Kutumia Zana ya Uthibitishaji wa Maudhui

Kumbuka: Iwapo bado huna akaunti ya Mpango wa Kuthibitisha Maudhui (CVP), unaweza kukagua ustahiki wako kwa kujaza fomu hii.

Zana ya Kuthibitisha Maudhui inapatikana katika Kidhibiti Maudhui cha Studio ya YouTube. Ili ufikie, hakikisha kuwa umeingia katika akaunti yako ya Kidhibiti Maudhui.

Zana hii inakuruhusu utumie fomu yetu ya mtandaoni ya biashara, inayofanana na fomu yetu ya wavuti ya maombi ya kuondoa video kwa kukiuka hakimiliki, lakini inajumuisha kipengele cha kutafuta video za umma za YouTube kwa maudhui ambayo una hakimiliki. Ukipata video zinazolingana na maudhui yako, unaweza kutuma maombi ya kuondoa video kwa kukiuka hakimiliki moja kwa moja kupitia fomu ya mtandaoni ya biashara.

Kutafuta video zinazolingana na maudhui yako

Ili utafute video zinazolingana na maudhui yako kwa kutumia Zana ya Kuthibitisha Maudhui:

  1. Ingia katika akaunti ya Kidhibiti Maudhui cha Studio.
  2. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Kudai mwenyewe .
  3. Katika upau wa kuchuja , weka maneno muhimu, vitambulisho vya video, au uchague kichujio cha kisha TUMIA.
    • Tumia ishara ya kuondoa "-" ili utenge maneno muhimu kwenye utafutaji wako.
    • Unaweza pia kutafuta ukitumia @username au kitambulisho cha chaneli ili upate video kutoka kwa mtu mahususi aliyepakia.
    • Unaweza kuchagua kutoka kwenye vichujio hivi:
      • Orodha ya zilizoruhusiwa (iwe video ipo au haipo kwenye orodha ya zilizoruhusiwa)
      • Kitambulisho cha Kituo
      • Hali ya dai (iwe ni dai lako au la wengine au si dai lako au la wengine)
      • Mtiririko mubashara (iwe video ni mtiririko mubashara au si mtiririko mubashara)
      • Tarehe ya kuchapishwa
      • Limekaguliwa (iwapo dai limekaguliwa)
      • Urefu wa video (chini ya dakika 4, dakika 4 hadi 20, au zaidi ya dakika 20)
  4. (Si lazima) Katika orodha ya matokeo ya utafutaji, unaweza kubofya Panga kulingana na  ili upange matokeo kulingana na Ufaafu, Tarehe ya kuchapishwa, au Jumla ya mara za kutazamwa.
Kidokezo: Ili uone matokeo zaidi kwenye ukurasa mmoja, bofya nambari karibu na Safu mlalo kwa kila ukurasa ili uibadilishe kutoka 30 (chaguomsingi) hadi 10, 50, au 100.
Kutuma maombi ya kuondoa video kwa kukiuka hakimiliki

Kabla ya kutuma ombi la kuondoa video, hakikisha unafahamu taarifa binafsi zinazokuwa sehemu ya ombi la kuondoa video kwa kukiuka hakimiliki.

Kutuma ombi la kuondoa video

Ili utume ombi la kuondoa video moja:

  1. Kwenye ukurasa wa Kudai mwenyewe , bofya safu mlalo ya video ili uipanue.
  2. Bofya kichupo cha Kuondoa katika sehemu ya juu ya safu mlalo.
  3. Bofya CHAGUA KIPENGEE.
  4. Kwa kutumia vichupo katika sehemu ya juu, unaweza kuteua Chagua kipengee ili uteue kipengee kilichopo au Buni kipengee ili ubuni kipengee kipya. Pata maelezo kuhusu jinsi ya kubuni vipengee.
  5. Iwapo unachagua kipengee kilichopo, bofya CHAGUA. Iwapo unabuni kipengee kipya, bofya BUNI.
  6. Katika kisanduku cha Sahihi, weka jina lako la kwanza na la mwisho (si jina la kampuni).
  7. Chini ya sehemu ya Kukubali, soma taarifa, kisha ubofye kisanduku cha kuteua ili ukubali taarifa.
  8. Bofya ONDOA.

Kutuma maombi ya kuondoa video nyingi

Unaweza kutuma maombi ya kuondoa video nyingi kwa kukiuka hakimiliki. Ili uombe kuondolewa kwa zaidi ya video moja inayohusiana na kipengee kimoja:

  1. Kwenye ukurasa wa Kudai mwenyewe , bofya visanduku vya kuteua karibu na video ambazo ungependa kutuma maombi ya kuziondoa.
    • Unaweza kuchagua hadi video 100 mara moja. Ili ufanye hivyo, katika sehemu ya chini ya ukurasa, hakikisha Safu mlalo kwa kila ukurasa zimewekwa kuwa 100, kisha bofya kisanduku cha kuteua juu ya matokeo ya utafutaji.
  2. Katika sehemu ya juu ya ukurasa, bofya ONDOA.
  3. Bofya CHAGUA KIPENGEE.
  4. Kwa kutumia vichupo katika sehemu ya juu, unaweza kuteua Chagua kipengee ili uteue kipengee kilichopo au Buni kipengee ili ubuni kipengee kipya. Pata maelezo kuhusu jinsi ya kubuni vipengee.
  5. Iwapo unachagua kipengee kilichopo, bofya CHAGUA. Iwapo unabuni kipengee kipya, bofya BUNI.
  6. Katika kisanduku cha Sahihi, weka jina lako la kwanza na la mwisho (si jina la kampuni).
  7. Chini ya sehemu ya Kukubali, soma taarifa, kisha ubofye kisanduku cha kuteua ili ukubali taarifa.
  8. Bofya TUMA.
Kufuta au kughairi maombi ya kuondoa video kwa kukiuka hakimiliki

Iwapo ombi la kuondoa video limesuluhishwa na limesababisha kuondolewa kwa maudhui, linaweza kufutwa. Iwapo ombi la kuondoa video bado halijasuluhishwa (kwa mfano, kuchelewesha kuondoa na uondoaji unaokaguliwa), linaweza kughairiwa.

Ili ufute au ughairi ombi la kuondoa video kwa kukiuka hakimiliki, ambalo lilitumwa kupitia Zana ya Kuthibitisha Maudhui:

  1. Ingia katika akaunti ya Kidhibiti Maudhui cha Studio.
  2. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Video Unazodai .
  3. Tafuta video kutoka kwenye ombi lako halisi la kuondoa.
    • Ili upate video haraka zaidi, bofya upau wa kuchuja  kisha Hali ya dai kisha Uondoaji, Chelewesha kuondoa, au Ombi la uondoaji linakaguliwa.
  4. Bofya mada ya video.
  5. Katika sehemu ya Madai kwenye video, karibu na Uondoaji, Chelewesha kuondoa au Ombi la uondoaji linakaguliwa, bofya MAELEZO.
  6. Kwa maombi ya uondoaji ambayo bado hayajasuluhishwa (chelewesha kuondoa na uondoaji unakaguliwa), bofya GHAIRI OMBI 1 LA KUONDOA. Kwa maombi ya uondoaji ambayo yamesuluhishwa, bofya FUTA OMBI 1 LA KUONDOA.
 

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
4150701418730738540
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false