

Huduma au bidhaa zilizo kinyume cha maadili

  • Huduma za kuwafanyia wanafunzi mazoezi yao ya elimu.
  • Kukwepa upimaji wa dawa za kulevya.
  • Kughushi au kutengeneza pasipoti bandia au hati nyinginezo za utambulisho.

Ili upate maelezo zaidi kuhusu hoja muhimu zilizotumiwa kwenye mwongozo huu, angalia jedwali letu la ufafanuzi.

Maudhui yasiyowafaa watoto na familia

Maudhui “yanayolenga watoto” lazima yafae hadhira ya familia ili yaweze kuchuma mapato kwenye YouTube. Hali hii inamaanisha lazima yafuate kanuni za ubora wa maudhui ya watoto na familia za YouTube na Sera zetu za Mpango.

Maelezo ya Sera

Maudhui yanayohimiza tabia mbaya

Kuhimiza tabia mbaya ambazo zinaweza kuathiri watoto vibaya.

Mwongozo wa matangazo Maelezo na chaguo za dodoso

Maudhui haya yanaweza kutumika kuchuma mapato ya matangazo

Maudhui ambayo yanahimiza tabia njema na hayawadhuru watoto.

Baadhi ya mifano ya maudhui ambayo yanapatikana katika aina hii:

  • Maudhui ya kuelimisha kuhusu tabia isiyofaa
  • Matangazo ya Huduma kwa Umma (PSA) au video kuhusu madhara ya kuchokoza au kudhalilisha watoto
  • Maonyesho kuhusu mazoea bora ya kula
  • Video kuhusu spoti na siha
  • Video za maelekezo ya jinsi ya kujifanyia jambo mwenyewe, mashindano au mizaha yenye kiwango cha chini cha hatari na isiyosababisha madhara yoyote makubwa ya mwili au hisia kwa watoto, kama vile:
    • Video za maelekezo ya jinsi ya kujifanyia jambo mwenyewe, maonyesho au utaratibu wa kufanya mambo, kama vile kuoka au kupika kwa vyombo vinavyotumika kwa njia salama na zinazofaa
    • Mizaha ambapo watoto hawatiwi kiwewe wala kupata madhara ya mwili
 
Maudhui haya hayatachuma mapato ya matangazo

Maudhui yanayoweza kuathiri watoto kwa kuhimiza tabia mbaya kama vile udanganyifu na uchokozi au maudhui yanayoweza kusababisha madhara mabaya ya kimwili au ya kihisia kwa watoto.

Baadhi ya mifano ya maudhui ambayo yanapatikana katika aina hii:

  • Maudhui yanayohimiza au kuendeleza tabia za watoto zisizofaa au maudhui kuhusu masuala ya kijamii yanayowadhuru watoto.
    • Tabia danganyifu, kama vile udanganyifu kwenye mitihani
    • Kuonyesha bunduki halisi au zinazoonekana kama za kweli katika maudhui ya watoto
    • Ulaji wa mfululizo wa vyakula vyenye viwango vya juu vya sukari au mafuta
    • Kuchokoza, kunyanyasa au kudhalilisha watoto
    • Maudhui kuhusu jinsi ya kubadilisha miili ili ionekane miembamba, yenye misuli au kuumbika zaidi, kupunguza au kuongeza kalori, n.k.
    • Video za maelekezo ya jinsi ya kujifanyia jambo mwenyewe au mashindano yanayoonyesha au yanayoweza kusababisha madhara makubwa ya mwili au hisia, kama vile: 
      • Kutumia kemikali zilizopigwa marufuku, vilipuzi, vijiti vya kiberiti kwenye maudhui ya kujitengenezea volkeno, n.k. 
      • Mashindano ya kubugia chakula ambayo huenda yakasababisha kunyongwa 
      • Kuhimiza ulaji wa vitu visivyolika
 

Maudhui ya watu wazima yanayolenga watoto

Mada ambazo mara nyingi zinahusiana na hadhira za vijana au watu wazima kama vile uchi, ngono, vurugu halisi, dawa za kulevya, pombe au lugha chafu katika video, kijipicha au jina la video.

Aina Matangazo machache au bila matangazo
Maudhui yanayofanywa kuonekana kuwa yanafaa watoto na familia, lakini yana mada za watu wazima.
  • Ngono na kudokezea ngono
  • Vurugu, silaha zinazoonekana halisi 
  • Lugha chafu ya wastani au iliyokithiri
  • Dawa za kulevya na pombe 
  • Kuwaonyesha watoto au wahusika maarufu katika vipindi vya watoto kwa njia nyingine zisizofaa kwa watoto na familia

Maudhui ya kuogofya yanayolenga watoto

Maudhui ambayo ni salama kwa watu wazima lakini yanaweza kuwashtua au kuwatisha watoto, kama vile wahusika katika filamu za kuogofya za watu wazima au mada za kutisha sana kama vile utekaji nyara, filamu za kuogofya n.k.

Aina Matangazo machache au bila matangazo
Maudhui yanayofanywa kuonekana kuwa yanafaa watoto na familia, lakini yana maudhui ya kuogofya au kutisha watoto.
  • Wahusika wanaokusudiwa kuwaogofya watoto, kama vile Momo au wahusika katika filamu za kuogofya za watu wazima 
  • Maudhui yanayoonyesha damu iliyoganda au maudhui mengine ya kuogofya ya vurugu
  • Maudhui yasiyoogofya yanayoweza kuwashtua watoto kama vile utekaji nyara, matukio ya kutisha, sirinji zinazotumiwa kama silaha, n.k.

Ili upate maelezo zaidi kuhusu hoja muhimu zilizotumiwa kwenye mwongozo huu, angalia jedwali letu la ufafanuzi.

Maudhui yanayohusiana na tumbaku

Maudhui yanayotangaza tumbaku na bidhaa zinazohusiana na tumbaku hayafai matangazo. Sera hii iko chini ya Matendo hatari katika dodoso la uthibitishaji unaojifanyia kwenye Studio ya YouTube, kwa hivyo hakikisha kuwa unarejelea hilo pia ili upate mwongozo wa kina.

Mifano (orodha ambayo haijataja vipengele vyote)
Aina Matangazo machache au bila matangazo
Kutangaza tumbaku
  • Sigara, biri, kutafuna tumbaku
Kutangaza bidhaa zinazohusiana na tumbaku
  • Kiko, usokotaji makaratasi, vifaa vya kuvuta mihadarati
Kutangaza bidhaa zilizobuniwa kuiga uvutaji wa tumbaku
  • Sigara za mitishamba, sigara za kielektroniki, kuvuta mvuke

Ili upate maelezo zaidi kuhusu hoja muhimu zilizotumiwa kwenye mwongozo huu, angalia jedwali letu la ufafanuzi.

Yanayochochea na kushusha hadhi

Huenda maudhui yanayochochea au kushusha hadhi yasifae matangazo. Sera hii iko chini ya Maudhui ya chuki na yanayodhalilisha katika dodoso la uthibitishaji unaojifanyia kwenye Studio ya YouTube, kwa hivyo hakikisha kuwa unarejelea hilo pia ili upate mwongozo wa kina.

Mifano (orodha ambayo haijataja vipengele vyote)
Aina Matangazo machache au bila matangazo
Maudhui yanayochochea na kushusha hadhi
  • Maudhui yanayolenga kuaibisha au kutukana mtu au kikundi
Maudhui yanayonyanyasa, yanayotisha au yanayochokoza mtu binafsi au kikundi cha watu
  • Maudhui yanayotaja mtu kwa lengo la unyanyasaji au matusi
  • Maudhui yanayosema kuwa janga halikutokea, au waathiriwa au familia zao wanaigiza janga, au wanashiriki katika kuficha tukio hilo
  • Mashambulizi mabaya na maneno ya kumkashifu mtu binafsi

Ili upate maelezo zaidi kuhusu hoja muhimu zilizotumiwa kwenye mwongozo huu, angalia jedwali letu la ufafanuzi.

Ufafanuzi

Tumebuni jedwali la ufafanuzi ili kukusaidia kufahamu vyema hoja zinazotumiwa sana kwenye mwongozo wetu wa maudhui yanayofaa watangazaji.

Ufafanuzi
Sheria na Masharti Ufafanuzi
Muziki Hii inamaanisha video zozote zilizo na muziki, kama vile video rasmi za muziki, video za picha, nyimbo zinazosindikiza, muziki wa utangulizi au utamatishaji au wimbo, miitikio ya video za muziki, kucheza muziki wakati wa mafunzo ya kucheza, muziki uliowekwa au uliopatikana kupitia zana za YouTube au muziki unaochezwa chinichini. Hii haitumiki kwenye mashairi au matumbuizo ya ushairi.
Ya Elimu

“Ya elimu” hurejelea kufahamisha au kufunza kuhusu mada bila kuweka maelezo ya kupotosha hadhira kimakusudi. Maudhui ya elimu huonyesha maoni kwa njia ya kawaida, kama vile katika mjadala wa mbinu salama za ngono. Hoja zifuatazo zinahusiana kimuktadha:

  • “Hali halisi” hurejelea kukumbuka na kuhifadhi matukio ya kihistoria kwa kunukuu hati halisi au kufafanua ukweli, kama vile historia ya Misri ya Kale.
  • “Sayansi” hurejelea kuendeleza hoja kupitia majaribio na nadharia ya kisayansi, kama vile wakati wa kuonyesha data kuhusu saikolojia ya binadamu.
Ya sanaa “Ya sanaa” hurejelea sanaa inayolenga kuonyesha ubunifu wa binadamu kama vile kupaka rangi, michoro, usanifu majengo, sanamu, fasihi, ushairi, muziki, maonyesho na maudhui ya kuigiza. Mfano ni video ya kukariri shairi.
Yaliyoigizwa

“Yaliyoigizwa” hurejelea maudhui yanayotokana na hati, kama vile mazingira ya filamu dhahania, yakiwemo maudhui yaliyohuishwa.

Ya kuogofya, Yanayotisha

"Ya kuogofya” au “yanayotisha” hurejelea ujumuishaji wa maonyesho dhahiri na halisi kama yafuatayo:

  • Majeraha au vidonda vinavyotokana na vitendo vya vurugu, kama vile mapigano mtaani.
  • Matendo ya unyanyasaji dhidi ya wanyama, kama vile kupiga teke.
  • Video za matendo ya ngono, sehemu za siri na ugiligili wa mwili.
Uhalisia

“Uhalisia” hurejelea viwango vitatu:

  • “Uhalisia wa kiwango cha chini”: Kuondoka kabisa katika uhalisia, kama vile paka anayezungumza.
  • “Uhalisia wa kiwango cha kawaida”: Kuondoka kidogo katika uhalisia, kama vile picha zilizokuzwa zaidi zinazoonyesha watu halisi kama vile binadamu au wahusika waliohuishwa katika michezo ya video.
  • “Uhalisia wa kiwango cha juu”: Hali halisi zinazoonyesha wanadamu kama wahusika wakuu, kama vile mapigano mtaani.
Dhahiri, Uwazi

“Dhahiri” au “uwazi” hurejelea kiwango cha uwepo au uonekanaji wa mada inayokiuka sera katika maudhui. Baadhi ya mifano ni pamoja na:

  • Video inayoonyesha utaratibu wa kuavya mimba.
  • Sauti kutoka kwa mtu anayenyanyaswa.
Isiyo dhahiri, Inayokisiwa

“Yasiyo dhahiri” au “yanayokisiwa” hurejelea pendekezo, uwepo au uonekanaji usio wa moja kwa moja wa mada inayokiuka sera. Baadhi ya mifano ni pamoja na:

  • Video inayoonyesha vitanda vikitetemeka na sauti za kingono zinazoashiria vitendo vya ngono.
  • Video inayoonyesha magari yakilipuka ili kuashiria tukio la kifo.
Inayolengwa, Inayoangaziwa

“Inayolengwa” au “lengo kuu” hurejelea wakati sehemu au video kamili inahusu mada fulani, na kuna marejeleo na ulengaji unaorudiwa wa mada. Marejeleo ya haraka kwenye mojawapo ya mada zilizoorodheshwa kuwa nyeti au za kutatanisha si sababu ya kuainisha kuwa 'Hamna Matangazo'. Kwa mfano, hatua ya kukubali kwa muda mfupi mada nyeti au ya kutatanisha (k.m. “Katika video ya wiki ijayo tutajadiliana kuhusu kupungua kwa visa vya watu kujiua.”) haitachukuliwa kuwa lengo kuu, lakini sehemu ya video inayozungumzia kuhusu mada kama hiyo itachukuliwa kuwa lengo kuu. Si lazima lengo liwe sauti. Iwapo kuna picha au maandishi yanayolenga suala nyeti, yatachukuliwa pia kuwa yanaangazia. Baadhi ya mifano ni pamoja na:

  • Video inayolenga jinsi ya kujijeruhi.
  • Maudhui yanayolenga tu kutumia lugha chafu zaidi bila muktadha au sababu nyingine.
Kwa muda mfupi

"Kwa muda mfupi" hurejelea matukio ambayo si lengo la maudhui (hayaangaziwi) na yanajumuisha marejeleo ya muda mfupi ya mada zinazotajwa kuwa nyeti au za kutatanisha. Kwa mfano, hatua ya kukubali kutaja kwa kifupi mada nyeti au ya kutatanisha (k.m. “Katika video ya wiki ijayo tutajadiliana kuhusu kupungua kwa visa vya watu kujiua.”) hakutachukuliwa kuwa lengo kuu, lakini itaonyeshwa kwa muda mfupi.

Maudhui yanayoshtua

Hurejelea njia inayokusudiwa kuzua shauku au hamu kuu, hasa kupitia kujumuishwa kwa maelezo yaliyotiwa chumvi, ya kuogofya au nyeti.

  • "Kula kwa njia ya kushtua" kama vile kula mnyama au sehemu za wanyama ambao wako hai au bado wanaonekana wakisonga.
  • "Kula au kuandaa kwa njia ya kushtua" ambapo maandalizi au ulaji huwa wa maigizo, kama vile sehemu ya maonyesho ya "mukbang" au ASMR.
  • "Maonyesho ya kushtua ya masuala tata" ambapo mada nyeti, kama vile uchokozi, huwa mada kuu ya burudani, hasa kupitia mtagusano mbaya wa wahusika.

Lazima video zote zinazopakiwa kwenye YouTube zitii Sheria na Masharti na Mwongozo wa Jumuiya ya YouTube. Ili uweze kuchuma mapato ukitumia matangazo, utahitaji kufuata Sera za uchumaji wa mapato kwenye YouTube na Sera za Mpango.

Huenda tukahifadhi haki ya kuzima matangazo kwenye chaneli yako nzima katika hali ambapo maudhui yako mengi hayafai watangazaji wowote au pale ambapo kuna matokeo ya ukiukaji mkubwa unaojirudia (k.m. upakiaji wa maudhui ambayo ni ya uchochezi, ya kushusha hadhi au ya chuki).

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
5635614493533618147
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false