Katika Maktaba ya Sauti kwenye Studio ya YouTube, unaweza kupata madoido ya sauti na muziki usiokuwa na mirabaha kwa matumizi kwenye video zako.
Fungua Maktaba ya Sauti
- Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
- Kwenye menyu ya kushoto, chagua Maktaba ya Sauti.
Unaweza pia kufikia Maktaba ya Sauti moja kwa moja kwenye youtube.com/audiolibrary.
Tafuta kwenye Maktaba ya Sauti
Tafuta muziki
Katika kichupo cha Muziki , tumia vichujio na upau wa kutafutia ili utafute nyimbo za kutumia kwenye video zako.
Ili upate wimbo fulani, weka jina, msanii ama neno muhimu la wimbo katika upau wa kutafutia. Unaweza pia kutumia vichujio kupata muziki kulingana na jina la wimbo, aina, hali, jina la msanii, maelezo na muda (urefu kwa sekunde).
Chuja matokeo yako ya utafutaji kwa kubofya kichujio cha kando ya msanii, aina au hali ya nyimbo mahususi. Unaweza kupanga matokeo yako ya utafutaji kulingana na jina la wimbo, jina la msanii, muda au tarehe kwa kubofya safu wima yao ya majina.
Hifadhi nyimbo unazopenda kwa kubofya aikoni ya nyota kando ya jina la wimbo. Ili uone orodha ya nyimbo unazopenda, bofya kichupo cha Zenye nyota.
Tafuta madoido ya sauti
Katika kichupo cha "Madoido ya sauti", tumia vichujio na upau wa kutafutia ili utafute madoido ya sauti ya kutumia kwenye video zako.
Ili upate madoido fulani ya sauti, weka neno muhimu au jina la wimbo katika upau wa kutafutia. Unaweza pia kuchuja madoido ya sauti kwa aina na muda (urefu kwa sekunde).
Cheza na upakue sauti
Ili usikilize sampuli ya wimbo, bofya Cheza . Ukipenda unachosikia, wekelea kiashiria juu ya tarehe na ubofye PAKUA ili upate faili ya MP3.
Wimbo utaendelea kucheza unapovinjari Maktaba ya Sauti. Kwa kutumia vidhibiti kwenye kicheza sauti, unaweza kusitisha, kusogeza na kucheza wimbo uliotangulia au unaofuata.
Kuweka maelezo
Ikiwa unatumia wimbo wenye leseni ya Creative Commons , ni sharti uweke maelezo kuhusu msanii anayeumiliki katika maelezo ya video yako. Ili uzalishe maelezo unayoweza kutumia:
- Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
- Kwenye menyu ya kushoto, chagua Maktaba ya Sauti.
- Pata wimbo unaotaka kutumia.
- Kumbuka: Ili uvinjari muziki wote wenye leseni ya Creative Commons, bofya upau wa kuchuja Maelezo yanahitajika.
- Katika safu wima ya "Aina ya leseni", bofya aikoni ya Creative Commons .
- Katika dirisha ibukizi, bofya "Nakili" ili unakili maandishi ya maelezo. Sasa unaweza kubandika maelezo haya katika sehemu ya maelezo ya video yako.
Ikiwa ungependa kupata muziki wenye leseni ya kawaida ya Maktaba ya Sauti ya YouTube ambao hauhitaji kuwekewa maelezo, bofya upau wa kuchuja Maelezo hayahitajiki.
Kuchuma mapato kutoka kwenye video yako
Iwapo upo kwenye Mpango wa Washirika wa YouTube, unaweza kuchuma mapato kwenye video zenye muziki na madoido ya sauti kutoka kwenye Maktaba ya Sauti.
Madoido ya sauti na muziki usiokiuka hakimiliki uliopakuliwa kwenye Maktaba ya Sauti hautadaiwa na mwenye haki kupitia mfumo wa Content ID.
Kumbuka:
- Ni madoido ya sauti na muziki kutoka kwenye Maktaba ya Sauti tu unaotambulika na YouTube kuwa maudhui yanayoweza kutumiwa bila ruhusa ya mwenye hakimiliki.
- YouTube haiwajibiki kwa matatizo yanayojitokeza kwenye madoido ya sauti na muziki ambao “hauna mirabaha” kwenye chaneli za YouTube au maktaba zingine za muziki.
- YouTube haiwezi kutoa mwongozo wa kisheria, ikiwa ni pamoja na mwongozo kuhusu matatizo ya muziki yanayotokea nje ya mfumo.
- Ikiwa una maswali kuhusu matumizi yako ya muziki, unaweza kuwasiliana na mwanasheria aliyehitimu.
Pata maelezo zaidi kuhusu aina ya maudhui unayoweza kutumia kuchuma mapato.