Vidokezo vya kutiririsha

Intro To Live Streaming on YouTube

Vidokezo vya mtandao

  • Jumla ya kasi ya biti unayotiririsha haiwezi kuzidi kiasi cha kipimo data cha upakiaji kinachopatikana. Acha nafasi kiasi (tunapendekeza asilimia 20).
  • Huenda ofisi yako ikawa na muunganisho wa kasi ya juu, lakini ikiwa watu wengi wanatumia mtandao huo, muunganisho wako unaweza kuwa hafifu.
  • Pima kasi ya mtandao. Kipimo data cha kupakua (kasi ya upakuaji) mara nyingi ni kubwa kuliko cha kupakia (kupakia). Hakikisha kuwa muunganisho wako unapopakia unatosha kutuma kasi ya biti yako ya kutiririsha. Tunapendekeza Msingi + Akiba + asilimia 20.
  • Hakikisha kuwa unatumia mtando unaoaminika. Muunganisho wako ukikatika itamaanisha mtiririko wako utakatika.
Vidokezo vya usimbaji
  • Weka mipangilio ya programu ya kusimba katika mtiririko mubashara angalau saa 2 kabla ya mtiririko kuanza.
  • Anzisha programu za kusimba angalau dakika 15 kabla ya tukio kuanza.
  • Kabla ya kubofya Anza Kutiririsha, angalia onyesho la kukagua kwenye Ukurasa wa kudhibiti utiririshaji wa moja kwa moja.
  • Kwa jaribio la programu ya kusimba ambalo halikufanikiwa, simamisha programu kuu ya kusimba (au uchomoe kebo yake ya Ethaneti) na uhakikishe kuwa kichezaji kinafikia programu mbadala ya kusimba.
  • Thibitisha uadilifu wa faili zote za kumbukumbu zilizo kwenye kifaa. Hakikisha kuwa ukubwa wa faili ya kumbukumbu iliyopo kwenye kifaa unaongezeka.
  • Thibitisha kuwa tukio linaweza kufikiwa kupitia chaneli na kurasa za kutazama.
  • Thibitisha kuwa tukio linaweza kufikiwa kupitia vifaa vya mkononi.
  • Fuatilia mitiririko kila mara ili uone ubora wa sauti na video.
  • Baada ya tukio lako kukamilika kwenye YouTube, simamisha programu ya kusimba.
Kutumia kamera ya wavuti
  • Unaweza kutiririsha ukitumia kompyuta ya kupakata na kamera ya wavuti, lakini ukitumia vifaa bora, utapata matokeo bora ya mtiririko mubashara.
  • Unaweza kutumia programu ya usimbaji kama vile Wirecast au www.youtube.com/webcam.
  • Kwa matukio ya utayarishaji yaliyo na idadi kubwa ya mitiririko, tunapendekeza utumie programu za maunzi za kusimba zilizo na kiwango cha kitaalamu.
  • Hakikisha kuwa umeifanyia mipangilio yako jaribio la kutosha kabla ya tukio.
Kudumisha usalama katika mitiririko mubashara
  • Maudhui: Fahamu aina za video za kutiririsha. Unaporekodi video za marafiki, watu mnaosoma nao au vijana, kumbuka kwamba video hizo hazipaswi kuwa za kuchochea ngono, za vurugu au hatari. Kumbuka kuwa kanuni hii pia inatumika kwa gumzo la moja kwa moja. Pata maelezo zaidi kuhusu Mwongozo wetu wa Jumuiya.
  • Taarifa binafsi: Kuwa makini kuhusu kushiriki taarifa yoyote binafsi unapotiririsha mubashara na katika Gumzo la Moja kwa Moja. Ufikiaji wa msimamizi wa chaneli yako unapaswa kupewa tu kwa wale unaowaamini. YouTube haitakuomba idhini za udhibiti katika mtiririko wako.
  • Udhibiti: Ripoti video zisiozofaa au uzuie watumiaji wanaokufanya wewe au wengine kutohisi vyema wasishiriki kwenye gumzo. Pata maelezo zaidi kuhusu kudhibiti gumzo la moja kwa moja.
  • Faragha: YouTube ina vipengele vya kukusaidia kudhibiti wanaoweza kuona mitiririko mubashara unayochapisha. Linda faragha yako kwa kuweka mitiririko mubashara ya kibinafsi iwe "ya faragha" au "haijaorodheshwa." Tumia ukurasa wa Mipangilio ya faragha na usalama ili uone zana zinazoweza kukusaidia kudhibiti utumiaji wako kwenye tovuti.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
2489341535409101046
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false