Kutatua masuala ya Mtiririko mubashara

Ikiwa unakabiliwa na hitilafu za Mtiririko wako mubashara kwenye YouTube, tumia vidokezo vya utatuzi vilivyo hapa chini. 

Unapata hitilafu ya kuanzisha programu yako ya kusimba

Ikiwa unatumia programu ya kusimba ya mhusika mwingine 

Ili uirekebishe, pata ufunguo mpya wa mtiririko katika Ukurasa wa kudhibiti utiririshaji wa moja kwa moja kisha usasishe programu yako ya kusimba.

  1. Nenda kwenye Studio ya YouTube.
  2. Ili ufungue Ukurasa wa kudhibiti utiririshaji wa moja kwa moja, kwenye upande wa juu kulia, bofya Tayarisha and then Tiririsha mubashara.
  3. Kwenye upande wa kushoto, Tiririsha.
  4. Ikiwa huu ni mtiririko wako mubashara wa kwanza katika Ukurasa wa kudhibiti utiririshaji wa moja kwa moja: Hariri mtiririko wako kisha ubofye Tayarisha mtiririko.
  5. Kwenye upande wa chini kulia, nakili ufunguo mpya wa mtiririko, na uubandike katika programu yako ya kusimba.
  6. Ukiwa tayari kutiririsha, anzisha programu yako ya kusimba ili utiririshe mubashara. 

Ikiwa unaingia kwenye akaunti ya YouTube ukitumia programu ya kutiririsha iliyoundwa na wahusika wengine na hutumii ufunguo wa mtiririko

Wasiliana na timu ya usaidizi ya programu hiyo kwa maelezo zaidi. Huenda wakahitaji kusasisha programu yao ili ifanye kazi na YouTube Moja kwa Moja.

Kagua hitilafu zilizoripotiwa kwenye mtiririko wako

Hitilafu za kutiririsha mubashara zinaweza kutofautiana kulingana na idadi ya watazamaji wanaoripoti hitilafu katika mtiririko wako mubashara. Unaweza kuangalia idadi ya watazamaji na idadi ya hitilafu zilizoripotiwa katika vipimo vya mtiririko wako mubashara.

Mtazamaji mmoja anaripoti hitilafu
  • Huenda kuna hitilafu kwenye kompyuta au muunganisho wa intaneti wa mtazamaji huyu.
  • Unaweza kumpendekezea ajaribu kutazama au kuunganisha kwenye mtiririko wako kwa njia tofauti.
  • Mwombe mtazamaji hatua anazofuata ili kuona hitilafu na ukague ili uone iwapo utaiona pia.
Watazamaji wengi - wanaotumia muunganisho mmoja wa intaneti - wanaripoti hitilafu
  • Huenda kuna hitilafu katika mtandao unaoshirikiwa wa watazamaji
  • Unaweza kuwaomba watazamaji wakague hali ya muunganisho wa intaneti na mtandao wao. Wanapaswa kuwa na uwezo wa kutazama mitiririko michache - kwa mfano, watumiaji 10 wanaotazama mitiririko 10 wanahitaji mara 10 ya kasi ya mtandao wa kupakua.
  • Mwombe mtazamaji hatua anazofuata ili kuona hitilafu na ukague ili uone iwapo utaiona pia.
Watazamaji wengi - kwenye miunganisho tofauti ya intaneti - wanaripoti hitilafu
Huenda ikawa kuna hitilafu katika programu yako ya kusimba mtiririko mubashara. Hatua zaidi za utatuzi zipo hapa chini.

Hakikisha kuwa programu yako ya kusimba mtiririko mubashara inafanya kazi

Programu ya kusimba mtiririko mubashara ni programu au zana inayorekodi na kubana mtiririko wako mubashara. Unaweza kutumia hatua zilizo hapa chini kutatua baadhi ya hitilafu zinazoweza kujitokeza kwenye programu yako ya kusimba.

  1. Hakikisha kuwa unatumia toleo jipya zaidi la programu yako ya kusimba. Vinginevyo, sasisha programu yako ya kusimba upate toleo jipya zaidi.
  2. Kagua mwonekano na sauti ya mtiririko wako moja kwa moja kwenye programu ya kusimba.
    • Ikiwa sauti ya mtiririko wako si nzuri: Huenda kukawa na hitilafu kwenye ubora wa sauti na vyanzo vya video vilivyounganishwa kwenye programu yako ya kusimba. Unaweza kutafuta hitilafu za programu ya kusimba kwenye dashibodi ya moja kwa moja na ukague shughuli ya CPU kwenye programu yako ya kusimba. Au, jaribu kutafuta hitilafu za sauti au video katika faili ya kumbukumbu kwenye kifaa chako. Ikiwa huoni hitilafu zozote, tunapendekeza ujaribu kutiririsha ukitumia programu tofauti ya kusimba.
    • Ikiwa mwonekano na sauti ya mtiririko wako ni nzuri: Huenda kukawa na hitilafu katika muunganisho wako wa intaneti wa kupakia. Jaribu hatua inayofuata hapa chini.
  3. Fanya jaribio la uthabiti wa muunganisho wa intaneti yako wa kupakia.
    • Fanya jaribio la muunganisho wa intaneti yako: Tembelea Jaribio la Kasiili ujaribu kasi ya muunganisho wa intaneti yako.
    • Ukipata hitilafu katika muunganisho wa intaneti: Wasiliana na mtoa huduma za intaneti ili aitatue.

Ripoti tatizo

Ukiendelea kukabiliwa na hitilafu ya mtiririko wako mubashara, wasiliana na timu yetu.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
11799680709520495913
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false