Kuangalia vipimo vya mtiririko wako mubashara

Wakati unatiririsha mubashara kwenye YouTube, unaweza kuona utendaji wa mtiririko wako. Utapata vipimo tofauti kulingana na iwapo unatiririsha kutoka kwenye simu au programu ya kusimba.

Kwenye Ukurasa wa Kudhibiti Utiririshaji wa Moja kwa Moja

Unaweza kukagua ubora na takwimu za mtiririko wako ukitiririsha katika Ukurasa wa Kudhibiti Utiririshaji wa Moja kwa Moja. Kwenye dashibodi ya mtiririko wako, unaweza kuona:

Ubora wa mtiririko

Hali ya mtiririko: Hali ya mtiririko unajumuisha ujumbe kuhusu hitilafu mahususi pamoja na maagizo

Takwimu katika wakati halisi

  • Waliotazama wakati sawa: Idadi ya waliotazama kwa wakati mmoja. Idadi ya juu ya waliotazama wakati sawa ni idadi ya juu zaidi ya watazamaji katika mtiririko mubashara.
  • Kipindi: Muda ambao mtiririko wako ulidumu.
  • Mara za kupendwa: Jumla ya idadi ya watumiaji ambao wamependa mtiririko. Mara za kupendwa huhamishiwa kwenye kumbukumbu ya Mfumo wa Kufikia Video Unapohitaji (VOD) katika mtiririko mubashara.
  • Kiasi cha gumzo: Idadi ya ujumbe uliotumwa katika gumzo la moja kwa moja kwa dakika moja.
  • Mara za kutazamwa: Jumla ya mara ambazo mtiririko mubashara ulitazamwa.
  • Wastani wa kipindi cha kutazama: Makadirio ya wastani wa dakika zilizotumika kutazama kwa kila utazamaji wa mtiririko mubashara.

Takwimu za baada ya kutiririsha

Takwimu za baada ya kutiririsha

Unapokamilisha mtiririko mubashara, kuna muhtasari wa haraka wa vipimo vya mtiririko wako.

  • Mara za kutazamwa: Jumla ya mara ambazo mtiririko mubashara ulitazamwa.
  • Watu Wapya Wanaofuatilia: Idadi ya watumiaji ambao walianza kufuatilia kituo chako wakati wa mtiririko.
  • Jumla ya muda wa kutazama: Jumla ya muda ambao tukio lilichezwa kwa utazamaji wote.
  • Upeo wa wanaotazama kwa wakati mmoja: Idadi ya juu zaidi ya utazamaji wakati wa mtiririko.
  • Kipindi: Urefu wa muda ambao mtiririko ulionyeshwa mubashara.
  • Wastani wa kipindi cha kutazama: Makadirio ya wastani wa dakika zilizotumika kutazama kwa kila utazamaji wa mtiririko mubashara.
  • Maoni: Idadi na aina ya maoni yaliyotokea wakati wa mtiririko.

Kwenye Studio ya YouTube

Takwimu za kiwango cha video

  • Wastani wa watazamaji waliotazama kwa Wakati Mmoja: Idadi ya wastani ya watazamaji waliotazama mtiririko wako kwa wakati mmoja katika muda wowote.
  • Idadi ya Juu ya watazamaji waliotazama mtiririko kwa Wakati Mmoja: Idadi ya juu ya watazamaji waliotazama mtiririko wako katika muda wowote.
  • Matukio makuu ya muda wa kutazama: Jinsi matukio mbalimbali ya mtiririko wako yalivyowavutia watazamaji (yanapatikana katika ripoti ya matukio makuu ya muda wa kutazama)
  • Maoni: Idadi na aina ya maoni yaliyotokea wakati wa mtiririko.

Takwimu za kiwango cha chaneli

  • Wastani wa idadi ya waliotazama mtiririko kwa Wakati Mmoja: Idadi ya wastani ya watazamaji ambao walitazama mtiririko kwa wakati mmoja, ambao ulifanikiwa kuwavutia kwenye mitiririko yako yote.
  • Idadi ya Juu ya watazamaji waliotazama kwa Wakati Mmoja: Idadi ya juu ya watazamaji waliotazama mtiririko kwa wakati mmoja, ambao ulifanikiwa kuwavutia kwenye mitiririko yako yote.
  • Saa ambazo watazamaji wametiririsha: Jumla ya saa zilizotumika kutiririsha mubashara kuanzia kipindi x hadi y.

Kutoka kwenye Takwimu za YouTube

Katika Takwimu za YouTube unaweza kupanga kulingana na Mubashara, Unapohitaji au Mubashara na unapohitaji.

Chaguo za kupanga data ziko katika menyu kunjuzi ambayo 'Ni ya moja kwa moja na inapatikana unapohitaji' katika Takwimu za YouTube

Utapata Ripoti za Muda wa Kutazama kwa video mahususi au kwa chaneli, kama vile upakiaji wa mara kwa mara.

Ripoti zinajumuisha:

  • Muda wa Kutazama
  • Muda wa Kutazama
  • Demografia
  • Mahali Video Zinapochezewa
  • Vifaa na Vyanzo vya Watazamaji

Unaweza kupata maelezo zaidi kuhusu data inayopatikana katika ripoti ya Muda wa Kutazama.

Katika Mtiririko Mubashara unaweza kuangalia Idadi ya juu ya waliotazama kwa wakati mmoja na ujumbe wa gumzo. Ripoti za kiwango cha video na vipimo zinapatikana kwenye Takwimu za YouTube dakika chache baada ya mtiririko wako kukamilika. Unaweza kupakua data kama faili ya CSV.

Data katika Takwimu za YouTube inatokana na Utambulisho wa Video. Data huchakatwa na kuondolewa taka na hupima maelezo tofauti na unayopata katika Ukurasa wa Kudhibiti Utiririshaji wa Moja kwa Moja.

Pata maelezo zaidi kuhusu Kuripoti Super Chat.

Kumbuka: Ripoti za mawasiliano na mapato hazipatikani wakati wa kuchuja kwa ajili ya kuonyesha mubashara. Utapata ujumbe huu kuhusu hitilafu: "Data hii haipatikani kulingana na hali ya mubashara au unapohitaji. Tafadhali chagua 'Mubashara na unapohitaji' au badilisha na uangalie ripoti tofauti."

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
13195172996289768230
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false