Kupata takwimu za orodha na vikundi vyako vya video

Unaweza kufikia kwa urahisi takwimu za orodha zako au kuweka video zako kwenye vikundi ili uangalie data yake pamoja.

Orodha

Unaweza kutumia orodha ili upange maudhui yako. Zinakuwezesha kuweka video kwenye vikundi na ufikie kwa urahisi takwimu zako katika sehemu moja. Kwa kila orodha yako, unaweza kufikia kichupo cha Muhtasari, Maudhui, Hadhira na Mapato ili upate maarifa yaliyojumlishwa pamoja ya video zako zote kwenye orodha. Pata maelezo kuhusu jinsi ya kubuni orodha.

Kufikia takwimu za orodha yako

Ili uangalie takwimu za orodha:

  1. Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
    • Au fungua programu ya Studio ya YouTube .
  2. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Maudhui .
  3. Chagua kichupo cha Orodha za video.
  4. Karibu na jina au maelezo ya orodha ya video ambayo ungependa kuangalia, chagua Takwimu .

Ili ulinganishe takwimu za orodha nyingi za video: 

  1. Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
    • Au fungua programu ya Studio ya YouTube .
  2. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Takwimu .
  3. Chagua kichupo cha Maudhui kisha Orodha za video.
    • Kumbuka: Kwa chaguomsingi, utaona orodha 5 maarufu za video katika siku 28 zilizopita.
  4. Unaweza kulinganisha orodha nyingi au ubofye kwenye orodha mahususi unayotaka kuangalia.

Jinsi takwimu za orodha ya kucheza hufanya kazi

Takwimu za orodha hutumia ripoti ya kikundi cha video ili kuonyesha takwimu zilizojumlishwa za video zote zilizo kwenye orodha. Kwa kila orodha yako, unaweza kufikia kichupo cha Muhtasari, Maudhui, Hadhira na Mapato ili upate maarifa yaliyojumlishwa pamoja ya video zako zote kwenye orodha. Pia, kuna vipimo vya kukusaidia uelewe tabia ya watazamaji katika kila orodha. Pata maelezo zaidi kuhusu vipimo vya orodha.
Video zisizojumuishwa kwenye takwimu za orodha ya kucheza

Vipimo kadhaa kwenye takwimu za orodha yako havijumuishi video zinazomilikiwa na chaneli zingine. Vipimo hivi hujumlisha shughuli zote za watazamaji kwenye video, bila kujali iwapo imetazamwa kwenye orodha au kwingineko kwenye YouTube. Kwa mfano, Jumla ya mara za kutazamwa, Hadhira na maarifa ya Mapato havijumuishi video kutoka kwa chaneli zingine.

Vipimo vingine kama vile mara za kutazamwa kwenye orodha, muda wa kutazama orodha na muda wa wastani wa kucheza orodha vinajumuisha video kutoka kwa chaneli zingine. Vipimo hivi vinaonyesha tu shughuli za watazamaji katika muktadha wa orodha yako.

Kumbuka kwamba unaweza kudhibiti video kwenye orodha yako moja kwa moja ndani ya Studio ya YouTube. Pata maelezo kuhusu jinsi ya kudhibiti orodha yako.

Vikundi

Vikundi ni mkusanyiko wa hadi video zako 500 zinazoweza kuwekewa mapendeleo. Unaweza kupanga maudhui yanayofanana pamoja na uone data yake katika sehemu moja ukitumia vikundi.

Unda vikundi

  1. Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
  2. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Takwimu.
  3. Bofya HALI YA KINA au ANGALIA ZAIDI ili uangalie ripoti iliyopanuliwa ya takwimu.
  4. Katika sehemu ya juu kushoto, bofya jina la chaneli katika upau wa kutafutia.
  5. Chagua kichupo cha Vikundi, kisha uchague UNDA KIKUNDI KIPYA.
  6. Weka jina la kikundi, chagua video na Hifadhi.

Dhibiti vikundi

  1. Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
  2. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Takwimu.
  3. Bofya HALI YA KINA au ANGALIA ZAIDI ili uangalie ripoti iliyopanuliwa ya takwimu.
  4. Katika sehemu ya juu kushoto, bofya jina la chaneli katika upau wa kutafutia.
  5. Chagua kichupo cha Vikundi, kisha uchague kikundi.
  6. Unaweza kubadilisha , kufuta na kupakua  data ya vikundi vyako.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
2042005659368988967
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false