Content ID kwa ajili ya washirika wa muziki

Vipengele vinavyofafanuliwa katika makala haya vinapatikana tu kwa washirika wanaotumia mifumo ya ulinganishaji wa Content ID katika YouTube.

Mfumo wa YouTube wa Content ID huwezesha washirika wa muziki kubaini na kudhibiti kwa urahisi muziki wao kwenye YouTube. YouTube huchanganua video zilizopakiwa na kuzilinganisha na hifadhidata ya muziki ambao umepakia. Maudhui katika video iliyopakiwa na mtumiaji yanapolingana na ya video unayomiliki, unapewa uamuzi wa kuchuma mapato kwenye video hiyo, kuizuia au kuifuatilia.

Ili utumie Content ID, unaunda vipengee katika mfumo wa usimamizi wa haki wa YouTube. Kila kipengee kinawakilisha sehemu ya mali ya uvumbuzi. Unaweza kuwasilisha aina nne za vipengee vya muziki:

YouTube pia hutambua uhusiano kati ya vipengee hivi. Kipengee cha Video ya Muziki kinaweza kupachika Kipengee cha Rekodi ya Sauti, na Rekodi ya Sauti inaweza kupachika Kipengee kimoja au zaidi cha Faili yenye Maelezo ya Umiliki wa Utungo.

Ili uunde vipengee, unapakia faili za maudhui na metadata yake inayohusiana ukitumia violezo vya lahajedwali. NI sharti uunde tu vipengee vya bidhaa ambazo unamiliki haki zake; kwa mfano, lebo za muziki hazipaswi kuunda Vipengee vya Faili zenye Maelezo ya Umiliki wa Utungo bila mkataba unaofaa, na wachapishaji wa muziki hawapaswi kuunda Vipengee vya Rekodi ya Sauti.

Kuunda kipengee cha rekodi ya sauti hakuundi Video ya Picha. Ili ufanye rekodi ipatikane kama Video ya Picha, ni sharti upakie rekodi ukitumia Lahajedwali la kupakia Video ya Picha au Mipasho ya DDEX ya YouTube Music.

Kutumia marejeleo yanayohusiana na vipengee, Content ID hubaini video zilizopakiwa na watumiaji zinazojumuisha kazi yako inayolindwa kwa hakimiliki na kufungua dai linaloonyesha umiliki wako wa maudhui ya ndani ya video.

Mojawapo ya vipengee vyako kinapodai umiliki wa video iliyopakiwa na mtumiaji, YouTube hutumia sera ya kipengee hicho kwenye video. Katika hali ambapo Kipengee cha Rekodi ya Sauti na Vipengee vyake vya Faili yenye Maelezo ya Umiliki wa Utungo vilivyopachikwa vina sera tofauti, YouTube hutumia sera zenye vikwazo vingi zaidi; angalia Jinsi sera zinavyotumika ili upate maelezo zaidi.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
3284591991150665367
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false