Kutazama, kupanga au kufuta maoni

Jinsi ya kuchapisha na kushirikiana kupitia maoni kwenye YouTube

Fuatilia chaneli ya Watazamaji ya YouTube ili upate habari, taarifa na vidokezo vipya.

Ikiwa mmiliki wa video amewasha maoni, unaweza kuchapisha maoni na kuweka alama ya imenipendeza, haijanipendeza kujibu maoni mengine katika video

Kutazama maoni kwenye video

Ili utazame maoni katika video, nenda kwenye ukurasa wa video. Majibu yamewekwa kwa mpango wa kufuatana ili iwe rahisi kufuata mazungumzo. Maoni ya YouTube huonyeshwa hadharani na mtu yeyote anaweza kujibu maoni unayochapisha.

Iwapo huwezi kupata maoni baada ya kupata arifa, inawezekana kuwa maoni hayo tayari yameondolewa. Maoni yanaweza kuondolewa na mchapishaji halisi, mmiliki wa kituo au kwa kukiuka sera.

Iwapo unafikiri maoni hayafai, unaweza kuyaripoti kama taka au matusi. Iwapo wewe ni mtayarishi, unaweza pia kutumia zana za kudhibiti maoni ili kudhibiti maoni kwenye video zako.
Angalia historia yako ya maoni

Unaweza kutazama maoni ya umma uliyotoa kwenye YouTube.

  1. Nenda kwenye Historia ya Maoni.
  2. Ili uende kwenye sehemu halisi ulipochapisha maoni yako, bofya au uguse maoni hayo.

Iwapo ulitoa maoni kwenye video iliyofutwa au iwapo YouTube iliondoa maoni yako kwa kukiuka sera, hayataonekana katika historia hii.

Pata kiungo kinachoweza kushirikiwa kwa ajili ya maoni

Unaweza kubofya au kugusa muhuri wa wakati wa maoni ili ubuni kiungo cha maoni yaliyoangaziwa. Kitendo hiki kitakupa kiungo kinachoweza kushirikiwa katika sehemu ya anwani ya maoni hayo mahususi na mfululizo wake.

Badilisha maoni yanayoonekana kwanza

Kwenye wavuti, unaweza kubadilisha jinsi maoni huonekana chini ya video. Tumia chaguo la Panga Kulingana Na ili uchague Maoni maarufu au Maoni mapya zaidi kwanza.

Bofya muhuri wa wakati ili ubuni kiungo cha 'Maoni Yaliyoangaziwa'. Kitendo hiki kitatenga mfululizo wa maoni yako na kutoa kiungo kinachoweza kushirikiwa katika sehemu ya anwani.

Futa maoni
  1. Nenda kwenye Historia ya Maoni.
  2. Bofya au uguse kiungo cha video.
  3. Karibu na maoni katika YouTube, chagua Zaidi ''.
    1. Chagua Badilisha  au Futa .

Kuwasiliana kupitia maoni kwenye televisheni yako inayoweza kuunganisha kwenye intaneti

Sasa unaweza kuangalia na kuwasiliana kupitia maoni unapotazama maudhui katika televisheni inayoweza kuunganisha kwenye intaneti au kifaa chako cha michezo ya video. Ili uangalie maoni ya video, nenda kwenye ukurasa wa kutazama wa video na uchague mada ya video. Sehemu ya Kuhusu itaonekana, ikiangazia kidirisha cha maoni ya video. Chagua kigae cha maoni ili uone orodha kamili ya maoni ya video, ikiwa ni pamoja na:

  • Maoni ambayo mtayarishi amebandika
  • Mara za kupendwa
  • Idadi ya majibu 

Chagua maoni mahususi ili uyasome yote, uangalie majibu, uweke alama ya kupendezwa au kutopendezwa na maoni hayo.

Ili ujibu au uchapishe maoni, sawazisha televisheni yako inayoweza kuunganisha kwenye intaneti au kifaa chako cha michezo ya video na simu yako na utoe maoni kwa kutumia simu yako. 

Ili uweke maoni au jibu:

  1. Fungua programu ya YouTube kwenye simu yako.
  2. Hakikisha kuwa umeingia katika Akaunti sawa ya Google kwenye vifaa vyote viwili. 
  3. Dirisha ibukizi litafunguka kwenye programu yako ya YouTube, litakalokuomba uunganishe YouTube kwenye televisheni yako.
  4. Gusa kipengele cha Unganisha.
  5. Maoni ya video unayotazama kwenye televisheni yako yatapakiwa kwenye programu ya YouTube, hali itakayokuruhusu kuyachapisha na kuyashughulikia kwa urahisi.
Kumbuka: Ukiwa umeondoka kwenye akaunti, unaweza kuona maoni, lakini huwezi kuyajibu au kuchapisha maoni yako mwenyewe.

 

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
3456508098056410850
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false