Kushirikiana kwenye orodha za kucheza

Unaweza kuwaruhusu marafiki zako waongeze video kwenye orodha yako ya kucheza. Unapowasha kipengele hiki, mtu yeyote unayeshiriki naye orodha ya kucheza anaweza kuongeza video kwenye orodha hiyo ya kucheza.

Kabla ya kuanza, tunga orodha ya kucheza. Iwapo unahitaji usaidizi, fuata hatua hizi ili utunge orodha ya kucheza.

Kuweka washirika kwenye orodha ya video

Fuatilia chaneli ya Watazamaji ya YouTube ili upate habari, taarifa na vidokezo vipya.
  1. Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
  2. Kwenye menyu ya Kushoto, chagua Maudhui.
  3. Bofya kichupo cha Orodha za kucheza.
  4. Karibu na orodha ya kucheza ambako ungependa kuongeza washirika, bofya Badilisha .
  5. Chini ya jina la orodha ya kucheza, bofya Zaidi .
  6. Bofya Shirikiana .
  7. Bofya kitelezi kilicho karibu na “Washirika wanaweza kuweka video kwenye orodha hii ya kucheza".
  8. Washa “Ruhusu washirika wapya”.
  9. Nakili kiungo cha orodha ya kucheza na ukishiriki na watu ambao ungependa kushirikiana nao.

Wakati orodha ya kucheza imebadilishwa au washirika wapya wamejiunga, mmiliki wa orodha ya kucheza atapokea arifa.

Kuweka video kwenye orodha ya kucheza

Baada ya kualikwa uongeze video kwenye orodha ya kucheza, unaweza kuongeza au kuondoa video ambazo uliweka awali.

Kuongeza video
  1. Ili uende kwenye ukurasa wa orodha ya kucheza, tumia kiungo ulichopata kutoka kwa mmiliki wa orodha ya kucheza.
  2. Fuata maagizo yaliyo kwenye skrini ili uthibitishe kuwa ungependa kuwa mchangiaji. Orodha ya kucheza itahifadhiwa kiotomatiki.
  3. Ili uweke video kutoka kwenye kompyuta au kifaa chako cha mkononi, nenda kwenye video ambayo ungependa kuweka kisha uchague Hifadhi kwenye video hiyo.

Baada ya kuweka video, jina lako litaonekana karibu na video hiyo katika orodha ya kucheza. Washirika wote watapokea arifa video mpya zitakapoongezwa kwenye orodha ya kucheza.

Kuondoa video
  1. Ili uende kwenye ukurasa wa orodha ya kucheza, tumia kiungo ulichopata kutoka kwa mmiliki wa orodha ya kucheza.
  2. Chagua Zaidi ''.
  3. Chagua Ondoa kwenye orodha ya kucheza .

Kumbuka: Unaweza tu kuondoa video ulizoweka kwenye orodha ya kucheza (wala si video zilizoongezwa na washirika wengine).

Kudhibiti michango ya video

Kuacha kukubali michango ya video kwenye orodha ya kucheza

Unaweza kuzima michango kwenye orodha za kucheza ambazo umeshiriki wakati wowote:

  1. Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
  2. Kwenye menyu ya Kushoto, chagua Maudhui.
  3. Bofya kichupo cha Orodha za kucheza.
  4. Karibu na orodha ya kucheza ambayo ungependa kuisasisha, bofya Badilisha .
  5. Chini ya jina la orodha ya kucheza, bofya Zaidi .
  6. Bofya Shirikiana .
  7. Zima "Ruhusu washirika wapya".
  8. Bofya kitelezi kilicho karibu na “Washirika wanaweza kuongeza video kwenye orodha hii ya kucheza."

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
6583838997350447957
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false