Unaweza kuondoa maudhui yanayopendekezwa ambayo hayakuvutii kwenye Ukurasa wako wa Kwanza. Kuondoa video hizi kunaweza kuboresha maudhui unayopendekezewa ili uone video zinazokufaa zaidi.
Kwenye televisheni yako inayoweza kuunganisha kwenye intaneti au katika kifaa chako cha michezo ya video
Kuondoa maudhui yanayopendekezwa kwenye ukurasa wa kwanza
Unaweza kuondoa video zinazopendekezwa kwa kuchagua “Hainivutii” kwenye ukurasa wako wa kwanza, au katika Ukurasa wa Kwanza na Ukurasa wa Tazama Video Inayofuata kwenye kifaa cha mkononi:
- Bonyeza na ushikilie kitufe cha kuchagua kwenye kidhibiti chako cha mbali.
- Chagua Hainivutii.
- Chagua 'Sababu ya kuondoa' ili ueleze ni kwa nini ungependa kuondoa video. Unaweza kuchagua Tayari nimetazama video, Sipendi video, au Usipendekeze kituo ili utusaidie kukupendekezea video zinazokufaa zaidi.
Futa maoni yako ya “Hainivutii" na “Usipendekeze kituo”
Maoni yako ya “Hainivutii” na “Usipendekeze kituo” yanaweza kutumika kuweka mapendeleo kwenye mapendekezo yako. Ili ufute maoni yote uliyotoa ya “Hainivutii” na “Usipendekeze kituo”, tafadhali fuata maagizo hapa chini ukitumia kompyuta, Android, au iPhone au iPad yako.
Mapendekezo kutokana na Shughuli zako kwenye Google
YouTube hutumia data inayotokana na Shughuli za Akaunti yako ya Google kukupendekezea video.
Unaweza kuangalia na kudhibiti shughuli zako katika myactivity.google.com. Pata maelezo zaidi kuhusu kudhibiti shughuli za Akaunti yako ya Google.
Maudhui yafuatayo yanayopendekezwa yanaweza kuondolewa kwenye ukurasa wa kwanza kwenye kompyuta yako:
- Video
- Vituo
- Sehemu
- Orodha za kucheza
Maudhui yanayopendekezwa yafuatayo yanaweza kuondolewa kwenye ukurasa wa kwanza kwenye kompyuta yako:
- Video
- Vituo
- Sehemu
- Orodha za kucheza
Unaweza pia kuondoa video zinazopendekezwa kwenye ukurasa wa Tazama Video Inayofuata kwenye kompyuta yako.
Ondoa video inayopendekezwa
-
Bofya Zaidi
karibu na jina.
-
Bofya Hainivutii
ili uondoe video kwenye mipasho yako.
-
Chagua Tueleze ni kwa nini ili ushiriki ni kwa nini ungependa kuondoa video. Unaweza kuchagua Nimeshatazama video au Sipendi video ili ufanye mapendekezo yako yakufae zaidi.
Ondoa kituo kinachopendekezwa
- Bofya Zaidi
karibu na jina.
- Chagua Usipendekeze kituo
.
Futa maoni ya "Hainivutii"
Uteuzi wako wa “Hainivutii” unaweza kutumika kuweka mapendeleo katika maudhui unayopendekezewa. Ili ufute maoni yako yote ya “Hainivutii”:
-
Tembelea ukurasa wa Shughuli Zangu. Huenda ukahitaji kuingia katika akaunti.
-
Kwenye upande wa kushoto, nenda kwenye Shughuli nyingine za Google.
-
Chini ya maoni ya "'Hainivutii' kwenye YouTube," bofya Futa.
Pata maelezo zaidi kuhusu historia ya video ulizotazama na historia ya mambo uliyotafuta.