Pakua programu ya YouTube ili upate hali bora ya utazamaji kwenye simu yako mahiri.
Kupakua programu
Kumbuka: Unapaswa uwe unatumia Android 9.0 au toleo jipya zaidi ili uweze kupakua programu.
- Fungua Duka la Google Play kwenye kifaa chako cha mkononi.
- Tafuta "YouTube."
- Chagua programu rasmi ya YouTube.
- Gusa Weka kwenye kifaa.
Tembelea Kituo cha Usaidizi cha Google Play ili upate maelezo zaidi kuhusu kupakua programu za Android.
Kumbuka: Unaweza pia kupakua programu ya YouTube kwenye TV inayotumia intaneti, kifaa cha kutiririsha maudhui au kifaa chako cha michezo ya video.