Pakua programu ya YouTube

Ili utazame YouTube kwenye simu mahiri au kishikwambi chako, pakua programu ya YouTube. Programu ya YouTube inapatikana katika vifaa vingi tofauti, ikiwa ni pamoja na simu za mkononi, televisheni zinazoweza kuunganisha kwenye intaneti na vifaa vya kutiririsha maudhui.  Pata maelezo zaidi kuhusu mahali pa kutazama YouTube.

Jinsi ya Kuingia Kwenye YouTube katika Televisheni Yako

Unaweza kupakua programu ya YouTube kwenye Google Play.

Tembelea Kituo cha Usaidizi cha Google Play ili upate maelezo kuhusu kudhibiti vipakuliwa vya programu ya Android kutoka Google Play.

Kumbuka: Programu itafanya kazi tu kwenye simu au vishikwambi vinavyotumia toleo la 6.0 la Android na matoleo mapya zaidi. 

YouTube kwenye televisheni mpya zinazoweza kuunganisha kwenye intaneti na vifaa vya kuhifadhia data

Toleo la hivi karibuni la programu ya YouTube linapatikana kwenye miundo ya vifaa vya 2013 na miundo mipya zaidi na baadhi ya miundo ya vifaa vya 2012.

YouTube kwenye Android TV

Ikiwa una kifaa kinachotumia Android TV, programu ya YouTube itapatikana kwenye orodha ya programu zako kwa chaguomsingi.

Toleo la 1.0 la programu ya YouTube la Android TV halitumiki tena.

YouTube kwenye Apple TV

Ikiwa una Apple TV ya toleo la 4 au jipya zaidi, programu ya YouTube itapatikana kusakinishwa kutoka App Store.

Dokezo: Apple TV za toleo la tatu au awali ya hilo hazina programu ya YouTube inayotumika tena. Ikiwa unatumia mojawapo ya vifaa hivi, unaweza kutumia Airplay kwenye vifaa ili kutiririsha YouTube.

YouTube kwenye vifaa vya michezo ya video

Unaweza kupakua YouTube kutoka kwenye maduka mengi ya vifaa vya michezo ya video, kama vile Nintendo, PlayStation, Xbox.

  1. Nenda kwenye duka la kifaa chako cha michezo ya video na utafute YouTube.
  2. Chagua Pakua.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
9461391452569854933
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false