Programu ya sasa ya YouTube haifanyi kazi kwenye miundo fulani ya vifaa, na matoleo ya zamani ya programu ya YouTube hayatafanya kazi.
Televisheni zinazoweza kuunganisha kwenye intaneti na vifaa vya michezo ya video
Unaweza kuangalia ikiwa televisheni zinazoweza kuunganisha kwenye intaneti na vifaa vya michezo ya video vinaoana na programu ya YouTube hapa.
Vifaa vya mkononi
Sasisha Matoleo ya Programu ya Android
Ukipata ujumbe ufuatao, inamaanisha kuwa unatumia toleo ambalo halitumiki tena. Utahitaji kusasisha ili ufikie programu ya YouTube. Ili usasishe upate toleo jipya la programu ya YouTube ya Android, tembelea Duka la Google Play.
Ikiwa ungependa kuendelea kutumia YouTube bila kusasisha programu, tembelea m.youtube.com kwenye kivinjari cha kifaa chako cha mkononi.
Matatizo ya kusasisha
Ikiwa huwezi kusasisha programu yako, toleo lako la mfumo wa uendeshaji wa Android haliwezi tena kutumia toleo jipya la programu ya YouTube. Ili upate toleo jipya la programu ya YouTube, sasisha ili upate toleo jipya la mfumo wa uendeshaji wa Android.
Unawea kuendelea kutumia programu ya YouTube bila kusasisha mfumo wako wa uendeshaji, lakini hatimaye, matoleo ya zamani ya programu ya YouTube hayataweza kutumika. Unaweza kutembelea m.youtube.com katika kivinjari cha kifaa chako cha mkononi wakati wote ili utazame YouTube.
YouTube haipaitani tena kwenye baadhi ya vifaa
Ujumbe: "YouTube haipatikani kwenye kifaa hiki kwa sababu hakitimizi mahitaji ya hivi karibuni."
Huwa tunasasisha mara kwa mara viwango vyetu vya usalama ili kutunza usalama wa watumiaji. Hii inamaanisha kuwa tunazima huduma zetu kwenye vifaa ambavyo haviendani tena na viwango hivyo. Ikiwa televisheni yako ina kivinjari, inawezekana kuendelea kutumia YouTube kupitia youtube.com
Wakati mwingine, unaweza kusasisha programu dhibiti ya kifaa chako ili urejeshe uwezo wa kufikia programu ya YouTube. Ikiwa huna uhakika wa jinsi ya kusasisha programu dhibiti yako, wasiliana na mtengenezaji wa kifaa chako.