Kutuma maoni

Kuripoti hitilafu kwenye YouTube

  1. Ingia katika akaunti kwenye YouTube.
  2. Chagua picha yako ya wasifu .
  3. Chagua Tuma maoni.
  4. Elezea hitilafu inayokukumba. Jinsi unavyoweka maelezo mengi zaidi kwenye ripoti yako, ndivyo unavyotusaidia kuelewa zaidi.
  5. Chagua iwapo ungependa kujumuisha picha ya skrini. Unaweza kuangazia maelezo kwenye skrini au kuondoa taarifa binafsi.
  6. Bofya Tuma.
Fuatilia chaneli ya Watazamaji ya YouTube ili upate habari, taarifa na vidokezo vipya.

Televisheni zinazoweza kuunganisha kwenye intaneti, Chromecast na vifaa vya michezo ya video

  1. Fungua programu ya YouTube kwenye kifaa chako.
  2. Katika ukurasa wa kutazama wa video yoyote, chagua Mipangilio .
  3. Chagua Maoni.
  4. Chagua sababu ya kutoa maoni.
  5. Chagua Tuma Ripoti.

Jinsi tunavyotumia maoni

Tunathamini muda unaotumia kututumia maoni. Maoni yako yanapelekwa moja kwa moja YouTube na tunayatumia kutatua hitilafu, kufanya maboresho ya bidhaa na kurekebisha matatizo. Watayarishi wa video hawaoni maoni yoyote yanayotumwa kupitia zana ya "Tuma Maoni". Ingawa hatuwezi kujibu kila ripoti, tunakagua na kushughulikia utatuzi wa hitilafu haraka iwezekanavyo.

Unapotuma maoni moja kwa moja kutoka YouTube kupitia kifaa chako cha mkononi, unaweza kuchagua kujumuisha maelezo muhimu. Maelezo haya husaidia kuchunguza hitilafu, kama vile toleo la programu na data ya mfumo. Jinsi unavyoweka maelezo mengi zaidi kwenye ripoti yako, ndivyo unavyotusaidia zaidi. Kwa mfano, Tunapotatua aina fulani za hitilafu, maelezo mahususi ya akaunti na picha za skrini kwa kiasi kikubwa husaidia kugundua na kurekebisha tatizo.

Unaweza kutumia Ukurasa wa Hitilafu Zinazojulikana yetu ili uone hitilafu ambazo kwa sasa tunashughulikia ili kuzitatua. Unaweza pia kuwaomba watumiaji wengine wa YouTube ili wakusaidie kutatua hitilafu kwenye Mijadala ya Usaidizi kwenye YouTube. Vilevile, ikiwa wewe ni Mtayarishi wa YouTube, pata maelezo kuhusu kupata usaidizi kwa kusoma makala haya.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
3324560492291891921
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false