Matangazo yanayocheza kwenye Video za YouTube au Video Fupi unazotazama yamewekewa mapendeleo yako. Yanatokana na Mipangilio ya Matangazo ya Google, maudhui uliyotazama na iwapo umeingia katika akaunti au la.
How to personalize the ads you see on YouTube and Google
Fuatilia Chaneli ya Watazamaji wa YouTube ili upate habari, taarifa na vidokezo vipya.
Unapokuwa umeingia katika akaunti, ishara hizi zisizokutambulisha zinaweza kuamua matangazo utakayoona:
- Aina ya video ulizotazama
- Programu zilizo kwenye kifaa chako na matumizi yako ya programu
- Tovuti unazotembelea
- Vitambulishi vinavyoficha utambulisho wa data vinavyohusishwa na kifaa chako cha mkononi
- Matumizi ya awali ya matangazo au huduma za utangazaji za Google
- Eneo lako la kijiografia
- Rika
- Jinsia
- Matumizi ya video za YouTube
Matangazo haya yanalingana na maudhui ya video ulizotazama iwe umeingia katika akaunti au la.
Dhibiti mipangilio ya faragha ya matangazo
Unaweza kudhibiti matangazo ambayo unaonyeshwa kulingana na Mipangilio ya Matangazo ya Akaunti yako ya Google. Unaweza pia kuona, kufuta au kusimamisha Historia ya Video Ulizotazama kwenye YouTube.
Zima matangazo
Ikiwa ungependa kuzima matangazo kwenye YouTube, angalia uanachama wetu unaolipiwa kwa ajili ya matumizi bila matangazo.
Ili uache kuona tangazo mahususi bila kuliripoti, chagua Zaidi au Maelezo Zuia tangazo kwenye tangazo. Chaguo hili linapatikana tu ukiamua kuwekea mapendeleo matangazo unayoona kwenye Kituo Changu cha Matangazo.
Kuripoti tangazo
Ukiona tangazo usilopenda, tumia maelezo yaliyo hapo juu kudhibiti mipangilio yako ya matangazo. Ukiona tangazo ambalo halifai au linakiuka sera za matangazo ya Google, unaweza kuliripoti.
Ili uripoti tangazo, chagua Zaidi au Maelezo Ripoti tangazo au uchague kujaza na kutuma fomu hii. Timu yetu itakagua ripoti yako ya tangazo na itachukua hatua panapofaa.
Kipengele cha kuripoti matangazo kinapatikana tu kwenye programu ya YouTube ya vifaa vya mkononi na kwenye kompyuta.
Jaza fomu za kupata wateja
Unapofungua fomu ya kupata wateja katika kampeni ya video kwenye YouTube, baadhi ya sehemu hujazwa kiotomatiki unapokuwa umeingia katika AKaunti yako ya Google.