Unaweza kuweka orodha za kucheza ulizotayarisha, ambazo Watayarishi wengine wametayarisha na video ulizoweka katika orodha ya kucheza ya Tazama Baadaye kwenye kichupo chako cha Wasifu. Kuhifadhi orodha za kucheza hukuwezesha kuzipata kwa urahisi na kuzitazama baadaye.
Iwapo unamiliki orodha ya kucheza, unaweza kuiweka hadharani kwenye Maktaba yako ili watazamaji wako waweze kuiweka kwenye Maktaba zao. Unaweza kusasisha mipangilio yako ya faragha ili uondoe orodha zako za kucheza kwenye mwonekano. Kwa kuondoa, bado unaweza kuona orodha za kucheza zilizohifadhiwa katika kituo chako, lakini watazamaji wengine hawataziona.
Programu ya YouTube
Kuweka orodha ya kucheza kwenye Maktaba yako
Kwenye ukurasa wa chaneli
- Gusa kichupo cha ORODHA ZA KUCHEZA ili uone orodha za kucheza za kituo hicho.
- Gusa Zaidi
karibu na maelezo ya orodha ya kucheza.
- Gusa Hifadhi.
Unapotazama video
Iwapo unatazama video ambayo ni sehemu ya orodha ya kucheza, gusa Hifadhi .
Kuangalia orodha za kucheza ulizohifadhi na ulizotayarisha
Ili uangalie orodha za kucheza ulizohifadhi na ulizotayarisha, nenda kwenye kichupo cha Wasifu.
Tovuti ya kifaa cha mkononi
Kuweka orodha ya kucheza kwenye Maktaba yako
Unapotazama video
Unapotazama video ambayo ni sehemu ya orodha ya kucheza, gusa Hifadhi .
Kuangalia orodha za kucheza ulizoweka kwenye Maktaba
Unaweza kuangalia orodha za kucheza ulizoweka kwenye Maktaba yako na ulizotayarisha kwa kugusa kichupo cha Maktaba .