Zana za YouTube za kutafsiri maudhui yako

Kwa wastani, thuluthi mbili za muda wa kutazama wa hadhira ya mtayarishi hutoka nje ya eneo lake la nyumbani. Ili ukuze hadhira yako ya kimataifa, fanya video zako ziweze kufikiwa kwa urahisi zaidi kwa lugha nyingine ukitumia zana zetu za tafsiri:

  • Metadata iliyotafsiriwa inaweza kuongeza ufikiaji na uwezo wa kutambulika wa video. Majina na maelezo ya video yaliyotafsiriwa yanaweza kuonekana katika matokeo ya utafutaji kwenye YouTube kwa watazamaji wanaozungumza lugha hizo nyingine.
  • Watazamaji wanaozungumza lugha nyingine wanaweza pia kupata na kutazama video zako zozote zilizo na manukuu.
  • Manukuu ya lugha sawa hufanya video zako zipatikane kwa watazamaji viziwi na walio na matatizo ya kusikia, wazungumzaji wasio wenyeji wa lugha husika na watazamaji katika mazingira yenye kelele.

Zana za kutafsiri maudhui yako

Kuweka tafsiri zako mwenyewe
  • Weka majina na maelezo ya video yaliyotafsiriwa kwenye video zako. Watazamaji wanaweza kugundua video zako katika lugha zao wenyewe. Tutaonyesha jina na maelezo ya video katika lugha inayofaa, kwa watazamaji wanaofaa.
  • Ili ufikie hadhira kubwa zaidi, ongeza manukuu yako mwenyewe. Hatua hii itawafaa zaidi watazamaji walio na matatizo ya kusikia.

Kutumia manukuu ya kiotomatiki

Unaweza kuwasha kipengele cha kutumia teknolojia ya utambuzi wa matamshi ili manukuu yawekwe kiotomatiki kwa lugha ya asili ya video.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Programu za Google
Menyu kuu
16716977579507305106
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
false
true
true
true
true
true
59
false
false
false
false