Kubadilisha upendavyo muundo wa chaneli ya YouTube

Unaweza kubadilisha muundo wa chaneli yako ya YouTube upendavyo ili watazamaji waweze kutazama kionjo cha chaneli, video inayoangaziwa, sehemu zinazoangaziwa ikiwa ni pamoja na sehemu ya "Kwa ajili yako" na "Klipu maarufu za jumuiya" wanapoingia kwenye kichupo cha Ukurasa wa kwanza wa chaneli yako.

Kutayarisha kionjo cha chaneli kwa watu ambao hawafuatilii chaneli

Kionjo cha chaneli yako huwapa kionjo cha chaneli yako ili watazamaji waweze kupata maelezo zaidi na kuifuatilia. Kwa chaguomsingi, matangazo hayataonyeshwa kwenye kionjo cha chaneli yako, isipokuwa video yako iwe ina maudhui yanayodaiwa kuwa ya wahusika wengine.
  1. Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
  2. Kwenye menyu ya kushoto, chaguaKuweka mapendeleo kisha Muundo.
  3. Chini ya Video inayoangaziwa, bofya WEKA kisha uchague video ya kionjo cha chaneli yako.
  4. Bofya Chapisha.

Video inayoangaziwa kwa wafuatiliaji wanaorudi

Unaweza kuangazia video yako au video yoyote kwenye YouTube kwa wafuatiliaji wanaorudi ili waitazame wanapotua kwenye Ukurasa wa kwanza wa chaneli yako.
  1. Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
  2. Kwenye menyu ya kushoto, chaguaKuweka mapendeleo kisha Muundo.
  3. Chini ya Video iliyoangaziwa, bofya WEKA na uchague video ya kuangazia.
  4. Bofya Chapisha.

Sehemu zinazoangaziwa

Unaweza kubadilisha upendavyo muundo wa Ukurasa wa kwanza wa kituo chako kwa kuweka hadi sehemu 12 maalum. Muundo wako utaonyesha sehemu 4 zilizojazwa kiotomatiki kwa chaguomsingi: Video fupi, Vipakiwa, Orodha za kucheza zilizoundwa na Usajili ulioweka hadharani.

Tunga sehemu

  1. Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
  2. Kwenye menyu ya kushoto, chaguaKuweka mapendeleo kisha Muundo.
  3. Katika upande wa chini, bofya WEKA SEHEMU.
  4. Sogeza ili uchague maudhui yako.
    1. Video: Chagua kuangazia video, Video Fupi na mitiririko mubashara.
    2. Orodha: Chagua kuangazia orodha moja, ulizotayarisha au nyingi.
    3. Uanachama: Chaneli ambako kipengele cha uanachama kimewashwa zinaweza kuchagua kuangazia video za wanachama pekee na zaidi.
    4. Chaneli: Chagua kuangazia chaneli unazofuatilia na zinazoangaziwa.
    5. Sehemu ya 'Kwa ajili yako': Chagua kupendekeza maudhui kwa watazamaji wako kulingana na mapendeleo yao.
    6. Sehemu ya 'Klipu maarufu za jumuiya': Chagua kuonyesha klipu maarufu za video zako kwenye kichupo cha Ukurasa wa kwanza wa chaneli yako.
  5. Bofya Chapisha.

Badilisha sehemu

  1. Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
  2. Kwenye menyu ya kushoto, chaguaKuweka mapendeleo kisha Muundo.
  3. Elea juu ya sehemu unayotaka kubadilisha na ubofye Chaguo '' kisha Badilisha maudhui ya sehemu .
  4. Katika sehemu ya kubadilisha skrini, chagua maudhui ya sehemu
  5. Bofya Chapisha.

Panga upya sehemu za kituo chako

  1. Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
  2. Kwenye menyu ya kushoto, chaguaKuweka mapendeleo kisha Muundo.
  3. Bofya upau wima kwenye sehemu unayotaka kusogeza, kisha uburute na udondoshe ili upange upya.
  4. Bofya Chapisha.

Sehemu ya "Kwa ajili yako"

Sehemu ya "Kwa ajili yako" huipatia hadhira yako hali ya utumiaji inayoifaa inapotembelea kichupo cha Ukurasa wa kwanza wa kituo chako. Sehemu hii huonyesha mseto wa maudhui yaliyowekewa mapendeleo kulingana na yaliyotazamwa na mtazamaji binafsi. Unaweza kuchagua aina za maudhui ya kuonyesha na kuchagua kuonyesha tu maudhui yaliyochapishwa ndani ya miezi 12 iliyopita.

Kudhibiti sehemu ya "Kwa ajili yako"

Studio ya YouTube

  1. Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
  2. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Kubadilisha upendavyo kisha Muundo.
    • Ili uweke sehemu, nenda chini na ubofye WEKA SEHEMU, karibu na "Sehemu zinazoangaziwa" kisha Chagua Kwa ajili yako.
    • Ili uondoe sehemu, bofya menyu ya vitone vitatu '' kwenye rafu ya "Kwa ajili yako" kisha uchague sehemu ya Ondoa.

Programu ya Studio ya YouTube

  1. Fungua programu ya Studio ya YouTube .
  2. Gusa picha yako ya wasifu  kisha Badilisha chaneli .
  3. Washa au uzime sehemu ya "Kwa ajili yako".

Kubadilisha sehemu ya "Kwa ajili yako"

Studio ya YouTube

  1. Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
  2. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Kubadilisha upendavyo  kisha Muundo.
  3. Nenda chini kwenye sehemu ya “Mapendekezo kwa watazamaji wako” kisha ubofye Mipangilio zaidi.
  4. Chagua aina ya maudhui utakayoonyesha na ikiwa ungependa kuonyesha tu machapisho ya miezi 12 iliyopita.
  5. Bofya Nimemaliza.
  6. Bofya Chapisha.

Programu ya Studio ya YouTube

  1. Fungua programu ya Studio ya YouTube .
  2. Gusa picha yako ya wasifu  kisha Badilisha chaneli .
  3. Chini ya sehemu ya "Kwa ajili yako", gusa Mipangilio Zaidi.
  4. Chagua aina ya maudhui ambayo ungependa kuonyesha. Unaweza kuchagua kuonyesha maudhui yako yote au maudhui yaliyochapishwa ndani ya miezi 12 iliyopita.
  5. Gusa Hifadhi.

Sehemu ya "Klipu maarufu za jumuiya"

Unaweza kuonyesha klipu maarufu za video zako kwenye kichupo cha Ukurasa wa kwanza wa chaneli yako. Klipu hizi zinaweza kutayarishwa na wewe au watazamaji wako. Ukishaziweka kwenye kichupo chako cha Ukurasa wa kwanza, klipu hizo huonekana kwa umma na hupangwa kulingana na umaarufu na jinsi zilivyopakiwa hivi majuzi. Pata maelezo kuhusu jinsi ya kudhibiti sehemu ya "Klipu maarufu za jumuiya".

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
6610155641490225849
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false