Kutazama YouTube kwenye PlayStation

Sasa unaweza kutazama video za YouTube kwenye PlayStation. Katika programu ya YouTube unaweza kuangalia vituo unavyofuatilia, na kutafuta maudhui katika programu ya YouTube. Pata maelezo kuhusu jinsi ya kutumia simu, kompyuta kibao au kompyuta yako kama kidhibiti cha mbali.

Pakua programu ya YouTube

Unganisha akaunti yako ya Google kwenye akaunti yako ya PlayStation

Unaweza kuunganisha akaunti zako za Google na PlayStation ili kuonyesha na kushiriki uchezaji kutoka kwa dashibodi yako kwenda kwenye YouTube.

Pata maelezo kuhusu jinsi ya kuingia katika akaunti yako ya PlayStation. Ikiwa huwezi tena kufikia kifaa, unaweza pia kubadilisha akaunti au kuondoka kwenye akaunti.

Kumbuka: Hutaweza kuingia katika akaunti yako ya YouTube kwa kuunganisha Akaunti yako ya Google na akaunti yako ya PlayStation. Utahitaji kuingia katika akaunti kwenye programu ya YouTube.
Vidhibiti vya video
Baada ya kuchagua video ya kucheza, upau wa vidhibiti vya kichezaji utafunguka utakaokuruhusu kufanya yafuatayo:
  • Kusimamisha/kuendelea : Bonyeza X kwenye kidhibiti chako cha mbali chenye upau wa shughuli za video inayolengwa ili usimamishe au uendelee kucheza video.
  • Kusogeza mbele : Bofya kulia kwenye kidhibiti ukiwa umechagua upau wa shughuli ya video ili usogeze mbele kwenye video.
  • Kusogeza nyuma Bonyeza kushoto kwenye kidhibiti ukiwa umechagua upau wa shughuli za video ili usogeze nyuma kwenye video.
  • Kuweka Manukuu : Iwapo video ina manukuu, chagua ili uwashe na kuzima manukuu ya video na kubadilisha mipangilio ya kuonyesha manukuu.
  • Kuripoti : Ripoti video iwapo ina maudhui yasiyofaa.

Unapocheza video, unaweza kupata chaguo zaidi kwa kuchagua Vitendo Zaidi. Hapo utaona:

  • Kufuatilia kituo.
  • Kukadiria video.
  • Kuripoti video kwa kukiuka Mwongozo wa Jumuiya.
Kumbuka: Video zinaweza kuchezwa kwa hadi 4K kwa fremu 60 kwa sekunde.

Kutafuta Video

Unaweza kutafuta video katika programu ya YouTube kwa kutumia kipengele cha Kutafuta kwa Kutamka. Huu ndio utaratibu:

  1. Unganisha maikrofoni kwenye kidhibiti chako cha DualShock® (au uunganishe Kamera ya PlayStation® iliyo na maikrofoni iliyojumuishwa ndani yake).
  2. Fungua programu ya YouTube na uende kwenye ukurasa wa Utafutaji.
  3. Chagua Maikrofoni upande wa kushoto wa kibodi ya skrini (au kwa njia ya mkato, bonyeza L2 L2 ya njia ya mkato ya kufikia Maikrofoni kwenye kidhibiti chako).
  4. Zungumza kwenye maikrofoni na useme unachotafuta.
  5. Matokeo yako yataibuka.

Kutazama video inayozunguka kwa digrii 360

Unaweza kutazama video za mwonekano wa digrii 360 kwenye PlayStation toleo la 4 au 5. Unapotazama video zinazozunguka kwa digrii 360, usukani wa kushoto na kulia kwenye kidhibiti kilichoambatishwa unaweza kutumiwa kugeuza video.

Kuoanisha kifaa cha pili kwenye PlayStation yako

Unaweza kutumia simu, kompyuta kibao au kompyuta yako kama kidhibiti cha mbali. Pata maelezo kuhusu jinsi ya kutenganisha PlayStation yako kupitia tovuti au programu ya YouTube ya vifaa vya mkononi.

Kupakia video

Unaweza kupakia video za michezo ya video moja kwa moja kwenye YouTube kwa kutumia kitufe cha Shiriki kwenye PlayStation yako. Huu ndio utaratibu:

  1. Bonyeza kitufe cha Shiriki kwenye kidhibiti chako cha PS4 kisha uchague Pakia Klipu ya Video.
  2. Chagua klipu ambayo ungependa kupakia kisha uchague YouTube.
  3. Punguza sehemu ya mwanzo au mwisho, weka mada, maelezo na lebo.
  4. Thibitisha mipangilio ya faragha na kuwa unapakia kwenye kituo sahihi.
  5. Chagua Shiriki.

Sasa klipu itaanza kupakiwa. Unaweza kufuatilia upakiaji wako kwa kutembelea Ukurasa wa arifa wa PS4 au PS5 yako.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
16341086582287256142
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false