Weka mipangilio ya arifa ya barua pepe

Vipengele vinavyoangaziwa katika makala haya vinapatikana tu kwa watumiaji wa Kidhibiti Maudhui cha Studio ya YouTube. Ili ufahamu kuhusu arifa za YouTube kwa ujumla, pata maelezo zaidi hapa.

Unapoweka mipangilio ya Kidhibiti chako cha Maudhui, unahitaji kubainisha anayepaswa kuarifiwa kupitia barua pepe shughuli fulani inapofanyika kwenye akaunti. Kwa mfano, huenda mtumiaji fulani pekee akahitaji kuarifiwa dai linapopingwa. Weka mipangilio ya arifa za barua pepe:

  1. Ingia katika akaunti ya Kidhibiti Maudhui cha Studio.
  2. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Mipangilio .
  3. Katika sehemu ya Muhtasari kwenye ukurasa wa Arifa za barua pepe, weka anwani za barua pepe katika visanduku husika vya maandishi:
    • Arifa ya msingi: Anwani msingi za barua pepe za akaunti ya Kidhibiti Maudhui.
      • Arifa ya barua pepe hutumwa kunapotekelezwa shughuli za Kidhibiti Maudhui, ikijumuisha shughuli zilizotajwa hapa chini (mizozo kuhusu umiliki, madai na taarifa kuhusu kuondolewa kwa video).
      • Maelezo kuhusu akaunti ya mshirika, na arifa za ripoti zitatumwa pia kwa anwani hizi za barua pepe.
    • Arifa kuhusu mizozo: Arifa ya barua pepe hutumwa kunapokuwa na shughuli inayohusiana na umiliki wa vipengee.
    • Arifa kuhusu madai: Arifa ya barua pepe hutumwa kunapokuwa na madai na rufaa mpya.
    • Arifa kuhusu wahusika wengine: (hutumwa kwa washirika fulani pekee) Arifa ya barua pepe hutumwa kukiwa na taarifa kuhusu madai kutoka kwa wahusika wengine.

    • Arifa kuhusu ombi la kuondolewa kwa video: Arifa ya barua pepe hutumwa kukiwa na taarifa kuhusu ombi ulilowasilisha la kuondolewa kwa video.
Kidokezo: Ili uweke anwani moja ya barua pepe katika kisanduku cha maandishi, bonyeza enter baada ya kuweka ili uhifadhi. Ili uweke anwani kadhaa za barua pepe, zitenganishe kwa koma. Baada ya kuweka anwani ya mwisho ya barua pepe, bonyeza enter ili uhifadhi.
  1. Bofya HIFADHI.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
6791458546849364059
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false