Kufahamu mipasho ya YouTube DDEX

Vipengele hivi vinapatikana tu kwa washirika wanaotumia Kidhibiti Maudhui cha YouTube kudhibiti maudhui yao yaliyo na hakimiliki.

Hadhira inayolengwa na hati hii ni washirika wa muziki ambao wangependa kufanya jambo moja au yote mawili kati ya yafuatatyo:

  • Kupakia Video ya Picha kwenye YouTube Premium.
  • Kupakia Video za Muziki kwenye vituo vyao.
  • Kudhibiti haki za rekodi ya sauti na/au video za muziki kupitia mfumo wa YouTube wa Content ID.

YouTube hutumia Matoleo ya 3.4 hadi 3.8 ya DDEX ya kiwango cha Arifa za Matoleo ya Kielektroniki (ERN). Hati hii inafafanua masharti mahususi ya mipasho ya YouTube Music DDEX. Kwa utangulizi wa jumla wa DDEX, angalia Mwongozo wa Mtindo wa Metadata ya Muziki kutoka Music Business Association. Kwa maelezo kuhusu kiwango cha DDEX ERN, angalia ddex.net. Mipasho yote inayowasilishwa kwenye YouTube inapaswa kufuata wasifu wa Albamu ya Sauti au wasifu wa Utoaji wa Nyenzo Moja, jinsi ilivyochapishwa na DDEX.

Kila ujumbe wa DDEX ERN hujumuisha vipengele vinne vya viwango vya juu:

  • <MessageHeader> huonyesha maelezo kuhusu ujumbe wenyewe: nambari maalum ya utambulisho, mtumaji na mpokeaji; na muhuri wa wakati.
  • <ResourceList> huonyesha maelezo kuhusu rekodi ya sauti na kazi ya sanaa husika.
  • <ReleaseList> hufafanua matoleo ambayo yanaweza kuandaliwa kutoka kwenye nyenzo katika ujumbe huu.
  • <DealList> hufafanua maelezo muhimu ya kibiashara kwa kila toleo, kama vile maeneo ambako toleo linaweza kupatikana, haki za matumizi na tarehe ya kuanza kwa kila toleo.

Vifurushi vya Video ya Picha vya DDEX huchakatwa kulingana na mpangilio ambao vimepokelewa, kulingana na muhuri wa wakati wa faili ya BatchComplete ambayo hukamilisha kifurushi hiki.

Kulingana na kanuni za DDEX, jina la faili ya DDEX linapaswa kujumuisha kitambulisho maalum cha toleo la albamu. Kitambulisho cha toleo huwa UPC, EAN, au GRid kilichotelewa na kipengele cha <ReleaseId>.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
7026113213920824860
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false