Kubadili kati ya chaneli kwenye Akaunti ya Google

Unaweza kudhibiti hadi chaneli 100 kwenye Akaunti moja ya Google. Pata maelezo kuhusu jinsi ya kutumia Akaunti za Biashara ili udhibiti chaneli zako za YouTube.

Badili kati ya chaneli

Kwenye YouTube, unaweza kutumia chaneli moja kwa wakati mmoja. Tumia maagizo yaliyo hapo chini ili ubadili kati ya chaneli za YouTube ulizounganisha kwenye Akaunti moja ya Google.

Fuatilia chaneli ya Watazamaji ya YouTube ili upate habari, taarifa na vidokezo vipya.

Unapoingia katika akaunti kwenye YouTube kwenye kifaa cha mkononi, utadokezwa uchague chaneli unayotaka kutumia

Ili ubadili utumie chaneli tofauti unayodhibiti:

Programu ya YouTube ya Android

  1. Fungua programu ya YouTube .
  2. Nenda kwenye picha yako ya wasifu .
  3. Katika sehemu ya juu, gusa Badilisha akaunti .
  4. Gusa chaneli kwenye orodha ili uanze kutumia akaunti hiyo.

Programu ya Studio ya YouTube kwenye Android

  1. Fungua programu ya Studio ya YouTube .
  2. Katika sehemu ya juu kulia, gusa wasifu wako .
  3. Katika sehemu ya juu, gusa Badilisha akaunti .
  4. Chagua chaneli ambayo ungependa kuitumia.

Badili akaunti kwa urahisi kwenye kifaa cha mkononi

Unaweza kuangalia Akaunti yako wakati wowote ili uthibitishe chaneli unayotumia.

Nina ruhusa ya kufikia chaneli, lakini haionekani kwenye orodha

Ikiwa chaneli yako haionekani, nenda kwenye studio.youtube.com ili ubadilishe chaneli.

Nina chaneli iliyounganishwa na Akaunti ya Biashara, lakini haionekani kwenye orodha

Iwapo chaneli yako haionekani, Akaunti ya Google ambayo umeingia kwa sasa haijaorodheshwa kama mdhibiti wa Akaunti ya Biashara ya chaneli hiyo.

Ili urekebishe tatizo: Fuata maagizo haya ili uweke Akaunti yako ya Google kama mdhibiti wa Akaunti ya Biashara iliyounganishwa kwenye chaneli hiyo.

Ikiwa ungependa kuondoa chaneli kwenye orodha hii

Kumbuka: Ukiona chaguo ambalo linaonyesha anwani yako ya barua pepe badala ya jina, hali hii hukuruhusu utumie YouTube kama mtazamaji bila chaneli. Huwezi kuliondoa, lakini unaweza kutumia chaguo hilo kufungua chaneli mpya ambayo itatumia jina ulilochagua la akaunti yako ya Google.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Programu za Google
Menyu kuu