Kufungwa kwa chaneli au akaunti

Ikiwa chaneli yako imefungwa, utapokea barua pepe inayoeleza sababu ya kufungwa. Ikiwa chaneli yako ya YouTube imefungwa, huruhusiwi kukwepa kufungwa huko au kuruhusu watu wengine watumie chaneli yako ili kukwepa kufungwa kwa chaneli zao, kwa kutumia au kufungua chaneli zingine za YouTube.

Masharti haya yanatumika kwenye chaneli zako zote zilizopo, chaneli zozote mpya unazofungua au kununua na chaneli zozote ambako unaangaziwa sana au mara kwa mara.

Wanaoshiriki katika Mpango wa Washirika wa YouTube hawana tena haki ya kuchuma mapato yoyote ikiwa chaneli zao zimefungwa. Huenda pia tukazuia mapato ambayo hayajalipwa na kuwarejeshea watangazaji au watazamaji pesa walizotumia kwa ununuzi, inapofaa na inapowezekana.

Kufungwa kutokana na ukiukaji wa Mwongozo wa Jumuiya

Sababu zinazoweza kufanya chaneli au akaunti zifungwe:

Unaweza kuarifiwa kuhusu kufungwa kwa chaneli kupitia barua pepe inayohusu kufungwa kwa chaneli au ufahamishwe unapoingia katika akaunti ya Studio ya YouTube. Katika tukio la kufungwa kwa chaneli, utapoteza uwezo wa kufikia Dashibodi yako ya Studio na vipengele vingine. Bado unaweza kuingia katika akaunti ya Studio ya YouTube ili ukague taarifa kuhusu kufungwa kwa akaunti.

Kukata rufaa dhidi ya kufungwa kwa chaneli kwa kukiuka Mwongozo wa Jumuiya

Kukata rufaa kwenye kifaa cha mkononi

Iwapo unaamini kuwa chaneli au akaunti yako ilifungwa kimakosa, unaweza kukata rufaa hapa.

Kukata rufaa kwenye kompyuta

  1. Fungua Studio ya YouTube.

    1. Kumbuka: Unaweza kuombwa uthibitishe upya wakati unaingia katika akaunti.
  2. Chini ya taarifa za kufungwa kwa chaneli, bofya Anza Kukagua.
  3. Kagua sababu ya kufungwa.
  4. Bofya Endelea.
  5. Chagua Anza Kukata Rufaa.
  6. Bofya Endelea.
  7. Toa anwani yako ya barua pepe na ueleze sababu yako ya kukata rufaa.
  8. Bofya Wasilisha.

Kuangalia hali ya kukata rufaa dhidi ya kufungwa kwa chaneli

  1. Fungua Studio ya YouTube.
  2. Angalia uthibitisho wa uwasilishaji wa rufaa yako na uangalie muda wa ukaguzi wa rufaa yako unaotarajiwa.

Utaarifiwa kupitia barua pepe kuhusu matokeo ya rufaa yako. Rufaa yako ikikubaliwa, utaelekezwa urudi kwenye dashibodi yako ya Studio ya YouTube. Rufaa yako ikikataliwa, utaondolewa kwenye akaunti pindi tu utakapokubali uamuzi.

Kufungwa kutokana na ukiukaji wa hakimiliki

Ikiwa chaneli yako imefungwa kwa sababu ya madai ya ukiukaji wa hakimiliki na unafikiri kuwa madai hayo si sahihi, unaweza kuwasilisha arifa ya kukanusha. Mchakato huu bado unapatikana kwa watayarishi wenye chaneli zilizofungwa, lakini hawataweza kufikia fomu ya wavuti ya kuwasilisha arifa ya kukanusha. Unaweza pia kuwasilisha arifa ya kukanusha kwa njia ya barua pepe, faksi, au barua ya posta.

Kwa maelezo zaidi kuhusu mchakato wa kuwasilisha arifa ya kukanusha, nenda kwenye Kituo cha Hakimiliki.

Kumbuka: Kuwasilisha arifa ya kukanusha huanzisha mchakato wa kisheria.

Kupakua data ya chaneli iliyofungwa

Ikiwa chaneli yako imefungwa, huwezi tena kupakua maudhui yako ya YouTube. Hata hivyo, unadumisha uwezo wa kupakua data yako ya Google. Pata maelezo kuhusu jinsi ya kupakua data yako ya Google.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
3220981701537594874
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false