Kudhibiti arifa za YouTube

Arifa za YouTube zinakufahamisha kunapokuwa na video na taarifa mpya kutoka katika vituo unavyopenda na maudhui mengine. Tutakutumia arifa kuhusu vituo unavyofuatilia na huenda pia tukakutumia arifa kulingana na mambo yanayokuvutia. Ili ubadilishe au uzime kabisa arifa zako, tumia maagizo yaliyo hapa chini.

Fuatilia chaneli ya Watazamaji ya YouTube ili upate habari, taarifa na vidokezo vipya.
Kumbuka: Mipangilio ya arifa inaweza kutofautiana kidogo kulingana na kifaa na si kila mara unapopakia maudhui mapya watazamaji watapata arifa.

Tofauti kati ya Arifa na Mipasho ya Vituo Unavyofuatilia

Mipasho ya Chaneli Unazofuatilia, inayopatikana kwenye vifaa vya mkononi na kompyuta, huonyesha video zozote zilizopakiwa hivi karibuni kutoka kwenye chaneli unazofuatilia.

Arifa zinaweza kukueleza kunapokuwa na video mpya, kutuma masasisho kutoka kwa usajili wako na pia zinaweza kukuarifu kuhusu maudhui ambayo unaweza kuyapenda. Tutakutumia barua pepe, arifa zilizowekewa mapendeleo kwenye vifaa vya mkononi au arifa kwenye kikasha katika kompyuta au kifaa chako cha mkononi. Unapofuatilia chaneli, utapata kiotomatiki arifa zilizowekewa mapendeleo zinazoangazia shughuli.

Arifa kwenye kikasha hupangwa kulingana na wakati, arifa mpya zaidi zikiwa katika sehemu ya juu. Baadhi ya arifa zinaweza kuangaziwa juu ya arifa mpya zaidi katika sehemu ya "Muhimu", ambayo inaangazia arifa tunazodhani zinaweza kuwa muhimu zaidi kwako. Mifano ya arifa muhimu inaweza kujumuisha jibu kwa maoni yako au watu wanapotuma video zako.

Ili upate arifa zote kutoka kwenye chaneli unayofuatilia, gusa kengele ya Arifa  . Kisha kengele hiyo itabadilika na kuwa kengele inayolia  ili kuashiria kuwa umechagua arifa zote.

Hutapata arifa iwapo mipangilio ya chaneli imewekwa kuwa inalenga watoto. Kengele ya arifa itawekewa mipangilio ya hamna arifa . Huwezi kubadilisha mipangilio hii.

Maana ya kengele za arifa za vituo unavyofuatilia

 Arifa zilizowekewa mapendeleo (Chaguomsingi)
 Hakuna arifa
 Arifa zote

Ukifuatilia kituo au video ambayo imewekewa mipangilio kuwa inalenga watoto, mipangilio yako ya kengele itawekwa kuwa hakuna arifa  na haitaweza kutumiwa

Kabla hujaanza: Hakikisha kuwa umeingia katika akaunti sahihi. Unaweza kupata mipangilio ya akaunti yako ya YouTube hapa:

  1. Ingia katika akaunti kwenye YouTube.
  2. Katika sehemu ya juu ya skrini yako, bofya picha yako ya wasifu.
  3. Bofya Mipangilio.
  4. Bofya Arifa.

Kupata taarifa kutoka vituo mahususi

Unapofuatilia kituo, utapata kiotomatiki arifa zenye mihtasari ya shughuli za kituo hicho na video zote mpya zitakuwa kwenye Mpasho wa Vituo unavyofuatilia. Unaweza kubadilisha mipangilio yako ya arifa ili tukujulishe kila mara kituo kinapochapisha maudhui au uzime arifa kabisa. 

Pata taarifa kutoka kwenye kituo unapokifuatilia:

  1. Nenda kwenye ukurasa wa kituo au ukurasa wa kutazama.
  2. Ikiwa bado hufuatilii kituo, bofya Fuatilia. Unapofuatilia kituo, utapokea kiotomatiki arifa zilizowekewa mapendeleo.
  3. Bofya kengele ya Arifa ili ubadilishe kati ya kupokea “Arifa zote” na “Arifa zilizowekewa mapendeleo.”
    • Arifa zote - Utapokea arifa kuhusu mitiririko mubashara na video zozote ndefu zinazopakiwa. Huenda pia ukapokea baadhi ya arifa zilizowekewa mapendeleo zinazohusu Video Fupi kulingana na vituo unavyofuatilia na historia ya video ulizotazama.
    • Arifa zilizowekewa mapendeleo - Utapokea arifa kuhusu baadhi ya mitiririko mubashara, Video Fupi na video zilizopakiwa. Maana ya "zilizowekewa mapendeleo" hutofautiana kwa kila mtumiaji. YouTube hutumia viashiria mbalimbali kuamua wakati wa kukutumia arifa. Maelezo haya ni pamoja na historia ya video ulizotazama, mara ambazo unatazama vituo fulani, umaarufu wa baadhi ya video na mara ambazo unafungua arifa.

Ukiacha kufuatilia chaneli na kisha uanze kukifuatilia tena, mipangilio yako ya arifa itabadilishwa kuwa arifa zilizowekewa mapendeleo au hamna arifa. Ikiwa ungependa kupokea arifa kuhusu kila video inayopakiwa, hakikisha unawasha arifa zote.

Kuangalia arifa zako

Sasa unaweza kuangalia na kupata arifa kwenye kompyuta yako.
  1. Kwenye kivinjari chochote, fungua YouTube
  2. Katika sehemu ya juu ya ukurasa, bofya kengele ya Arifa   ili uangalie arifa.
  3. Chagua arifa unayotaka kufungua ili utazame video au maoni. 
Unaweza pia kudhibiti arifa kwenye kikasha cha kompyuta yako.
  1. Karibu na arifa, bofya Zaidi ''.
  2. Bofya Ficha arifa hiiZima arifa zote kutoka <channel name> au Zima taarifa zote za [type of notification].

Kuchagua aina ya arifa unazotaka

Unaweza kudhibiti aina ya arifa unazopokea kutoka YouTube na jinsi unavyozipokea.

  1. Ingia katika akaunti kwenye YouTube.
  2. Nenda kwenye mipangilio yako ya arifa.
  3. Chini ya sehemu tofauti kwenye ukurasa, chagua arifa unazotaka:
    • Vituo unavyofuatilia: Hukuarifu kuhusu shughuli kwenye vituo unavyofuatilia.
    • Video zinazopendekezwa: Hukuarifu kuhusu video ambazo huenda ukazipenda kulingana na maudhui unayotazama. Video hizi si za vituo unavyofuatilia.
    • Shughuli kwenye kituo changu: Hukuarifu kuhusu maoni na shughuli nyinginezo kwenye kituo au video zako.
    • Shughuli kwenye maoni yangu: Hukuarifu maoni yako yanapopendwa kwa mibofyo ya imenipendeza, alama za moyo au yanapobandikwa.
    • Majibu kwenye maoni yangu: Pata taarifa mtu anapojibu maoni yako.
    • Mitajo: Hukuarifu wengine wanapotaja kituo chako.
    • Maudhui yaliyoshirikiwa: Hukuarifu mara kwa mara maudhui yako yanaposhirikiwa kwenye vituo vingine.
  4. Chini ya "Arifa za barua pepe," chagua aina za arifa za barua pepe ambazo ungependa kupokea.

Tofauti kati ya Arifa na Mipasho ya Vituo Unavyofuatilia

Mipasho ya Chaneli Unazofuatilia, inayopatikana kwenye vifaa vya mkononi na kompyuta, huonyesha video zozote zilizopakiwa hivi karibuni kutoka kwenye chaneli unazofuatilia.

Arifa zinaweza kukueleza kunapokuwa na video mpya, kutuma masasisho kutoka kwa usajili wako na pia zinaweza kukuarifu kuhusu maudhui ambayo unaweza kuyapenda. Tutakutumia barua pepe, arifa zilizowekewa mapendeleo kwenye vifaa vya mkononi au arifa kwenye kikasha katika kompyuta au kifaa chako cha mkononi. Unapofuatilia chaneli, utapata kiotomatiki arifa zilizowekewa mapendeleo zinazoangazia shughuli.

Arifa kwenye kikasha hupangwa kulingana na wakati, arifa mpya zaidi zikiwa katika sehemu ya juu. Baadhi ya arifa zinaweza kuangaziwa juu ya arifa mpya zaidi katika sehemu ya "Muhimu", ambayo inaangazia arifa tunazodhani zinaweza kuwa muhimu zaidi kwako. Mifano ya arifa muhimu inaweza kujumuisha jibu kwa maoni yako au watu wanapotuma video zako.

Ili upate arifa zote kutoka kwenye chaneli unayofuatilia, gusa kengele ya Arifa  . Kisha kengele hiyo itabadilika na kuwa kengele inayolia  ili kuashiria kuwa umechagua arifa zote.

Hutapata arifa iwapo mipangilio ya chaneli imewekwa kuwa inalenga watoto. Kengele ya arifa itawekewa mipangilio ya hamna arifa . Huwezi kubadilisha mipangilio hii.

Arifa za Mmiliki wa Kituo

Ili ubadilishe mipangilio ya video mahususi ya arifa za video zinazotumwa kwa wanaofuatilia:
  1. Nenda kwenye Studio ya YouTube kisha Maudhui  kisha Video.
  2. Chagua video ambayo haijaorodheshwa kisha Maelezo kisha ONYESHA ZAIDI.
  3. Nenda chini kwenye sehemu ya Leseni.
  4. Teua au uondoe chaguo la Chapisha kwenye mipasho ya wanaofuatilia kituo na uwaarifu katika video hiyo mahususi.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
13069535482513742342
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false