Kutumia lahajedwali la kupakia Video za Picha

Vipengele hivi vinapatikana tu kwa washirika wanaotumia Kidhibiti Maudhui cha YouTube kudhibiti maudhui yao yaliyo na hakimiliki.

Ili utayarishe Video za Picha za rekodi zako, unahitaji kuwasilisha faili za maudhui na metadata za rekodi. Unawea kutayarisha vipengee vya video ya picha kwa kupakia faili ukitumia Mipasho ya DDEX ya YouTube Music au lahajedwali la kupakia faili nyingi ya “Sauti - Video za Picha”.

Huwezi kuweka majina ya wasanii au vichwa vilivyotafsiriwa ukitumia lahajedwali, au orodha ya wachangiaji. Unahitaji kutumia mipasho ya DDEX ili kujumuisha vipengee hivi.

Ili kutayarisha Video za Picha ukitumia lahajedwali:

  1. Ingia katika akaunti ya Kidhibiti Maudhui cha Studio.

  2. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Uwasilishaji wa maudhui .

  3. Bonyeza kichupo cha Violezo.

  4. Pata kiolezo cha Sauti - Video za Picha na ubofye aikoni ya kupakua ya .

  5. Weka metadata ya rekodi yako ya sauti kwenye lehajedwali, rekodi moja kwa kila safu mlalo.

    Kiolezo cha lahajedwali kina maelezo kuhusu data ya kuweka kwenye kila safu wima. Angalia Kutayarisha Video za Picha kwa maelezo kuhusu jinsi YouTube inavyotumia metadata katika Video ya Picha inayotayarishwa. Angalia Mwongozo wa kubadilisha muundo wa lahajedwali kwa maelezo kuhusu muundo sahihi wa lahajedwali

    Sehemu zote zinahitaji kuwekwa katika muundo wa maandishi dhahiri, ikiwa ni pamoja na sehemu ambazo thamani zake ni tarehe au zenye nambari za kipekee (kama vile UPC).
  6. Unapokuwa na lahajedwali lako lililokamilika na faili za maudhui zilizorejelewa, endelea kwa kufuata hatua katika Pakia maudhui kwa kutumia Kipakiaji cha vifurushi.

    Kwa maelezo kuhusu masharti ya faili za kazi ya sanaa na rekodi, angalia Aina ya faili ili upate nyenzo.

     

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
11333366731056055222
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false