Kipengee ni nini?
Katika mfumo wa kudhibiti haki kwenye YouTube, kipengee ni mkusanyiko wa maelezo kuhusu kipande cha mali ya uvumbuzi. Wenye hakimiliki huweka vipengee kwenye Kidhibiti Maudhui cha Studio ya YouTube ili waweze kudhibiti maudhui yao yaliyo na hakimiliki kwenye YouTube.
Vipengee si video za YouTube. Vipengee huunganishwa na video za YouTube zinapodaiwa. Video zilizopakiwa na wenye hakimiliki zinaweza kudaiwa au video za watumiaji wengine zinaweza kudaiwa zinapopatikana na maudhui yanayolingana na kipengee cha mwenye hakimiliki.
Sehemu za kipengee
Kipengee kina sehemu zifuatazo:
- Faili ya marejeleo: Maudhui halisi yaliyo na hakimiliki, kama vile video ya muziki.
- Metadata: Maelezo kuhusu maudhui yaliyo na hakimiliki, kama vile jina.
- Maelezo ya umiliki: Maelezo kuhusu maeneo unakomiliki haki za maudhui na kiwango cha maudhui unachomiliki.
- Sera: Maagizo yanayoelezea YouTube hatua za kuchukua maudhui yanayolingana na yako yanapopatikana.
Kuweka kipengee
Ni lazima uweke kipengee ili zana zetu za kudhibiti haki ziweze kupata na kushughulikia maudhui yanayolingana na yako. Kuna njia kadhaa za kuweka kipengee:
- Wakati wa kupakia video au kwa kuweka sera ya kupakia
- Kutumia Zana ya Kutumia Unapodai Mwenyewe
- Kutumia Kipakiaji cha vifurushi cha YouTube
- Kutumia mbinu ya kupakia video nyingi, kama vile DDEX au SFTP
- Kutumia API za YouTube
Aina za vipengee
Unapoweka kipengee, utaombwa kuchagua aina ya kipengee hicho. Kuna aina kadhaa tofauti za vipengee:
Aina ya kipengee | Maelezo | Mfano wa metadata |
---|---|---|
Rekodi ya Sauti | Rekodi ya sauti. |
|
Faili yenye Maelezo ya Umiliki wa Utungo | Mgawo wa umiliki wa utungo wa muziki. |
|
Video ya Muziki | Maudhui ya muziki yenye sauti na video. Kwa kawaida hutolewa na studio ya kurekodia muziki. |
|
Video ya Picha | Video iliyo na rekodi ya sauti na picha tuli. Video za picha hutumiwa kwenye nyimbo zisizo na video halisi za muziki. |
|
Filamu | Filamu yenye urefu kamili. |
|
Kipindi cha televisheni | Kipindi kutoka kwenye onyesho la televisheni. |
|
Wavuti | Aina nyingine yoyote ya maudhui ya video ambayo haipo kwenye aina nyingine za vipengee. |
|
Kwa nini aina ya kipengee ni muhimu?
Ni muhimu kuchagua aina sahihi ya kipengee kwa sababu kadhaa:
- Aina tofauti za vipengee zina chaguo tofauti za metadata
- Aina ya kipengee haiwezi kubadilishwa kwa urahisi
- Kwa kutegemea mkataba wako na YouTube, aina ya kipengee inaweza kubainisha iwapo unaweza kuchuma mapato kutokana na video unazodai au la.
Ikiwa huna uhakika wa aina unayopaswa kutumia, wasiliana na msimamizi wako wa washirika au timu ya usaidizi ya YouTube ili upate usaidizi. Unaweza pia kuangalia mbinu bora za vipengee.
Vipengee vilivyopachikwa
Mara nyingi waandashi, wasanii na kampuni nyingi tofauti huhusika katika utayarishaji wa wimbo au video ya muziki. Ili kuwakilisha umiliki wao wa pamoja kwa usahihi, baadhi ya vipengee vya muziki vinaweza kupachikwa ndani ya vingine.
Composition Share asset | Sound Recording asset | Music Video asset | ||
Composition Share assets represent the rights of the song writers. One or more Composition Share assets can be embedded in a Sound Recording asset. |
Sound Recording assets represent the rights of the song producer and performer. One Sound Recording asset can be embedded in a Music Video asset. |
Music Video assets represent the rights of the music video producer. |
Rekodi za sauti zilizo na wamiliki wengi tofauti zinaweza pia kutumia vipengele katika rekodi za sauti ili kuwakilisha maelezo kamili ya umiliki.