Kualika mtumiaji kwenye Kidhibiti chako cha Maudhui

Vipengele hivi vinapatikana tu kwa washirika ambao hutumia Kidhibiti Maudhui cha Studio ya YouTube. Wasiliana na Msimamizi wako wa Washirika wa YouTube ili uweze kuvitumia.
Shirika lako linapofungua akaunti ya Kidhibiti Maudhui, mtumiaji mmoja huchukua jukumu la msimamizi. Msimamizi anaweza kuwaalika watu wengine ili wadhibiti maudhui. 

Wasimamizi wanaweza pia kutunga majukumu tofauti yanayobainisha vipengele vinavyopatikana kwa watumiaji mahususi na vizuizi vinavyotumika. Pata maelezo zaidi kuhusu kutunga majukumu na kuweka mipangilio ya Kidhibiti chako cha Maudhui.

Mwaliko ukishatumwa, muda wa kuutumia utaisha baada ya siku 30.

Tuma mwaliko

Kabla ya kutuma mwaliko, hakikisha mtumiaji unayetaka kumwalika ana akaunti ya Google. Anwani za barua pepe zilizounganishwa na akaunti za Google ndizo tu zinazoweza kualikwa.

  1. Ingia katika akaunti ya Kidhibiti Maudhui cha Studio.
  2. Kwenye menyu ya kushoto, bofya Mipangilio.
  3. Bofya Ruhusa. Ukurasa huu huonyesha orodha ya watumiaji walio na idhini ya kufikia Kidhibiti Maudhui na jukumu walilokabidhiwa.
  4. Bofya ALIKA.
  5. Katika sehemu ya Barua pepe, weka anwani ya barua pepe ya mtumiaji unayetaka kumwalika.
  6. Katika sehemu ya Idhini ya kufikia, chagua jukumu ambalo ungepend kumkabidhi mtumiaji uliyemwalika. Pata maelezo zaidi kuhusu majukumu.
  7. Bofya NIMEKAMILISHA.
  8. Kwenye ukurasa wa Ruhusa, bofya HIFADHI ili utume mwaliko.
    • Kumbuka, muda wa kutumia mialiko utaisha baada ya siku 30.

Kuthibitisha kuwa mwaliko umetumwa

Baada ya mwaliko kutumwa, ujumbe wa kuthibitisha utaonekana katika sehemu ya chini ya ukurasa waRuhusa. Unaweza pia kurudi baadaye na kuthibitisha ikiwa ulituma mwaliko kwenye ukurasa wa Ruhusa:

  1. Bofya Chagua kichujio .
  2. Chagua Neno muhimu.
  3. Weka anwani ya barua pepe ya mtumiaji uliyemwalika.
  4. Bofya TUMIA.
  5. Hakikisha kuwa aikoni ya Amealikwa  inaonekana kando ya barua pepe yake.
    • Ikiwa aikoni ya Amealikwa inaonekana, inamaanisha ulituma mwaliko bila tatizo. Sasa mtu aliyealikwa anahitaji kukubali mwaliko akitumia kiungo katika barua pepe yake.
    • Ikiwa aikoni ya Amealikwa haipo, inamaanisha mtumiaji ameshakubali mwaliko na anaweza kudhibiti maudhui.
    • Iwapo barua pepe yake haijaorodheshwa, huenda ikamaanisha kuwa mwaliko haukutumwa. Thibitisha unatumia anwani sahihi ya barua pepe na utume tena mwaliko.
Kumbuka: Baadhi ya viendelezi vya wengine vinawez kugeuza isivyo orodha ya watumiaji au majukumu. Ukikabiliwa na hitilafu zozote za ruhusa, zima viendelezi vya wengine na ujaribu kufanya mabadiliko yako tena.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
9248790718485708360
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false