Kutazama YouTube kwenye Xbox One

Sasa unaweza kutazama video za YouTube kwenye Xbox One. Katika programu ya YouTube unaweza kuona vituo unavyofuatilia, kutafuta video, na kutumia kifaa chako cha mkononi kama kidhibiti cha mbali.

Pakua programu ya YouTube

Ingia au uondoke katika akaunti ya YouTube

Unapofungua programu ya YouTube mara ya kwanza, unaweza kuingia kupitia Akaunti yako ya Google. Ukiwa umeingia katika akaunti, una uwezo wa kufikia vipengele zaidi vya YouTube kama vile orodha za kucheza na vituo unavyofuatilia.

Ingia katika akaunti ya Xbox One:

  1. Nenda kwenye Mipangilio ya Kuingia katika akaunti
  2. Chagua INGIA KATIKA AKAUNTI. Utapata msimbo wa kuanza kutumia. 

Ingia katika akaunti kwenye kompyuta yako:

  1. Nenda kwenye www.youtube.com/activate kisha uweke msimbo wa kuanza kutumia ulioonyeshwa kwenye Xbox One. 
  2. Bofya Ruhusu Ufikiaji, hatua inayokamilisha mchakato wa kuingia katika akaunti.

Pata maelezo kuhusu jinsi ya kutenganisha akaunti yako kwenye Xbox One.

Vidhibiti vya video

Baada ya kuchagua video ya kucheza, upau wa vidhibiti vya kichezaji utaonekana utakaokuruhusu kufanya yafuatayo:

  • Kurudisha Nyuma  - Bonyeza A ili uongeze kasi ya kurudi nyuma.

  • Kusimamisha/kuendelea  - Kusimamisha au kuendelea kucheza video.
  • Kusogeza mbele haraka  - Bonyeza A ili uzidishe kasi ya kusogeza mbele.
  • Kuweka Manukuu  - Iwapo video ina manukuu, chagua hili ili uone manukuu ya video.

Tumia kitufe cha B urudi kuvinjari video.

Vidhibiti vya sauti na ishara

Unaweza pia kudhibiti programu ya YouTube kwa kutumia sauti au ishara zako.

Sauti

Ili uwashe kipengele cha kudhibiti kwa sauti, sema "Xbox Chagua". Sasa unaweza kusema neno au kifungu chochote kilichoangaziwa kwenye skrini ili ufungue kipengee hicho.

Ishara

Ili uwashe vidhibiti vya ishara, pepea mkono wako mbele ya dashibodi yako na aikoni inapaswa kuonekana kwenye skrini yako. Sukuma mkono wako mbele ili uchague kipengee. Unaweza pia kufunga mkono wako ili "ushikilie" video na usogeze kushoto ili urudi nyuma au kulia ili usogeze mbele.

Kuoanisha kifaa chako cha mkononi

Tumia kifaa chako cha mkononi kama kidhibiti cha mbali. Pata maelezo kuhusu jinsi ya kuunganisha Xbox One kupitia m.youtube.com, Programu ya YouTube ya Androidau programu ya YouTube ya iOS.

Ubora wa video

YouTube inapatikana katika ubora wa 4K kwenye miundo ya Xbox One S, Xbox One X, Xbox Series S, na Xbox Series X. Ubora wa juu zaidi wa kifaa halisi cha Xbox One ni 1080p. Uchezaji wa HDR unaruhusiwa kwenye miundo ya Xbox One S, Xbox One X, Xbox Series S, na Xbox Series X.
YouTube inapatikana katika ubora ufuatao kwenye vifaa vya Xbox One.
  • Xbox One: hadi 1080p kwa fremu 60 kwa sekunde
  • Xbox One S: hadi 4K kwa fremu 60 kwa sekunde
  • Xbox One X: hadi 4K kwa fremu 60 kwa sekunde

Uchezaji wa HDR unaruhusiwa kwenye miundo ya Xbox One S, Xbox One X, Xbox Series S, na Xbox Series X. 

Ujumbe kuhusu hitilafu kwenye Xbox

Ukiona ujumbe kuhusu hitilafu unaosema “YouTube haipatikani sasa hivi,” huenda muunganisho wako wa intaneti si thabiti.

Fuata mwongozo wetu wa utatuzi ili ukusaidie kutatua tatizo hilo. 

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
4316489684162069973
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false