Kuweka chaneli chaguomsingi kwenye akaunti

Ikiwa Akaunti yako ya Google inajumuisha zaidi ya chaneli moja ya YouTube, unaweza kuona dirisha ibukizi ili uchague chaneli unapoingia katika akaunti:

Channel switcher

Iwapo ungependa kuingia moja kwa moja katika chaneli moja kila wakati, unaweza kuweka chaneli chaguomsingi kwenye dirisha ibukizi. Teua tu chaneli unayopenda kuangalia na uchague Usiniulize tena. Bado unaweza kubadilisha kwenda chaneli nyingine kwenye akaunti kwa urahisi.

Kumbuka: Chaneli chaguomsingi pia itatumika katika zana na programu za washirika wengine (kwa mfano: programu ya kuhariri video) ambazo haziruhusu ubadilishaji wa chaneli. Unapoweka kitambulisho cha Akaunti yako ya Google katika zana hizi, chaneli chaguomsingi itatumika kiotomatiki.

Kubadilisha chaneli chaguomsingi

Ili ubadilishe chaneli chaguomsingi kwenye Akaunti yako ya Google:

  1. Kwenye kompyuta, ingia katika akaunti ya YouTube ukitumia Akaunti yako ya Google.
  2. Badilisha utumie chaneli ambayo ungependa kuiweka kuwa chaneli chaguomsingi.
  3. Nenda kwenye mipangilio ya akaunti ya kina.
  4. Katika sehemu ya chini ya "Chaneli Chaguomsingi" chagua "Tumia chaneli hii (jina la chaneli) ninapoingia katika akaunti yangu ya <barua pepe>."
  5. Bofya Hifadhi.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
13690963586528993015
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false