Kuripoti video, vituo na maudhui mengine ambayo hayafai kwenye YouTube

Tunategemea wanachama wa jumuiya ya YouTube waripoti maudhui ambayo wanaona kuwa hayafai. Utambulisho wako hufichwa wakati wa kuripoti maudhui, kwa hivyo watumiaji wengine hawawezi kufahamu aliyeripoti.

Je, nini hufanyika baada ya mimi kuripoti maudhui?

Maudhui yanaporipotiwa, hayaondolewi kiotomatiki. Maudhui yaliyoripotiwa hukaguliwa kwa kufuata mwongozo huu:

Ili uangalie ikiwa video uliyoripoti imeondolewa, unaweza kuangalia Historia yako ya kuripoti.

Fuatilia chaneli ya Watazamaji ya YouTube ili upate habari, taarifa na vidokezo vipya.

Jinsi ya kuripoti maudhui

Kuripoti video

YouTube hukagua video zilizoripotiwa saa 24 kwa siku, siku 7 za wiki. Video inaweza kuripotiwa wakati wowote baada ya kupakiwa kwenye YouTube. Ikiwa timu yetu ya ukaguzi haitapata ukiukaji wowote, hakuna kiasi cha ripoti kitakachobadilisha hilo na video itaendelea kuwepo kwenye tovuti yetu.

  1. Ingia katika akaunti ya YouTube.
  2. Nenda kwenye video ambayo ungependa kuripoti.
  3. Chini ya video, bofya Zaidi 더보기 kisha Ripoti .
  4. Chagua sababu inayoeleza vyema zaidi ukiukaji ulio kwenye video.
  5. Bofya INAYOFUATA.
  6. Toa maelezo yoyote ya ziada ambayo yanaweza kusaidia timu ya ukaguzi kufanya uamuzi wake. Jumuisha mihuri ya wakati au maelezo ya ukiukaji, ikiwezekana.
  7. Bofya RIPOTI.

Kumbuka: Ili uangalie hali ya video unayoripoti, tembelea historia yako ya Kuripoti. Pata maelezo zaidi kuhusu historia yako ya Kuripoti.

Ripoti Video fupi

YouTube hukagua video zilizoripotiwa saa 24 kwa siku, siku 7 za wiki. Video inaweza kuripotiwa wakati wowote baada ya kupakiwa kwenye YouTube. Ikiwa timu yetu ya ukaguzi haitapata ukiukaji wowote, hakuna kiasi cha ripoti kitakachobadilisha hilo na video itaendelea kuwepo kwenye tovuti yetu.
Unaweza kuripoti Video Fupi za YouTube kutoka kwenye Kichezaji cha Video Fupi.
  1. Ingia katika akaunti kwenye YouTube.
  2. Nenda kwenye Video fupi ambayo ungependa kuripoti.
  3. Katika kona ya chini kulia, bofya Zaidi  kisha Ripoti .
  4. Chagua sababu inayoeleza vyema zaidi ukiukaji ulio kwenye video.
  5. Bofya Inayofuata.
  6. Toa maelezo yoyote ya ziada ambayo yanaweza kusaidia timu ya ukaguzi kufanya uamuzi wake. Jumuisha mihuri ya wakati au maelezo ya ukiukaji, ikiwezekana.
  7. Bofya RIPOTI.
Kumbuka: Ili uangalie hali ya video unayoripoti, kwenye kompyuta, tembelea historia yako ya Kuripoti. Pata maelezo zaidi kuhusu historia yako ya Kuripoti.

Ripoti kituo

Unaweza kuripoti watumiaji, picha za mandharinyuma zisizofaa au ishara za wasifu zisizofaa.

  1. Ingia katika akaunti kwenye YouTube.
  2. Nenda kwenye ukurasa wa chaneli ambao ungependa kuripoti.
  3. Katika sehemu ya juu, bofya KUHUSU.
  4. Bofya Ripoti mtumiaji .
  5. Teua chaguo linalofaa zaidi linaloeleza kwa nini ungependa kuripoti kituo:
    • Ripoti sanaa ya chaneli
    • Ripoti picha ya wasifu
    • Ripoti mtumiaji
  6. Si lazima: Dirisha litakalofunguka linaweza kukuomba uweke maelezo zaidi. Weka maelezo mengine yoyote ambayo ungependa kushiriki.
  7. Bofya WASILISHA.

Kumbuka: Unaporipoti kituo, hatuhakiki video za kituo. Tunatumia video ambazo unaweza kuambatisha kwenye ripoti yako ili uelewe zaidi kuhusu kituo, lakini hatukagui video kwa ajili ya ukiukaji. Vipengele vya kituo ambavyo tunakagua vinajumuisha, lakini si tu, picha ya wasifu, kitambulishi na maelezo ya kituo. Ikiwa unafikiri kuwa video mahususi za kituo zinakiuka sera zetu, unapaswa kuripoti video mahususi.

Ripoti orodha ya kucheza

Unaweza kuripoti orodha ya kucheza ikiwa maudhui, kichwa, maelezo au lebo zinakiuka Mwongozo wetu wa Jumuiya.
  1. Ingia katika akaunti kwenye YouTube.
  2. Nenda kwenye orodha ya kucheza ambayo ungependa kuripoti.
  3. Chini ya mada ya orodha ya kucheza, bofya Zaidi 더보기 kisha Ripoti orodha ya kucheza .
  4. Bofya WASILISHA.

Ripoti kijipicha

Unaweza kuripoti kijipicha cha video kinachokiuka Mwongozo wetu wa Jumuiya.
  1. Ingia katika akaunti ya YouTube.
  2. Tafuta video ambayo ungependa kuripoti katika ukurasa wako wa kwanza, kwenye video zilizopendekezwa au katika matokeo ya utafutaji. Huwezi kuripoti kijipicha kwenye ukurasa wa kutazama wa video.
  3. Katika sehemu ya chini ya kijipicha, bofya Zaidi '' kisha Ripoti .
  4. Chagua sababu inayoeleza ni kwa nini ungependa kuripoti kijipicha.
  5. Bofya RIPOTI.

Ripoti kiungo katika maelezo ya video

Kwenye kompyuta, unaweza kuripoti kiungo kwenye maelezo kinachokiuka Mwongozo wetu wa Jumuiya.
  1. Ingia katika akaunti kwenye YouTube.
  2. Nenda kwenye video iliyo na kiungo katika maelezo, ambacho ungependa kuripoti.
  3. Chini ya video, bofya Zaidi  kisha Ripoti .
  4. Chagua sera ambayo inakiukwa na kiungo.
  5. Teua kisanduku karibu na Hali hii inatumika kwenye viungo vilivyo ndani ya maelezo ya video.
  6. Bofya INAYOFUATA.
  7. Toa maelezo yoyote ya ziada ambayo yanaweza kusaidia timu ya ukaguzi kufanya uamuzi wake. Jumuisha maelezo ya ukiukaji, ikiwezekana.
  8. Bofya RIPOTI.
Ripoti maoni
  1. Ingia katika akaunti kwenye YouTube.
  2. Nenda kwenye video na maoni ambayo ungependa kuripoti.
  3. Karibu na maoni, bofya Zaidi '' kisha Ripoti .
  4. Chagua sababu inayoeleza ni kwa nini ungependa kuripoti maudhui.
  5. Bofya RIPOTI.
  6. Si lazima: Kama Mtayarishi, baada ya kuripoti maoni, unaweza kuzuia maoni ya mtu huyo yasionyeshwe kwenye kituo chako. Teua kisanduku kando ya Mfiche mtumiaji kwenye kituo changu kisha bofya SAWA.

Maoni yangu yaliwekewa alama kuwa ni taka kimakosa

Iwapo unaamini kuwa maoni yako yaliwekewa alama kuwa ni taka kimakosa, unaweza kuwasiliana na aliyepakia kisha kumwomba arejeshe maoni yako.

Ripoti ujumbe wa gumzo la moja kwa moja

Wanachama wa Jumuiya wanaweza kuripoti ujumbe usiofaa ulioachwa kwenye mitiririko mubashara.

  1. Ingia katika akaunti kwenye YouTube.
  2. Nenda kwenye mtiririko mubashara na ujumbe ambao ungependa kuripoti.
  3. Elekeza kwenye ujumbe ambao ungependa kuripoti.
  4. karibu na ujumbe,  bofya Zaidi '' kisha Ripoti .
  5. Chagua sababu inayoeleza vyema zaidi kwa nini ungependa kuripoti ujumbe.
  6. Bofya RIPOTI.
Ripoti tangazo

Iwapo utapata tangazo lisilofaa au linalokiuka Sera za Google Ads, unaweza kuliripoti. Jaza kisha utume fomu hii.

Ili uripoti tangazo kwenye video:

  1. Bofya Maelezo kwenye tangazo.
  2. Chagua Ripoti tangazo.
  3. Jaza kisha uwasilishe fomu. Timu yetu itakagua ripoti yako ya tangazo na itachukua hatua ikiwa inafaa.

Kumbuka: Unaweza tu kuripoti matangazo kwenye YouTube ya kifaa cha mkononi au katika kompyuta.

Kuripoti maudhui kwenye YouTube katika TV yako

Unaweza kuripoti video moja kwa moja kwenye programu ya YouTube TV.

  1. Fungua programu ya YouTube .
  2. Nenda kwenye video ambayo ungependa kuripoti.
  3. Nenda kwenye Mipangilio kisha Ripoti.
  4. Chagua sababu ya kuripoti video.
  5. Baada ya kuchagua sababu, ujumbe wa uthibitishaji utaonekana.

Chaguo zingine za kuripoti

Ikiwa mchakato wa kuripoti haubainishi kikamilifu suala lako, tuna mifumo mingine unayoweza kutumia.

Kuripoti kuhusu faragha

Ili utume malalamiko kuhusu faragha, anzisha utaratibu wa kuwasilisha malalamiko kuhusu faragha. Tunaheshimu faragha yako kila wakati katika mchakato.
Kuripoti suala la kisheria
Ili uripoti suala la kisheria kwa niaba yako au mteja wako:
  1. Nenda kwenye maudhui au kituo unachotaka kuripoti.
  2. Chini ya maudhui au kituo, bofya Zaidi kisha Ripoti .
  3. Kwenye orodha itakayoonekana, bofya Suala la kisheria.
  4. Chagua suala husika. Ikiwa suala lako halijabainishwa, bofya Suala lingine la kisheria.
  5. Katika sehemu ya chini, bofya ENDELEA.
  6. Jaza fomu na uitume.
Ili kuharakisha uwezo wetu wa kuchunguza dai lako, tunakuhimiza utume dai lako kupitia fomu yetu ya wavuti badala ya faksi au posta.
Kumbuka kwamba matumizi mabaya ya fomu zetu za kisheria yanaweza kusababisha kufungwa kwa Akaunti yako ya Google.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
15496993451346300446
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false