Vidokezo kuhusu kuwa salama mtandaoni

Wizi wa data binafsi

Wizi wa data binafsi ni wakati ambapo mtu anahadaiwa ili kushiriki maelezo yake binafsi, kama vile nambari za kadi ya mikopo au data nyingine ya fedha. Kawaida, mdukuzi anapopata maelezo hayo, huyatumia kuiba pesa, mali au utambulisho wako.

Kumbuka, YouTube kamwe haitakuomba nenosiri, anwani ya barua pepe au maelezo mengine ya akaunti yako. Usidanganyike mtu apowasiliana nawe akijifanya kuwa ni mhudumu wa YouTube.

Ukipata video kwenye YouTube ambazo anaamini zinaweza kuwa taka au za wizi wa data binafsi, ziripoti ili zikaguliwe na timu na YouTube. Ili upate maelezo zaidi kuhusu taka na wizi wa data binafsi, tembelea Muungano wa Kitaifa wa Usalama wa Mtandaoni (National Cyber Security Alliance).

Ikiwa una wasiwasi kuwa huenda Akaunti yako ya Google imevamiwa, pata maelezo kuhusu jinsi ya kuimarisha usalama wa Akaunti ya Google iliyodukuliwa au kuvamiwa.

Usalama wa Akaunti

YouTube huchukua hatua madhubuti za usalama kulinda maelezo tunayohifadhi. Kwa maelezo zaidi, soma Sera ya Faragha ya Google.

Kumbuka kuwa ni jukumu lako kulinda usalama wa nenosiri lako. USIWAHI kushiriki nenosiri lako na wengine.

Dumisha usalama wa akaunti yako

Tumeunda orodha hakikishi ambayo ni rahisi kutumia ili kukusaidia kulinda kompyuta, kivinjari, Gmail, na Akaunti yako ya Google. Tunakuhimiza usome orodha hakikishi yote, lakini tungependa kuangazia hatua zifuatazo zinazoweza kukusaidia kumarisha usalama wa chaneli yako ya YouTube.
  • Weka nambari ya simu ya kurejesha akaunti, na anwani mbadala ya barua pepe kwenye Akaunti yako ya Google. Bila nambari ya simu na anwani salama ya barua pepe, mtu anaweza kuingia katika akaunti yako kwa kujua au kukisia swali lako la usalama. Unaweza kusasisha maelezo ya usalama hapa.
  • Sasisha na udumishe usalama wa maelezo yako ya kurejesha akaunti.
  • Unda nenosiri la kipekee na thabiti kwa Akaunti yako ya Google (na usitumie kitambulisho chako cha kuingia na nenosiri lako katika tovuti zingine). Vifuatavyo ni baadhi ya vidokezo vya kukusaidia kuunda nenosiri dhabiti:
    • Nenosiri lako linapaswa kuwa la angalau herufi nane, changanya nambari na herufi, na usiweke maneno ya kawaida.
    • Chagua neno au ufupisho na ujumuishe nambari katikati ya baadhi ya herufi.
    • Weka alama za uakifishaji.
    • Changanya herufi kubwa na ndogo.
    • Usitumie nenosiri ambalo umetumia katika akaunti nyingine.
    • Ikiwa akaunti yako ni ya kampuni au shirika, badilisha nenosiri na maelezo ya kurejesha akaunti mhudumu anapoacha kufanya kazi kwenye kampuni yako.

Ikiwa unaamini kuwa akaunti yako imevamiwa, unaweza kuripoti hapa.

Pata maelezo kuhusu jinsi ya kuepuka na kuripoti matukio ya ulaghai kwenye Google.

Kituo cha Usalama cha Google

Elewa data yako iliyo kwenye Google na kwenye wavuti. Soma baadhi ya ushauri na vidokezo vya kudhibiti data yako na kuwa salama mtandaoni.

Mtaala wa Uanateknolojia Mwema wa Google

Mtaala wa Uanateknolojia Mwema wa Google (Google Digital Citizenship Curriculum) ni mtaala rahisi na shirikishi unaolenga walimu na wanafunzi wa shule za sekondari. Kupitia masomo kadhaa mafupi, pata maelezo kuhusu faragha, sera na jinsi ya kuwa mwanateknolojia mwema.

Kituo cha Usalama wa Familia cha Google

Kituo cha Usalama wa Familia cha Google kina vidokezo na ushauri wa kulinda usalama wa familia yako mtandaoni.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
17918065626046326876
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false