Kuweka kadi za maelezo kwenye video

Unaweza kutumia kadi za maelezo kufanya video zako ziwashirikishe zaidi watazamaji. Kadi za maelezo zinaweza kuangazia video, orodha ya kucheza, kituo au kiungo. Kadi hazipatikani kwenye video zilizobainishwa kuwa zinalenga watoto.

Kuweka kadi kwenye video

Ili uweke kadi kwenye video, fuata hatua zilizo hapa chini.

  1. Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
  2. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Maudhui.
  3. Bofya video ambayo ungependa kuhariri.
  4. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Kihariri.
  5. Chagua Kadi za maelezo  kisha uchague kadi ambayo ungependa kuweka. Kumbuka: Unaweza kuweka hadi kadi 5 kwenye video moja.
    • Video: Kadi hii ya maelezo hukuwezesha kuunganisha video ya YouTube ya umma ya kuwashirikisha watazamaji wako. 
    • Orodha ya kucheza: Kadi hii ya maelezo hukuwezesha kuunganisha orodha ya kucheza ya YouTube iliyo wazi kwa umma ili itazamwe na watazamaji wako.
    • Chaneli: Kadi hii ya maelezo hukuwezesha kuunganisha chaneli ya YouTube ili kuwashirikisha watazamaji wako. Kwa mfano, unaweza kutumia kadi ya maelezo kushukuru kituo kilichokusaidia na video yako au kuwapendekezea watazamaji kituo kingine.
    • Kiungo: Ikiwa umejiunga kwenye Mpango wa Washirika wa YouTube, kadi hii ya maelezo hukuwezesha kuunganisha kwenye tovuti ya nje ili ushiriki na hadhira yako. Unaweza pia kuweka skrini za mwisho kwenye video zako. Kumbuka: Hakikisha kuwa tovuti yako ya nje uliyounganisha inatii sera zetu, ikiwa ni pamoja na Mwongozo wa Jumuiya na Sheria na Masharti yetu. Ukiukaji unaweza kusababisha kuondolewa kwa kadi au kiungo, maonyo au kufungwa kwa Akaunti yako ya Google.
  6. Badilisha wakati wa kuanza wa kadi chini ya video.
  7. Weka ujumbe na maandishi ya kishawishi yasiyo ya lazima kuhusu video. Kumbuka: Ni sharti uweke ujumbe na maandishi ya kishawishi kwenye kadi za kituo.
  8. Bofya Hifadhi.

Jinsi watazamaji wanavyoweza kutumia kadi

Kadi zimebuniwa ili kuboresha video na kuimarisha hali ya utumiaji ya watazamaji kwa maelezo yanayofaa. Kadri mfumo unavyobadilika, tunapanga kuuborehsa ili uonyeshe vishawishi na kadi zinazofaa zaidi kulingana na utendaji, tabia ya watazamaji na kifaa wanachotumia.

Jinsi watazamaji wanavyopata kadi

  • Mtazamaji anapotazama video yako, ataona kishawishi kwa wakati uliobainisha.
  • Wakati kishawishi hakionyeshwi, watazamaji wanaweza kuelea juu ya kichezaji kisha wabofye aikoni ya kadi . Kwenye vifaa vya mkononi, watazamaji wanaweza kuona aikoni ya kadi wakati wowote vidhibiti vya kichezaji vinapoonyeshwa.
  • Wanapobofya kishawishi au aikoni, wanaweza kuvinjari kadi kwenye video.

Jinsi kadi zinavyoweza kubadilisha maudhui yako

Jinsi kadi zinavyoonyeshwa kwenye video

Kadi huonyeshwa chini ya maelezo ya video. Ikiwa kuna kadi nyingi kwenye video, watazamaji wanaweza kuziptia wakati video inacheza.

Ni nani anayeweza kuona kadi?

Kipengele hiki kinapatikana kwa watazamaji kwenye kompyuta. Kipengele hiki hakipatikani kwenye Adobe Flash.

Watazamaji hawawezi kuona kadi kwenye video zilizobainishwa kuwa zinalenga watoto.
 

 

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
10857151909523197669
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false