Kipengele cha ruhusa za chaneli hukuwezesha kuwapatia watumiaji wengine idhini ya kufikia chaneli yako kupitia majukumu mahususi. Kubainisha majukumu hukuwezesha kuchagua kiwango sahihi cha ufikiaji. Hamia kipengele cha ruhusa za chaneli ili uzuie hatari za usalama kama vile kushiriki nenosiri na upunguze mashaka mengine ya faragha.
Iwapo chaneli yako ya YouTube imeunganishwa na Akaunti ya Biashara, wanachama kadhaa wanaweza kudhibiti chaneli kupitia Akaunti zao za Google. Huhitaji jina tofauti la mtumiaji au nenosiri kudhibiti chaneli za YouTube kupitia Akaunti ya Biashara. Akaunti ya Biashara inaweza kuunganishwa na chaneli ya YouTube lakini si Huduma nyingine za Google.
Kwanza, angalia iwapo chaneli yako imeunganishwa na Akaunti ya Biashara. Iwapo haipo, unaweza kubadilisha wasimamizi wa chaneli, lakini si wamiliki. Ili uhamishe umiliki wa chaneli, badilisha iwe Akaunti ya Biashara kwa kuondoa majukumu yote yaliyo katika ruhusa zilizowekwa.
Kutatua hitilafu za kuweka majukumu kwenye Akaunti za Biashara
Unapaswa kutumia ruhusa za chaneli kudhibiti ufikiaji wa mtumiaji wa chaneli yako.
Ikiwa unahitaji kutumia majukumu ya Akaunti ya Biashara (haipendekezwi) na unatatizika kuweka mengine, huenda ukahitajika kujiondoa kwenye ruhusa za chaneli kisha ujiunge tena baadaye. Ili urudi kwenye Akaunti yako ya Biashara, ni lazima umwalike kila mtu kwenye Akaunti ya Biashara tena.
Ili ujiondoe, chagua “Jiondoe kwenye ruhusa katika Studio ya YouTube” kwenye Mipangilio ya Studio ya YouTube Ruhusa. Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kujiondoa kwenye ruhusa za kituo.
Kuangalia au kuweka majukumu kwenye Akaunti yako ya Biashara
Tumia majukumu kwenye Akaunti ya Biashara ikiwa tu inahitajika. Ni muhimu kutoa kiwango kinachofaa cha idhini kwa watumiaji ili uepuke matatizo ya usalama. Epuka kufanya vitu hatari kama vile kushiriki manenosiri.
Ni wajibu wa mmiliki wa kituo kufahamu maelezo ya umiliki wake wa Akaunti ya Biashara. Tunapendekeza uangalie ruhusa za Akaunti ya Biashara mara kwa mara ili udumishe usalama wa akaunti yako.
Ili uone anayesimamia Akaunti yako ya Biashara:
- Nenda katika sehemu ya Akaunti za Biashara ya Akaunti yako ya Google.
- Katika sehemu ya "Akaunti Zako za Biashara," chagua akaunti unayotaka kuangalia.
- Chagua Dhibiti ruhusa. Utapata orodha ya watu wanaoweza kudhibiti akaunti, ikijumuisha wamiliki.
Kualika watu wapya kwenye Akaunti yako ya Biashara:
- Ili ualike watu wapya, chagua Alika watumiaji wapya .
- Weka anwani zao za barua pepe.
- Chini ya majina yao, wachagulie jukumu:
- Wamiliki wanaweza kutekeleza vitendo vingi na wanadhibiti wanaosimamia akaunti. Ni lazima akaunti iwe na mmiliki mkuu mmoja.
- Wasimamizi wanaweza kutumia Huduma za Google zinazotumika kwenye Akaunti za Biashara (kwa mfano, kushiriki picha katika Picha kwenye Google au kuchapisha video kwenye YouTube).
- Wasimamizi wa mawasiliano wanaweza kufanya vitendo sawa na vya Wasimamizi, lakini hawawezi kutumia YouTube.
- Gusa Alika Nimemaliza.
Yeyote utakayemwalika atapokea barua pepe ambapo anaweza kukubali mwaliko wako.
Jiwekee mipangilio ya mmiliki mkuu wa Akaunti yako ya Biashara
Pamoja na kuwa na mmiliki mkuu mmoja kwenye Akaunti ya Biashara, tunapendekeza kuwa uwe na angalau mmiliki mwingine mmoja anayehusishwa na Akaunti yako ya Biashara.
Ikiwa umeshindwa kumteua mmiliki mkuu mpya, thibitisha kuwa umeondoka kwenye ruhusa za kituo. Wasimamizi hawatakuwa na chaguo la kubadilisha jukumu la mmiliki mkuu.
- Kwenye kompyuta yako, nenda katika sehemu ya Akaunti za Biashara ya Akaunti yako ya Google.
- Chini ya "Akaunti Zako za Biashara," chagua akaunti unayotaka kudhibiti.
- Bofya Dhibiti ruhusa.
- Tafuta jina lako kwenye orodha.
- Kidokezo: Ikiwa umeshindwa kupata jina lako, ni lazima mmiliki mwingine wa kituo akuweke uwe mmiliki. Baada ya kukubali mwaliko na kusubiri siku 7, jaribu tena ukianzia hatua ya 1.
- Karibu na jina lako, bofya kishale cha chini Mmiliki mkuu Hamisha.