Pata data kuhusu vipengee vyako
Takwimu za vipengee hukuonyesha jinsi vipengee vyako vinavyofanya kazi. Unaweza kuona ni vipengee gani vinapata umaarufu zaidi, kulinganisha utendaji wa vipengee vinginevyo na kugundua video bora zinazoongoza katika utendaji wa vipengee. Data hii inapatikana kila siku, lakini inaweza kuchelewa kwa siku kadhaa. Ili kutazama data kwenye vipengee vyako:
- Ingia katika akaunti ya Kidhibiti Maudhui cha Studio.
- Kwenye Menyu ya kushoto, chagua Takwimu .
- Kwenye kichupo cha Muhtasari, nenda kwenye sehemu ya Video maarufu. Sehemu hii huonyesha video, vituo na vipengee ambavyo data yake imebadilika kwa kiasi kikubwa ndani ya siku 7 zilizopita.
- Bofya kichupo cha Vipengee na uchague kitendo:
- Bofya kipengee ili upate data ya kipengee husika.
- Elea juu ya kipengee na ubofye aikoni ya kulinganisha ili ulinganishe utendaji wa kipengee kwa siku 7 zilizopita.
- Ripoti za utendaji huhesabu idadi za watazamaji zinazodaiwa pekee
- Takwimu za YouTube huhesabu idadi za utazamaji zinazodaiwa au zisizodaiwa zilizopakiwa na mshirika
Tazama takwimu za mapato yako
Kwenye ukurasa wa Takwimu , unaweza kubofya kichupo cha Mapato ili kuona data ya makadirio ya mapato. Kumbuka kuwa:
- Makadirio ya data ya mapato kwenye Takwimu za YouTube husasishwa kila siku.
- Data katika sehemu ya Takwimu za YouTube huchelewa kwa takribani siku 2 kwa data ya makadirio ya mapato.
- Data ya mapato yanayokadiriwa kwenye Takwimu za YouTube haionyeshi marekebisho batili ya shughuli katika muda halisi. Data ya mwisho ya mapato iliyoripotiwa kwenye ripoti za fedha zinazoweza kupakuliwa huenda zikatofautiana na data ya Takwimu za YouTube.
Tumia hali ya kina
Takwimu za YouTube kwenye hali ya kina inakuruhusu uone data mahususi zaidi kuhusu vituo, vipengee na hadhira yako. Unaweza kulinganisha vipimo vya utendaji wa maudhui na kuhamisha data yako. Ili utumie hali ya kina:
- Ingia katika akaunti ya Kidhibiti Maudhui cha Studio.
- Kwenye Menyu ya kushoto, chagua Takwimu .
- Kwenye kona ya upande wa juu kulia, bofya HALI YA KINA.
- Kwenye ukurasa huu unaweza kuchukua hatua kadhaa, ambazo zimeorodheshwa hapa. Kwa watumiaji wa Kidhibiti Maudhui, vitendo vya ziada vinajumuisha:
- Bofya kichupo cha Vituo ili utazame data kwenye vituo binafsi.
- Bofya kichupo cha Vipengee ili utazame data kwenye vipengee binafsi.
- Bofya kichupo cha Zaidi ili utazame data ya Umiliki wa kituo au Hali ya dai.
Kumbuka kuwa, kwenye ukurasa wa hali yoyote ya kina, unaweza kubofya aikoni ya kupakua ili kuhamisha data. Pata maelezo zaidi kuhusu kutumia hali ya kina kwenye Takwimu za YouTube.
Panga data kwa kutumia vikundi vya Takwimu
Vikundi ni mikusanyiko ya video, vituo au vipengee vilivyowekewa mapendeleo. Vikundi vinakuruhusu kupanga maudhui yanayofanana pamoja ili uone data yote katika sehemu moja, hali ambayo itakuwezesha kufuatilia utendaji kwa njia rahisi.
Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kuanzisha na kusimamia vikundi vya takwimu.