Vifaa usivyoweza kutumia kutazama: Miundo ya vifaa visivyotumia programu za YouTube

Programu ya sasa ya YouTube haifanyi kazi kwenye miundo fulani ya vifaa, na matoleo ya zamani ya programu ya YouTube hayatafanya kazi.

Televisheni zinazoweza kuunganisha kwenye intaneti na vifaa vya michezo ya video

Unaweza kuangalia ikiwa televisheni zinazoweza kuunganisha kwenye intaneti na vifaa vya michezo ya video vinaoana na programu ya YouTube hapa.

Vifaa vya mkononi

Sasisha Matoleo ya Programu ya Android

Ukipata ujumbe ufuatao, inamaanisha kuwa unatumia toleo ambalo halitumiki tena. Utahitaji kusasisha ili ufikie programu ya YouTube. Ili usasishe upate toleo jipya la programu ya YouTube ya Android, tembelea Duka la Google Play.

Ikiwa ungependa kuendelea kutumia YouTube bila kusasisha programu, tembelea m.youtube.com kwenye kivinjari cha kifaa chako cha mkononi.

Matatizo ya kusasisha

Ikiwa huwezi kusasisha programu yako, toleo lako la mfumo wa uendeshaji wa Android haliwezi tena kutumia toleo jipya la programu ya YouTube. Ili upate toleo jipya la programu ya YouTube, sasisha ili upate toleo jipya la mfumo wa uendeshaji wa Android.

Unawea kuendelea kutumia programu ya YouTube bila kusasisha mfumo wako wa uendeshaji, lakini hatimaye, matoleo ya zamani ya programu ya YouTube hayataweza kutumika. Unaweza kutembelea m.youtube.com katika kivinjari cha kifaa chako cha mkononi wakati wote ili utazame YouTube.

YouTube haipaitani tena kwenye baadhi ya vifaa

Ukiona ujumbe huu unapofungua YouTube kwenye televisheni au kifaa cha michezo ya video, programu ya YouTube haitafanya kazi tena kwenye kifaa chako.

Ujumbe: "YouTube haipatikani kwenye kifaa hiki kwa sababu hakitimizi mahitaji ya hivi karibuni."

Huwa tunasasisha mara kwa mara viwango vyetu vya usalama ili kutunza usalama wa watumiaji. Hii inamaanisha kuwa tunazima huduma zetu kwenye vifaa ambavyo haviendani tena na viwango hivyo. Ikiwa televisheni yako ina kivinjari, inawezekana kuendelea kutumia YouTube kupitia youtube.com

Wakati mwingine, unaweza kusasisha programu dhibiti ya kifaa chako ili urejeshe uwezo wa kufikia programu ya YouTube. Ikiwa huna uhakika wa jinsi ya kusasisha programu dhibiti yako, wasiliana na mtengenezaji wa kifaa chako. 

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
16940852847092094919
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false