Idadi ya wanaofuatilia chaneli yako huonyesha idadi ya watazamaji wanaofuatilia chaneli yako ya YouTube. Unaweza kuangalia idadi ya wanaofuatilia kituo chako katika muda halisi na uone ukuaji wa kituo chako katika kipindi fulani kwenye Takwimu za YouTube. Utapata barua pepe na upate uhuishaji wa kukupongeza ndani ya Studio ya YouTube unapotimiza lengo.
Kupata idadi ya wanaofuatilia chaneli yako
- Ingia katika Studio ya YouTube.
- Katika Menyu ya kushoto, chagua Takwimu .
- Kwenye kichupo cha Muhtasari, tafuta kadi ya Muda halisi.
- Bofya ANGALIA IDADI HALISI ili uone idadi ya wanaofuatilia chaneli yako kadiri muda unavyosonga.
Kuelewa idadi ya wanaofuatilia chaneli yako kwenye YouTube
Hadhira yako inaweza kuona toleo lililofupishwa la idadi ya wanaofuatilia kituo chako. Idadi hii ya wanaofuatilia chaneli yako imefupishwa kulingana na idadi ya watu wanaofuatilia chaneli yako.
Ikiwa una | Masasisho ya idadi ya wanaofuatilia chaneli yako kwa kila: |
Chini ya watu 1,000 wanaofuatilia | Mtu 1 mpya anayefuatilia |
Watu 1,000–9,999 wanaofuatilia | Watu 10 wapya wanaofuatilia |
Watu 10,000–99,999 wanaofuatilia | Watu 100 wapya wanaofuatilia |
Watu 100,000–999,999 wanaofuatilia | Watu 1,000 wanaofuatilia |
Watu 1,000,000–9,999,999 wanaofuatilia | Watu 10,000 wapya wanaofuatilia |
Watu 10,000,000–99,999,999 wanaofuatilia | Watu 100,000 wapya wanaofuatilia |
Wapya 100,000,000–999,999,999 wanaofuatilia | Watu 1,000,000 wapya wanaofuatilia |
Ili uelewe jinsi idadi ya wanaofuatilia chaneli yako itakavyoonyeshwa, tumia jedwali lililo hapo chini.
Kwa mfano, ikiwa una | Idadi ya wanaofuatilia chaneli yako ni: | Idadi ijayo ya wanaofuatilia itakuwa: |
Watu 123 wanaofuatilia | 123 | 124 |
Watu 1,234 wanaofuatilia | 1.23 Elfu | 1.24 Elfu |
Watu 12,345 wanaofuatilia | 12.3 Elfu | 12.4 Elfu |
Watu 123,456 wanaofuatilia | 123 Elfu | 124 Elfu |
Watu 1,234,567 wanaofuatilia | Milioni 1.23 | Milioni 1.24 |
Watu 12,345,678 wanaofuatilia | Milioni 12.3 | Milioni 12.4 |
Watu 123,456,789 wanaofuatilia | Milioni 123 | Milioni 124 |
Kuondoa akaunti zilizofungwa na watumiaji taka
- Akaunti zilizofungwa: Akaunti zilizofungwa na mtayarishi au zilizosimamishwa na YouTube kutokana na ukiukaji wa sera.
- Watumiaji bandia: Watumiaji wanaopatikana kupitia mbinu bandia, kama vile kununua wanaofuatilia kupitia huduma ya wengine.
Mara kwa mara tunathibitisha uhalali wa akaunti na vitendo kwenye chaneli yako ya YouTube. Huenda pia tukafanya marekebisho ya vipimo vya tovuti katika Takwimu za YouTube ili kurekebisha matatizo ya uthabiti katika vyanzo tofauti. Michakato hii huhakikisha kuwa vipimo vya tovuti yetu havina taka, matumizi mabaya na akaunti zilizofungwa ili kufanya YouTube iwe sehemu ya haki kwa kila mtu.
Ni muhimu idadi ya wanaofuatilia iendelee kuwa sahihi ili kuhakikisha kuwa unakuza hadhira yako kwa njia halisi. Watumiaji bandia na akaunti zilizofungwa hazitahesabiwa kwenye jumla ya idadi yako ya wanaofuatilia. Hazitaonekana pia kwenye orodha yako ya wanaofuatilia na hazitaathiri utazamaji au muda wa kutazama.