Kukashifu

Sheria za kashfa zinatofautiana kutoka nchi hadi nchi lakini kwa kawaida zinahusu maudhui yanayodhuru sifa ya mtu mwingine au biashara. Ingawa ufafanuzi wa kashfa unatofautiana kutoka nchi hadi nchi, kwa ujumla, kashfa ni tamko lolote lisilo la kweli linalodhuru sifa ya mtu au kusababisha mtu kutengwa au watu kumkwepa.

Tunazingatia vigezo vya kisheria vya eneo husika katika mchakato wetu wa kuzuia kashfa na katika baadhi ya matukio, tunahitaji amri ya mahakama. Ili tuweze kushughulikia ombi la kuzuia kashfa, dai linahitaji kuwa mahususi na kuwa na vielelezo vya kutosha. Kwa mfano, linahitaji kueleza ni kwa nini unaamini matamko si ya kweli na jinsi yanavyoharibu sifa yako.

Katika matukio mengine, waliopakia huondoa kwa hiari yao maudhui hatari. Kwa sababu mchakato wa kupata amri ya mahakama unaweza kuwa na gharama kubwa na kupoteza muda, tunahimiza watumiaji wawasiliane moja kwa moja na waliopakia maudhui husika.

Ikiwa umeshindwa kuwasiliana na aliyepakia, zingatia iwapo video inatimiza vigezo vya kuondolewa chini ya sera yetu ya faragha au unyanyasaji.

Ikiwa umejaribu kuwasiliana na aliyepakia, na unaamini dai la kashfa linafaa zaidi kuliko malalamiko ya faragha au unyanyasaji, tafadhali chagua nchi ambako dai linafanyika kwenye menyu kunjuzi hapa chini kisha ufuate maagizo. 

Kwa sababu hatuko katika nafasi ya kuamua kuhusu ukweli wa madai ya machapisho, hatuondoi machapisho ya video kutokana na madai ya kashfa. Kwa mujibu wa Kifungu cha 230(c) cha Sheria ya Ustahifu wa Mawasiliano, tunapendekeza ufuatilie madai yoyote unayoweza kuwa nayo moja kwa moja dhidi ya mtu aliyechapisha maudhui hayo. Iwapo utachagua kuchukua hatua za kisheria dhidi ya mtayarishi wa maudhui, kumbuka kuwa tutakuwa tayari kutii amri inayotaka mtayarishi wa maudhui aondoe chapisho husika.

Iwapo kuna amri ya mahakama inayohusu maudhui yanayochapishwa kwenye www.youtube.com unaweza kuisambaza kupitia barua kwenye anwani ifuatayo: YouTube, Inc., Attn Legal Support, 901 Cherry Ave., Second Floor, San Bruno, CA 94066.

Au, unaweza kuwasiliana na aliyeipakia.

Iwapo una swali linalohusiana na hakimiliki, tafadhali tembelea Kituo chetu cha Hakimiliki. Iwapo una swali la ziada linalohusiana na ukiukaji wa Sera za YouTube, tafadhali tembelea Kituo chetu cha Kuripoti.

 

Usipopata nchi yako kwenye menyu kunjuzi hapo juu

YouTube.com inasimamiwa na sheria ya Marekani.

Kwa sababu hatuko katika nafasi ya kuamua kuhusu ukweli wa madai ya machapisho, hatuondoi machapisho ya video kutokana na madai ya kukashifiwa. Kwa mujibu wa Kifungu cha 230(c) cha Sheria ya Ustahifu wa Mawasiliano, tunapendekeza ufuatilie madai yoyote unayoweza kuwa nayo moja kwa moja dhidi ya mtu aliyechapisha maudhui hayo. Iwapo utachagua kuchukua hatua za kisheria dhidi ya mtayarishi wa maudhui, kumbuka kuwa tunaweza kuwa tayari kutii amri yoyote inayotaka mtayarishi wa maudhui aondoe chapisho husika.

Iwapo kuna amri ya mahakama inayohusu maudhui yaliyochapishwa kwenye www.youtube.com unaweza kuituma kwa barua kwenye anwani ifuatayo: YouTube, Inc., Attn Legal Support, 901 Cherry Ave., Second Floor, San Bruno, CA 94066.

Au, unaweza kuwasiliana na aliyeyapakia.

Iwapo una swali linalohusiana na hakimiliki, tafadhali tembelea Kituo chetu cha Hakimiliki. Iwapo una swali la ziada linalohusiana na ukiukaji wa Sera za YouTube, tafadhali tembelea Kituo chetu cha Kuripoti Video Zisizofaa.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
2358991531463480539
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false