Jinsi vipimo vya matukio ya kushiriki huhesabiwa

Vipimo vya matukio ya kushiriki kwenye YouTube (utazamaji, kupenda, kutopenda na wanaofuatilia) vinaonyesha ni mara ngapi kumekuwa na matukio ya kushiriki video yako ya YouTube au kituo chako. Vipimo hivi vinaweza kuwa muhimu katika kukadiria umaarufu wa jumla wa video au kituo chako.

Tunataka kuhakikisha kwamba vipimo vyako ni vya ubora wa juu na vinatoka kwa binadamu halisi na si programu za kompyuta. Mifumo yetu huchukua muda fulani kutambua utazamaji, kupenda, kutopenda na ufuatiliaji ambao ni halali.

Kumbuka: Huenda ikachukua muda kabla ya vipimo vyako kuonekana kwenye mfumo wetu katika saa chache za kwanza baada ya kuchapisha video yako.

Mabadiliko kwenye vipimo

Baada ya matukio halali ya kushiriki kuhesabiwa, idadi ya vipimo vyako inapaswa kusasishwa mara kwa mara. Muda wa kufanya mabadiliko haya hutofautiana kwa kutegemea umaarufu na utazamaji wa video au kituo. Kumbuka kwamba tunaendelea kuthibitisha na kurekebisha matukio ya kushiriki kila mara.

Kwenye baadhi ya video na vituo, huenda idadi ya vipimo vyako ikaonekana ndogo au isionekane kwenye vipimo unavyovitarajia. Vipimo huthibitishwa kialgoriti ili kudumisha matumizi ya haki na chanya kwa watayarishi wa maudhui, watangazaji na watazamaji. Ili ithibitishe kwamba vipimo ni sahihi, YouTube inaweza kupunguza kasi, kufanya visisonge au kubadilisha idadi ya vipimo vyako kwa muda na kuondoa matukio ya ubora wa chini wa kucheza video.

Kumbuka: Kutumia vifaa kadhaa kutazama video moja na kutiririsha video moja kwenye madirisha na vichupo kadhaa ni mifano ya matukio ya ubora wa chini wa kucheza video.

Utazamaji katika utangazaji wa kulipiwa

Ikiwa video yako inatumika kama tangazo kwenye YouTube, tunaweza kuhesabu utazamaji wa tangazo kama utazamaji wa video yako. Utazamaji huu katika utangazaji unaolipiwa unahesabiwa kama utazamaji kwa sababu unaashiria kwamba mtazamaji alitazama video.

  • Matangazo ya ndani ya mtiririko yanayoweza kurukwa: Utazamaji katika utangazaji unaolipiwa utahesabiwa kama utazamaji wakati:
    • Mtu ametazama tangazo zima ambalo ni la urefu wa sekunde 11–30
    • Mtu ametazama angalau sekunde 30 ya tangazo ambalo ni la urefu wa zaidi ya sekunde 30
    • Mtu ameshiriki katika tukio la kuhusisha tangazo
  • Matangazo ya video ya ndani ya mipasho: Utazamaji katika utangazaji unaolipiwa utahesabiwa kama utazamaji wakati mtu amebofya tangazo na video ikaanza kucheza

Angalia utazamaji ukitumia Takwimu za YouTube

Ikiwa unaangalia video ambayo ulipakia, unaweza kufuatilia utazamaji wako kwa kina zaidi ukitumia Takwimu za YouTube. Kumbuka kwamba Shughuli ya muda halisi inaonyesha tu makadirio ya shughuli inayoweza kuwa ya utazamaji. Huenda isilingane na idadi unayoiona kwenye ukurasa wa kutazama.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
16440300589321017716
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false